SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 8, 2015

BLIND AIOKOA MAN UNITED DAKIKA ZA MWISHO

MANCHESTER United imeponea chupuchupu kulala mbele ya West Ham United baada ya kuata sare ya 1-1 ugenini usiku huu.
Cheikhou Kouyate aliifungia West Ham bao la kuongoza dakika ya 49 na United wakahaha tangu hapo kusaka bao la kusawazisha hadi kuelekea kupoteza mchezo.
Hata hivyo, kiungo Daley Blind akawanusuru Mashetani Wekundu kulala baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika ya 90.
Man United ilipata pigo baada ya beki wake Luke Shaw kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekndu. Pamoja na matokeo hayo, Man United wanabaki nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, wakati West Ham wanabaki nafasi ya nane.
Daley Blind (left) celebrates a late equaliser as Manchester United rescued a point at West Ham on Sunday afternoonll









MRISHO NGASSA APIGA MBILI YANGA

Mshambuliaji mwenye kasi wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa ameibuka shujaa baada ya kuifungia Yanga mabao mawili katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.


Yanga imelipa kisasi kwa kuichapa Mtibwa Sugar kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Katika mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo, Mtibwa iliichapa Yanga kwa idadi hiyo mjini Morogoro.
Kwa ushindi huo sasa Yanga imekwea kileleni kwa kuwa na pointi 25 ikiiacha Azam yenye 22, lakini ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Ngassa ameibuka shujaa katika mechi ya leo ameingia katika dakika ya 53 kuchukua nafasi ya Kpah Sherman aliyechemsha leo.

Dakika hiyohiyo aliyoingia, Ngassa alipiga mpira uliogonga mwamba wa juu.

Dakika mbili baadaye aliandika bao la kwanza baada ya krosi safi ya chinichini ya Simon Msuva kumfikia Amissi Tambwe, akiwa langoni, akashindwa kuunganisha. Yeye akaimalizia kazi hiyo.

Kama hiyo haitoshi, dakika ya 62, Ngassa alifunga bao la pili kwa kumchambua kipa Said Nduda baada ya pasi safi ya kupenyeza ya Haruna Niyonzima.

Baada ya bao hilo, Yanga walionekana kucheza vizuri zaidi huku Niyonzima na Coutinho wakionyesha kutawala zaidi katikati na Msuva na Ngassa wakizidi kuwasumbua mabeki wa Mtibwa kutokana na kasi yao kuwa kubwa.

Juhudi za beki Salim Mbonde, zilisaidia kwa kiasi kikubwa Yanga kutoongeza bao jingine.


Mara kadhaa, Mtibwa Sugar walifika langoni lakini wakashindwa kuzitumia nafasi zake kutokana na papara za washambuliaji wake akiwemo Ame Ally ‘Zungu’.

YANGA YAIBULUZA MTIBWA

Timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro shukran kwa Mrisho Ngassa ambaye alifunga magoli yote mawili katika kipindi cha pili.

MATOKEO KUTOKA TAIFA

Timu ya Yanga inaongoza goli 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro

