WINGA wa Dar Young Africans,
Simon Happygod Msuva amefurahia hali ya hewa ya Tunisia na kusema
wanaweza kuwafunga Etoile du Sahel.
Mchezo huo wa marudiano wa
hatua ya 16 ya kombe la shirikisho utapigwa kesho jumamosi katika dimba
la Olympique de Sousse katika mji wa Sousse kuanzia majra ya saa 3
kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.
Katika mchezo wa awali
uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam, Young Africans
ilitoka sare ya bao 1- 1 na Etoile na mshindi wa jumla atacheza hatua
ya mtoano (Play-off) dhidi ya timu zitakazokuwa zimetolewa kwenye Ligi
ya Mabingwa (CL) kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi.
kuelekea katika mechi Msuva
amesema: “Sisi tunashukuru Mungu hali ya hewa iko vizuri, tunaamimi
kesho tunaweza kufanya chochote. Kama wao waliweza kupata goli moja
kwetu nasisi tunaweza kupata kwao”.
Msuva ndiye kinara wa mabao
Yanga na ligi kuu Tanzania bara kwa sasa akiwa ameshafumania nyavu mara
17 akifuatiwa na mchezaji mwenzake wa Yanga Amissi Tambwe mwenye magoli
14.
0 maoni:
Post a Comment