Sare ya bila kufungana
dhidi ya Prisons ya Mbeya imezidi kuibana Azam FC.
Sasa imefikisha pointi 27
baada ya mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi,
Dar es Salaam, leo.
Yanga inaendelea kuongoza
ikiwa na pointi nne zaidi ya Azam FC ikiwa ni baada ya kuitwanga Mbeya City kwa
mabao 3-1.
Azam imecheza mechi 15, imeshinda saba, sare sita na wamepoteza mbili.