HUYU NDIE MANAGER MDOGO MWENYE UBUNIFU WA KUIBUI VIPAJI ALI KIBA,MATONYA NA WENGINE WAMEPITA KWAKE

Kwa jina kamili anajulikana kama hemed kavu al maarufu  HK.. a.k.a hyperman hk  kijana mwenye kipaji chakugundua na kukuza vipaji vya vijana mbalimbali, wasanii wengi wanaofanya vizuri kwa sasa wamepita kwenye mikono ya hyperman hk nakupata njia nzuri ya mafanikio yao. kipindi cha miaka nane au sita iliyopita alikuwa Anafanya kazi club bilicanas hapo alikuwa na program yake yakukuza vipaji inayoitwa JAM SESSION.. Ilikuwa inaanza saa8 mchana mpaka saa1 usiku program hii imewakuza wasanii wengi sana akiwemo CHIDY BENZI,BOB JUNIOR,MR BLUE,DULLY SYKES,SUMER LEE,C PWAA,ALI KIBA,MATONYA,MB DOG, na wengine kibao..mwaka 2008 aliamia new maisha club na kundeleza gurudumu lake la kukuza vipaji mbalimbali na kuamua kuanzia kusimamia wasanii kama manager miaka ya 2000.ambapo alikuwa na msanii chipukizi  ytony ambaye kwa muda mrefu aliomba kumenejiwa na hk.. hapo ndipo hk akaamua kumpa nafasi kijana huyo ya kuwa msanii wa kwanza kupata bahati ya kufanya kazi na hk kama mtu na msanii wake. ytony mpaka sasa anatamba na ngoma kama MASEBENE,MY SHITOBE,NA MAMA aliomshirikisha Barnabas... baadae akamchukua marehemu sharo milionea mwaka 2012 na kufanikiwa kurecod nae ngoma mbalimbali ikiwemo ile aliyoimba na Ali kiba ya changanyachanganya lakini kwa bahati mbaya alifaiki dunia.[r.i'p sharo. ] hapo ndipo hk alipoongeza msanii mwingine wa kike ajulikanae kama SNURA MUSHI .. aliehit na ngoma zake kama MaJANGA,NIMEVURUGWA,USHAHARIBU N,K.. HK ana kipaji chakugundua ngoma mbalimbali zinazoweza kuwa ngoma kubwa sana pia ana upeo mkubwa wakutengeneza title ya nyimbo zinazohit kama wimbo wa masebene, majnga,na risasi kidole ya mashujaa band iliyoimbwana chalz baba.. hizi ni baadhi ya nyimbo alizozitengeneza hyperman hk.Pia anauwezo mkubwa wakukuza nyimbo na kujulikana na kuwa nyimbo kubwa tanzania akiamua kuifanyia nyimbo promotion kwa mfano ngoma kama chungwa ya suma lee NA HAKUNAGA,VIMEPANDA BEI BLADY KEY,NAINAI OMMY DIMPOZI,MAWAZO DIAMOND,DARE SALAAM STAND UP YA CHIDY BENZI,MAJANGA YA SNURA,MASEBENE YA Y TONY,KIZUNGUZUNGU YA SSHARO MILIONEA,SINDELELA YA ALI KIBA,WA ALADE YA BARNABAS, N,K
BOB JUNIOR akiwa na hk
mr blue akiwa na hk 
RADO Akiwa nyumbani kwa HK
sumer lee akiwa nyumbni kwa hk
CHIDY BENZ akiwa nyumbani kwa HK
Wasanii mbalimbali wanapenda kutembela na kukutana na hk kwa ajili yaa ushauri au kusikiliza nyimbo zao pindi wanapozitoa tu kbla ya kuzipeleka kokote pale umpa hk na kuwapa majibu ya ngoma zao,kama kali au zio kali.
HK akiwa na ESTHER WASILA
HK AKIENDESHA SHOW NEW MAISHA CLUB DAR
HYPERMAN HK Ni kijana mwenye kipaji cha kubuni vitu mbalimbali zinavyohusu burudani kwa sasa yupo katika club ya kimataisha inayojulikana kama new maisha club.yenye matawi yake dar,dodoma,mtwara  na morogoro. akiwa kama general intertaiment manager.. kwenye shughuli yakubuni burudani zote zinazofanyika katika club hizo yeye ndio incharge manyota.
Uzoefu wake wa miaka isiyopungua 15 katika game hii ndio inamfanya azidi kuwa nguli wa kazi hizi.
burudani nyingi zilizokuwa gumzo hapa mjini zimebuniwa na hk na majina yakimytaani yenye kuwa gumzo kubwa kana neno bunyero bunyero.
Aidear hii ya kitofauti imewafanya watu wengi sana kumuona hk ni mtu mwenye kipaji cha kipekee sana.. kwamana kuitoa burudani ya ushwahilini na kuileta uzunguni na kukubalika haikuwa kazi ndogo lakini ilieleweka na kukubalika sana. Mara ya kwanza burudani hii ya kibao kata iliyopewa jina la BUNYERO BUNYERO watu hawakudhani kama itagfika huku ilipo lakini ikawa ndio siku kubwa yenye kuingiza watu maisha club kuliko siku zote..kwanza ilikuwa inafanyika siku ya jumatano lakini watu walijaa hakuna sehemu ya club hapa dar inajaza watu hatamia siku ya jumatano lakini maisha club kupitia program hii inaingiza watu wasiopungua 500 siku ya jumatano kwa kiingilio cha elfu 10.,,, kwasasa usiku huo umepewa jina jipya linalojulikana kama usiku wa TAMNYETAMNYE.
Mengi yamefanywa na kijana huyu ebu anza kumfatilia ujue upeo wake zaidi juu ya ubunifu alonao kwenye facebook hemed kavu
instagram @hkhyper02
tweeter hyperman hk
whatsaap no 0713435543.

ALICHOSEMA OKWI KUHUSU UWANJA WA MKWAKWANI

MSHAMBULIAJI nyota wa Simba SC, Emmanuel Okwi amesema Uwanja wa Mkwakwani, Tanga haufai kabisa kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa sababu eneo la kuchezea ni baya.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana baada ya mechi dhidi ya wenyeji, Coastal Union ya Tanga, Mganda huyo alisema kwamba hakuna namna ambavyo hata mchezaji nyota anaweza kucheza vizuri Mkwakwani.
“Kila nilichojaribu kufanya leo (jana) kilikuwa kigumu, Uwanja mbaya kabisa, lakini tutafanya nini na hii ndiyo ligi yetu na hivyo ndivyo viwanja vyetu,”alisema Okwi.  
Emmanuel Okwi amesema Uwanja wa Mkwakwani haufai kwa mechi za Ligi Kuu

Simba jana ilazimishwa sare ya 0-0 na Simba SC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Hakukuwa na mchezo wa kuvutia sana kutokana na timu zote kucheza mipira mirefu kwa kuhofia ubovu wa Uwanja wa Mkwakwani na matokeo hayo yanafanya Coastal ifikishe pointi 18, wakati Simba SC inatimiza pointi 17.

