SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Nov 23, 2014

MESSI APIGA HAT TRICK BARCELONA IKIICHAPA SEVILLA 5-1, AFIKISHA MABAO 252

Wachezaji wa Barcelona walilazimika kumbeba nahodha wao,Lionel Messi baada ya kufunga bao la tatu, hat trick na kuisaidia Barca kuitwanga Sevilla kwa mabao 5-1. Katika mechi hiyo ya La Liga iliyopigwa kwenye Uwanja wa Camp Nou, Messi alionyesha kuvunja rekodi iliyowekwa na Telmo Zarra. Nyota huyo wa zamani wa Athletic Bilbao aliyetamba kati ya mwaka 1940 na 1955 alimaliza La Liga akiwa amefunga mabao 251. Kwa mabao matatu ya Messi dhidi ya Sevilla, amefanikiwa kufikisha 252 na pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye mabao mengi zaidi La Liga akiwa na miaka 27 tu.

Nov 22, 2014

MAN UNITED 'WAJILIA RAHA' KWA ARSENAL, WAWACHAPA 2-1 EMIRATES.

MANCHESTER United imeendeleza ubabe dhidi ya Arenal, baada ya usiku huu kuichapa mabao 2-1 Uwanja wa Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. United walipata bao la kwanza dakika ya 56, baada ya beki Kieran Gibbs kumfunga mwenyewe kipa wake, Wojciech Szczesny katika harakati za kuokoa krosi ya Antonio Valencia, kabla ya Nahodha Wayne Rooney kufunga la pili dakika ya 85 akimalizia pasi ya Angel di Maria. Olivier Giroud aliifungia Arsenal la kufutia machozi dakika ya 90. Beki wa United, Luke Shaw alitolewa nje dakika ya 16 baada ya kuumia kifundo cha mguu, wakati kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere alinusurika kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Marouane Fellaini. Lakini kiungo huyo wa England alitolewa nje dakika ya 55 baada ya kuumia pia. Kipa Szczesny pia alitolewa uwanjani baada ya kuumia. Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny/Martinez dk59, Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Ramsey/Giroud dk77, Arteta, Wilshere/Cazorla dk55, Oxlade-Chamberlain, Welbeck na Sanchez Manchester United; De Gea, Smalling, McNair, Blackett, Valencia, Carrick, Fellaini, Di Maria, Shaw/Young dk16/Fletcher dk89, Rooney na Van Persie/James Wilson dk75. Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney (kulia) akishangilia baada ya Kieran Gibbs kujifunga Woljciech Szczesny na Kieran Gibbs wa Arsenal wakipamiana kabla ya kujifunga PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2837001/Arsenal-vs-Manchester-United-Team-news-kick-time-probable-line-ups-odds-stats-Premier-League-clash.html#ixzz3JpEIaEU5

Make Money at : http://bit.ly/copy_win

MAN UNITED 'WAJILIA RAHA' KWA ARSENAL, WAWACHAPA 2-1 EMIRATES.

MAN UNITED 'WAJILIA RAHA' KWA ARSENAL, WAWACHAPA 2-1 EMIRATES. MANCHESTER United imeendeleza ubabe dhidi ya Arenal, baada ya usiku huu kuichapa mabao 2-1 Uwanja wa Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. United walipata bao la kwanza dakika ya 56, baada ya beki Kieran Gibbs kumfunga mwenyewe kipa wake, Wojciech Szczesny katika harakati za kuokoa krosi ya Antonio Valencia, kabla ya Nahodha Wayne Rooney kufunga la pili dakika ya 85 akimalizia pasi ya Angel di Maria. Olivier Giroud aliifungia Arsenal la kufutia machozi dakika ya 90. Beki wa United, Luke Shaw alitolewa nje dakika ya 16 baada ya kuumia kifundo cha mguu, wakati kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere alinusurika kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Marouane Fellaini. Lakini kiungo huyo wa England alitolewa nje dakika ya 55 baada ya kuumia pia. Kipa Szczesny pia alitolewa uwanjani baada ya kuumia. Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny/Martinez dk59, Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Ramsey/Giroud dk77, Arteta, Wilshere/Cazorla dk55, Oxlade-Chamberlain, Welbeck na Sanchez Manchester United; De Gea, Smalling, McNair, Blackett, Valencia, Carrick, Fellaini, Di Maria, Shaw/Young dk16/Fletcher dk89, Rooney na Van Persie/James Wilson dk75. Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney (kulia) akishangilia baada ya Kieran Gibbs kujifunga Woljciech Szczesny na Kieran Gibbs wa Arsenal wakipamiana kabla ya kujifunga PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2837001/Arsenal-vs-Manchester-United-Team-news-kick-time-probable-line-ups-odds-stats-Premier-League-clash.html#ixzz3JpEIaEU5

