MRENO
Cristiano Ronaldo ndiye mwanasoka tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri
wenye thamani ya Pauni Milioni 152, ikiwa ni Pauni Milioni 7 zaidi ya
hasimu wake mkubwa, Muargentina Lionel Messi.
Baada
ya msimu mzuri wa 2014, ambao ilishuhudiwa Ronaldo akiiwezesha Real
Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya naye akishinda tuzo ya
Mwanasoka Bora wa Dunia, maarufu kama Ballon d'Or, ameongeza idadi ya
utajiri anaomzidi nyota wa Barcelona na Argentina.
Kwa mujibu wa Orodha ya Matajiri ya Goal.com, ilitotolewa leo, Ronaldo na Messi bado ndiyo wanasoka wanaofurahia zaidi kazi hiyo kuliko wenzao wote duniani.
Cristiano Ronaldo akiwa na tuzo yake ya Ballon d'Or baada ya kukabidhiwa mjini Zurich, Uswisi Januari mwaka huu
ORODHA YA WACHEZAJI 10 TAJIRI ZAIDI DUNIANI
1. Cristiano Ronaldo £152.3
2. Lionel Messi £145m
3. Neymar £97.9m
4. Zlatan Ibrahimovic £76.1m
5. Wayne Rooney £74.6m
6. Kaka £69.6m
7. Samuel Eto'o £63.1m
8. Raul £61.6m
9. Ronaldinho £60.2m
10. Frank Lampard £58m
Lionel Messi anashika nafasi yaa pili kwa utajiri wa thamani ya Pauni Milioni 145
0 maoni:
Post a Comment