KURASA ZA MBELE ZA MAGAZETI YA MICHEZO ZIPO HAPA

.
 .
 

KAGERA SUGAR YAFUTA MIKOSI IMESHINDA WENGINE WAPATA SARE

HATIMAYE Kagera Sugar imepata ushindi wa kwanza baada ya mechi nne za Uwanja wa nyumbani, kufuatia kuilaza 1-0 Mgambo Shooting Uwanja wa Kambarage, Shinyanga jana.
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza Kagera wanacheza Uwanja wa Kambarage kama wa nyumbani, baada ya kuhama Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
 
Kagera ililazimika kuondoka Bukoba baada ya Uwanja wa Kaitaba kuanza kukarabatiwa Januari mwaka huu na kuhamia Kirumba, Mwanza.
Hata hivyo, baada ya kufungwa mechi tatu mfululizo Mwanza, uongozi wa timu hiyo ukadai unafanyiwa hujuma na wenyeji wa mkoa huo, Toto Africans hivyo wakahamia Shinyanga.
Atupele Green aliifungia Kagera jana 

Na jana bao pekee ka Atupele Green limewafanya wapate cha kuongea kuhusu Mwanza- kwamba kweli walikuwa wanafanyiwa fitina na wenye mji wao, Toto.
Kagera ilikuwa timu pekee iliyoibuka na ushindi katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana, baada ya mechi nyingine zote kumalizika kwa sare. 
 
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Simba SC ilitoka sare ya 0-0 na wenyeji Coastal Unin, Uwanja wa Jamhuri Morogoro, mabingwa watetezi, Azam FC walitoka sare ya 2-2 na wenyeji Polisi, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, JKT Ruvu walitoka 1-1 na Mbeya City, Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Prisons walitoka 1-1 na Ruvu na Shooting, wakati Uwanja wa Nangwanda, Sijaona, Mtwara wenyeji Ndanda FC walilazimishwa sare ya 0-0 na Stand United ya Shinyanga.
 
Ligi hiyo inaendelea leo kwa mchezo mmoja kati ya Yanga SC na Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

HIVI NDIVYO GERRAD ALIVYO CHEZA DERBY YA MWISHO LIVERPOOL


Mchezaji wa Liverpool Steven Gerrad akifanya shambulizi katika mechi ya jana dhidi ya Everton na timu hizo zilitoshana nguvu kwa kupata suluhu ya bila kufungana.
 Everton (4-3-3): Robles 7; Coleman 7, Stones 7, Phil Jagielka 7, Oviedo 6.5; McCarthy 6, Barry 5.5, Besic 7.5 (Alcarez 86); Mirallas 6 (Lennon 60, 6) Naismith 6.5 (Barkley 85), Lukaku 6.
Subs not used: Griffiths, Gibson, Kone, Browning
Booked: McCarthy, Oviedo, Naismith, Besic

Liverpool (3-4-3): Mignolet 7; Can 7, Skrtel 8, Sakho 6.5; Henderson 7.5, Lucas 5 (Allen 16, 6), Gerrard  6, Moreno 6; Ibe 8.5, Sterling 6 (Lambert 82), Coutinho 6 (Sturridge 55, 6).
Subs not used: Ward, Johnson, Lovren, Markovic
Booked: Henderson 
Referee: Anthony Taylor (Cheshire)
Star man: Jordon Ibe 


















MAN CITY ILIPOLAZIMISHWA SARE NYUMBANI NA HULL


The visitors nearly took the lead when defender Ahmed Elmohamady's (centre) header deflected off Gael Clichy (right) and onto the post
Ahmed Elmohamady wa Hull City (katikati) akipambana na beki wa Manchester City, Gael Clichy (kulia) mbele ya kipa Joe Hart katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Etihad. Timu hizo zilitoka 1-1, Hull wakitangulia kupata bao dakika ya 35, mfungaji David Meyler wakati la Man City lilifungwa na James Milner kwa shuti la mpira wa adhabu dakika za lala salama.
James Milner (right) proved Manchester City's hero by scoring an injury time equaliser as Manchester City drew 1-1 at home with HullWachezaji wa Man City wakishangilia baada ya kufunga goli la kusawazisha
 Milner (centre) curled home an unstoppable free-kick from close range that broke Hull hearts and salvaged a point for City
 The England international (left) celebrates his strike with team-mate Pablo Zabaleta as City rescue a point