Make Money at : http://bit.ly/copy_win

Nov 21, 2014

ARSENAL NI VIBONDE WA 'KUPIKA NA KUPAKUA' KWA MAN UNITED, MECHI 11 ZILIZOPITA WAMESHNDA MOJA TU


REKODI YAO YA KWENYE LIGI TANGU 2009

Mechi walizocheza: 11 
Man United walizoshinda: 7 
Arsenal waliyoshinda: 1
Walizotoka sare: 
MECHI kati ya Arsenal dhidi ya Manchester United wakati wote imekuwa moja ya michezo ya kusisimua katika historia ya  Ligi Kuu ya England – lakini The Gunners wameshinda mechi moja tu kati ya 11 zilizopita baina ya klabu hizo.
Louis van Gaal atasafiri na kikosi chake chenye majeruhi kibao hadi Uwanja wa Emirates Jumamosi mchana akitambua kwamba timu yake imekuwa na historia nzuri siku za karibuni dhidi ya wapinzani wake hao.
Licha ya kuboronga msimu uliopita, lakini bado United ilijimudu kuichapa Arsenal 1-0 Uwanja wa Old Trafford na kutoka nayo sare ya bila kufungana katika mchezo mwingine Kaskazini mwa London.
Aaron Ramsey scored the only goal of the game the last time Arsenal beat Manchester United in 2011
Aaron Ramsey alifunga bao pekee mara ya mwisho Arsenal ilipoifunga Manchester United mwaka 2011
Arsenal beat Manchester United 1-0 in 2011 - their only win in the last 11 games against United
Arsenal iliifunga Manchester United 1-0 mwaka 2011 - ushindi wao pekee katika mechi 11 dhidi ya United
Danny Welbeck - who is now at Arsenal - scored the last time Manchester United won at the Emirates in 2012
Danny Welbeck - ambaye kwa sasa yupo Arsenal - alifunga bao la ushindi dakika ya mwisho Manchester United ikishinda Uwanja wa Emirates mwaka 2012
Former Arsenal striker Robin van Persie scored the winner for United at Old Trafford last season
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Robin van Persie alifunga bao la ushindi kwa United Uwanja wa Old Trafford msimu uliopita

MECHI BAINA YA ARSENAL NA MAN UTD
Feb 12, 2014Arsenal0-0Man Utd
Nov 10, 2013Man Utd1-0Arsenal
Apr 28, 2013Arsenal1-1Man Utd
Nov 3, 2012Man Utd  2-1Arsenal
Jan 22, 2012Arsenal1-2Man Utd
Ago 28, 2011Man Utd8-2Arsenal
May 1, 2011Arsenal1-0Man Utd
Dec 13, 2010Man Utd1-0Arsenal
Jan 31, 2010Arsenal1-3Man Utd
Ago 29, 2009Man Utd2-1Arsenal
May 16, 2009Man Utd0-0Arsenal

Wakati kocha Sir Alex Ferguson akiwa katika msimu wake wa mwisho Old Trafford, mabao ya Robin van Persie na Patrice Evra yaliipa United ushindi wa 2-1 nyumbani wakati Van Persie pia alifunga tena dhidi ya Arsenal aliporejea Emirates baadaye msimu huo kusawazisha baada ya Theo Walcott kuanza kufunga na kufanya sare ya 1-1.
Ushindi wa mwisho wa Arsenal katika Ligi Kuu ya England dhidi ya United ulikuwa Mei mwaka 2011 wakati Aaron Ramsey alipofunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 nyumbani.
Kutoka kwenye kikosi cha Arsenal wakati huo, wachezaji watano bado wapo klabuni, akiwemo kipa Wojciech Szczesny, Laurent Koscielny, Walcott, Ramsey na Jack Wilshere.
Lakini ikiwa Wenger anatafuta ahueni anahitaji kutazama juu ya rekodi ya ugenini ya United, bado hawajashinda mechi yoyote ugenini msimu huu na hawajachukua pointi tatu katika mechi zao za ugenini tangu Aprili 5, mwaka huu walipoifunga Newcastle 4-0.
Misimu iliyopita, mechi kati ya Arsenal vs Manchester United ilikuwa ya kuamua bingwa, lakini mwaka huu inaonekana kama ni mechi ya kuwania nafasi ya nne na ya mwisho ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini kikubwa zaidi, The Gunners wanatarajiwa kufuta uteja wao kwa United.

