Jan 31, 2015
LIVERPOOL YATAKATA EPL
11:15 PM
Mshambuliaji Daniel Sturridge amerejea kwa kishindo kutoka kwenye maumivu yake baada ya kuifungia timu yake ya Liverpool bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham United Uwanja wa Anfield jioni ya leo.
Raheem steling aliifungia liverpool goli la kuongoza dakika 51 kabla ya Sturridge ailiye tokea bench kuchukua nafasi ya Lazar Markovic dakika ya 68 na kufunga bao dakika ya 80.
Daniel Sturridge akishangilia baada ya kuifungia timu yake ya Liverpool goli la pili dhidi ya West Ham United katika ushindi wa 2-0
Raheem steling aliifungia liverpool goli la kuongoza dakika 51 kabla ya Sturridge ailiye tokea bench kuchukua nafasi ya Lazar Markovic dakika ya 68 na kufunga bao dakika ya 80.
Daniel Sturridge akishangilia baada ya kuifungia timu yake ya Liverpool goli la pili dhidi ya West Ham United katika ushindi wa 2-0
FULL TIME; STAMFORD BRIDGE
10:31 PM
Chelsea imetoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Man city katika uwanja wa njumbani Stamford bridge Chelsea ili wali kuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wake Remmy dakika ya 41dakika chache baadae David silva
CONGO DR YAFUZU NUSU FAINALI KOMBE LA MATAIFA AFRIKA
10:02 PM
DR Congo ilitoka nyuma na kuishinda Congo kwa mabao 4-2 na kufika katika semi fainali ya mechi za kombe la Afrika.
Congo DR ilitoka nyuma 2-0 na kuishinda Congo katika mechi iliokuwa na kasi na mchezo mzuri kutoka pande zote mbili.Ferebory Dore alifunga krosi safi huku Thievy Bifouma akifanya mabao kuwa 2-0.
Katika dakika ya 16 Diermerci Mbokani alifunga bao la kwanza ,kabla ya Bolika kufunga bao la pili naye Joel Kimuaki akafunga bao la tatu.
Mbokani aliwazunguka tena mabeki wa Congo na kufunga bao la nne na la ushindi katika shambulizi la ghafla.
DOMAYO AIBEBE AZAM FC CONGO
9:45 PM
Timu ya Azam fc imetoka sare ya 2-2 dhidi ya Zesco united magoli ya Azam fc yamefungwa na kiungu Frank domayo habari kutoka katika mtandao wa Azam unasema kuwa mechi ilikuwa nzuri sana kipimo sahihi kwa mechi za CAF Champions league, Mwalimu ameona mapungufu, atayafanyia kazi. Mechi ya Awali TP Mazembe 3-1 Don Bosco
Azam FC itacheza mechi ya mwisho dhidi ya Don Bosco Jumanne tarehe 3/2/2015
NAHODHA RUVU JKT AKUBALI KIPIGO CHA SIMBA, ASEMA WATAJIPANGA
7:56 PM
Nahodha wa Ruvu JKT, George Minja amesema kufungwa kwao mabao 2-1 dhidi ya Simba ilikuwa ni hali ya kimchezo.
Minja amesema wana imani kuwa wana imani wataweza kucheza vizuri katika mechi zijazo na kurekebisha mambo.
"Mechi
ilikuwa ngumu na utaona tumeshindwa lakini ni hali ya kimchezo, lakini
tuna nafasi ya kufanya vizuri katika mechi zijazo," alisema.
Simba imeifunga JKT mabao 2-1 na kupata ushindi wake wa tatu msimu huu.
GOOOAAAL; KUTOKA TAIFA
5:23 PM
Dan Sserunkuma anaipatia simba goli la pili dakika ya 48 kipindi cha pili Simba 2 Jkt ruvu 1
HALIMBAYA SIMBA MECHI INAENDELEA
4:38 PM
Simba 1 na Jkt 1
Goli la Simba limefungwa na Dani Sserunkuma na goal la Jkt limefungwa na George minja
Goli la Simba limefungwa na Dani Sserunkuma na goal la Jkt limefungwa na George minja
PICHA JINSI BEN POL, SHILOLE, ROMA NA LINEX WALIVYO PAGAWISHA AZURRA BEACH
4:21 PM
Jana ilikuwa FURAHIDAY kwa watu wa nguvu Dar Es Salaam, staa wetu ambaye kwa sasa yuko kila kona kwa ile hit ya Sophia, Ben Pol alitukutanisha pale Azurra Beach Club kwa pamoja tukaenjoy kwa bata la nguvu kama ishara ya kuuaga mwezi January ndani ya mwaka 2015.
Ilipendeza, nyamachoma, vinywaji na muziki mzuri kutoka kwa Ben Pol mwenyewe, Shilole, Linex na rapper ROMA.
Pichaz za burudani yote hizi hapa mtu wangu.
MAWAKALA WAGONGANA KUMPELEKA ULAYA SAID NDEMLA
4:17 PM
Mawakala zaidi ya watano wamejitokeza kwa Klabu
ya Simba na kuomba kumchukua kiungo wa klabu hiyo, Said Ndemla kwenda kufanya
majaribio katika moja za timu za nje, hasa barani Ulaya.
Ikiwa mipango hiyo itakubalika na kwenda
inavyotakiwa, maana yake ni kuwa itakuwa mara yake ya kwanza.
Awali, kulitolewa taarifa kuwa, wachezaji
wengine wa klabu hiyo, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Hassan Kessy, walikuwa
kwenye mipango ya kwenda kufanya majaribio katika Klabu ya Real Madrid ya
Hispania.
Evans Aveva ambaye ni rais wa Simba ndiye
aliyefunguka kila kitu kwa kusema:
“Tunashukuru tunaendelea kutengeneza vijana na
wanafanya vizuri, mawakala watano kutoka nje wameanza kuvutiwa na uwezo wa Said
Ndemla, mipango inafanyika ili baada ya msimu huu wa ligi kuu kumalizika aweze
kwenda nchi tofauti kufanya majaribio.
“Kwenye mchezo wetu na Azam viongozi wa Real
Madrid walivutiwa na kiwango cha Singano na Kessy, waliomba CD zao kwenda
kuifanyia kazi.