YANGA SC imeanza vizuri michuano
ya kombe la Shirikisho barani Afrika kufuatia kuichapa mabao 2-0 BDF XI
ya Botswana katika mchezo wa kwanza wa raundi ya awali uliomalizika
jioni hii uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam.
Mabingwa hao mara 24 wa Tanzania
walianza mechi hiyo kwa kuonesha kandanda safi na katika dakika ya
kwanza ya mchezo waliandika bao la kuongoza kupitia kwa Mrundi, Amissi
Tambwe aliyefunga kwa kichwa akimalizia mpira wa kona wa winga
machachari, Simon Msuva.
Tambwe aliyekuwa na umakini leo
alitia kambani bao la pili dakika ya 55’ kwa njia ya kichwa akimalizia
krosi ya Mrisho Khalfan Ngassa.
Katika vipindi vyote viwili,
Yanga walitawala mchezo wakicheza pasi nyingi, lakini walishindwa
kutengeneza nafasi nyingi za kufun
Hata hivyo Yanga waliendelea kupoteza baadhi ya nafasi walizopata na wangekuwa makini wangepata ushindi mkubwa zaidi.
Kikubwa walichofanikiwa BDF XI ni kucheza mpira wa kujilinda na kushambulia kwa kushitukiza.
Malengo yao yalikuwa kukwepa kichapo kikubwa ili wakajipange upya nyumbani na ndio utamaduni wa michuano mikubwa barani Afrika.
Kitu wanachotakiwa kujirekebisha
Yanga ni kucheza mpira wa pasi wenye madhara, kwasababu wanajikuta
wakigongeana pasio nyingi katika eneo lao na kushindwa kuisogeza timu na
kulazimisha mashambulizi.
Mechi ya nyumbani lazima utumie mbinu nyingi kufika langoni kwa mpinzani hata kama anacheza soka la kujihami zaidi.
Yanga wanastahili pongezi kwa ushindi huo waliopata kwasababu BDF wanahitaji ushindi wa mabao 3-0 ili kuwatupa nje Yanga.
Kwa upande wa Yanga wanahitaji
kufungwa bao 1-0 au sare ya 1-1 ili kusonga mbele na kwa uwezo waliokuwa
nao Wanajangwani wanaweza kushinda.
Kikubwa ni kuongeza nidhamu hasa katika kutumia nafasi wanazopata na kutengeneza nafasi nyingi za magoli.
Baada ya Yanga, kesho uwanja wa
Azam Complex, Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, Azam fc
watachuana na mabingwa wa Sudan, EL Merreick katika mechi ya raundi ya
kwanza ligi ya mabingwa barani Afrika.