KIPA WA SIMBA SC APATA ULAJI OMAN, AWA BOSI WA KIPA WA YANGA SC.


Kipa wa zamani wa Simba SC, Spear Mbwembwe (kulia) akiwa na kipa wa zamani wa Yanga SC, Juma Mpongo mjini Muscat, Oman jana. Mbwembwe ametua jana kwa ajili ya kuwa kocha wa makipa wa klabu ya Seeb ya Ligi Kuu ya nchini humo. Mpongo amekuwa kipa wa timu hiyo tangu mwanzoni mwa msimu huu na sasa bosi wake atakuwa Mtanzania mwenzake.

MUONEKANO WA JEZI MPYA ZINAZOPIGIWA KURA


JEZI ZA NYUMBANI

N1
N1
B
B
C
C
D
D
(Imetolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, TFF )

Nov 20, 2014

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

GHANA YAAMKA, YAICHAPA TOGO YA ADEBAYOR 3-1, YAFUZU AFCON

Pamoja na kucheza bila Gyan Asamoh na Andre Ayew Ghana imefanikiwa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).
Black Star imefanikiwa kufuzu kwa kuichapa Togo iliyoongozwa na Emmanuel Adebayor iliyokuwa ugenini kwa mabao 3-1, leo.
Kutokana na ushindi huo, Ghana imefikisha pointi 11 na kufuzu katika michuano hiyo mikubwa ya soka Afrika kwa timiu za taifa.
Ghana ilionekana kuizidia Togo kwa kila kitu huku safu ya ushambuliaji ya Ghana ikiichachafya safu ya ulinzi ya wageni.

Nov 14, 2014

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

.
DSC05567
.
.

ANGALIA PICHA ZA TASWIRA NNE ZA DAVID MOYES AKIWA KATIKA KAZI YAKE


KOCHA DAVID MOYES AKIWA AMEANZA RASMI KWA MARA YA KWANZA KUKINOA KIKOSI CHAKE KIPYA CHA REAL SOCIEDAD CHA HISPANIA. KOCHA HUYO WA ZAMANI WA MAN UNITED AMEANZA KAZI MPYA BAADA YA KUTIMULIWA NA MASHETANI HAO NA NAFASI YAKE KUCHUKULIWA NA LOUIS VAN GAAL AMBAYE HATA HIVYO BADO HAJAKAA VIZURI. MOYES AMESAINI MKATABA WA MIEZI 18 KUINOA TIMU HIYO YA HISPANIA

Nov 13, 2014

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI




.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Nov 12, 2014

WASANII WA TANZANIA WAMUOMBEA RAIS JAKAYA KIKWETE.

Staa wa muziki wa Bongo fleva Nasib 'Abdul Diamond'.

SIKU chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanyiwa pasuaji wa tezi dume (prostrate), mastaa mbalimbali wameguswa na kuunganisha nguvu ya pamoja kumfanyia maombi mazito kiongozi huyo wa nchi ili aweze kupona haraka.Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji huo Novemba 8, mwaka huu katika Hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, mastaa wamesema wameguswa na kuumwa huko kwa rais lakini wameshukuru kwamba upasuaji umefanyika salama hivyo wanamuombea apone haraka ili aweze kurudi katika afya yake ya kawaida.
“Mungu asaidie upone haraka baba…tunaumwa nawe,” aliandika Aman Temba ‘Mh. Temba’ mtandaoni huku Esterlina Sanga ‘Linah’ akiandika:“Furaha ya moyo wangu inakamilika na mengi lakini kubwa kuliko yote ni kuona tabasamu lenye afya na uzima tele kwako baba, shujaa rais wangu. Get well soon my shujaa.”
Staa wa filamu Bongo, Jackline Wolper.
Mbali na wasanii hao, wengine walioonesha kuguswa na kuumwa kwa rais na kuandika hisia zao ni Diamond, Linex, Wolper, Shetta, Shilole na MwanaFa.
Mbali na wasanii wananchi mbalimbali wa kawaida kwa nyakati tofauti walieleza hisia zao kupitia gazeti hili:
“Nilipopata tu taarifa kwamba mheshimiwa rais amefanyiwa upasuaji, nilishtuka kidogo lakini baada ya hapo mimi pamoja na wenzangu tukafanya maombi maalumu ya kumuombea rais wetu aweze kupona haraka na kuendelea na majukumu yake ya kawaida.
Msanii wa Bongo Fleva, Shetta.
“Niwaombe Watanzania wote tuungane kwa pamoja kumuombea rais wetu maana maombi yetu yana maana kubwa mbele za Mungu,” alisema Mazula, mkazi wa Tabata.
Tezi dume ni nini?
Tezi dume ipo kwa binadamu wa kiume ambapo ina muonekano kama wa yai (oval shape) na upana wake huwa ni CM4 na unene CM3 ingawa kwa mujibu wa madaktari, vipimo hivyo vinatofautiana kwa kila mwanaume.
Estelina Sanga 'Linah'.
Tezi dume inazunguka shingo ya kibofu cha mkojo na kuzunguka mrija unaopeleka mkojo nje, kwa kawaida tezi hii ina umbo la wastani na huongezeka ukubwa kadri umri wa mtu unavyozidi kuongezeka.

CAF yahaha kutafuta mbadala wa Morocco.


Shirikisho la kanda kanda barani Africa CAF linaendelea kuchambua ni nchi gani itakayookoa jahazi ya kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 baada ya kuthibitisha Morocco kuondolewa rasmi kuandaa fainali hizo.
Nchi ya Morocco imeondolewa kutokana na kukataa kuwa mwenyeji ya mashindano hayo mwakani kwa hofu ya ugonjwa wa Ebola.
Mwandishi wa habari anasema fainali hizo zinaweza sasa kupelekwa Angola nchi iliyokuwa mwenyeji wa fainali hizo miaka minne iliyopita.
Nchi nyingine zinazodhaniwa kuweza kuandaa mashandano hayo ni Gabon na Nigeria. Shirikisho la kanda kanda barani Afrika linasema litatoa uamuzi ni nchi ipi itakayoandaa mashindano hayo haraka iwezekanavyo.

Lewis Hamilton atang'ara Abu Dhabi

                             Lewis Hamilton

Nguli wa zamani wa dunia wa mbio za magari Nigel Mansell amesema Lui Hamilton anayo nafasi moja iliyosalia kufanya vyema na kutinga fainali huko Abu Dhabi November 23.
Katika mahojiano maalumu na BBC Radio 5 Mansell anasema nafasi ya ushindi iko wazi mbele ya Lui na sasa ni uamuzi wake kuamua kushindwa ama kushinda!
Hamilton anaiongoza timu ya Mercedes kwa pointi 17, na nafasi ya kufanya maajabu anayo mikononi mwake.
Awali ni awali ,mwaka 1986 huko Australia kwenye
Mbio za Langa langa zilishuhudia William akiukosa ushindi hivi hivi baada ya kupata pancha . lakini yeye anasema hana tofauti na bata, mzoefu wa kupata,!
Alisahau maumivu ya tairi kukosa upepo na kuukosa ushindi pale alipojiona ana bahati ya mtende kuota jangwani baada ya kupata tuzo ya Sports Personality of the Year zitolewazo na BBC kakosa huku kapata kule!
Kama wewe ni shabiki sugu wa michezo!Tuzo hizo zimewadia tena ingia katika mtandao wa BBCSWAHILI.COM utapata maelekezo ya namna ya kupiga kura kumchagua mchezaji umtakaye, akwae tuzo hiyo ya BBC SPORTS PERSONALITY OF THE YEAR, na Mshindi atatangazwa baadaye mwezi ujao kazi kwako

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

.
.
.
.