SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 23, 2015

SIMBA UMOJA NI NGUVU, UTENGANO NI DHAHIFU


avevaaSiku zote unapokuwa puppet au kibaraka kwa lugha ya kiswahili mbali na hilo au kuwa mbabe katika uongozi hakutakuwa na tija hata kidogo na hakutakuwa na matokeo mazuri.
Kingine ni hili suala la matabaka katika sehemu ambayo umoja unahitajika ili kujenga kitu cha msingi ambao utasimama bila kuwa na nyufa ni kama tu unapoanza kujenga nyumba yako mtu wangu, usipotengeneza vizuri msingi wa jambo utaishia kuona nyumba inadondoka au nyufa zinaanza kutokea.
Haya ni mambo mawili ambayo Simba imekumbwa nayo kwa wakati huu na chanzo kikubwa ni uongozi uliopo madarakani bila kupepesa macho.
Matabaka yameiandama Simba toka kwa Uongozi wenyewe hadi kwa wachezaji wenyewe wanakuwa na matabaka.
Ninapoongelea wachezaji nabase moja kwa moja kutokana na jinsi value zao na jinsi wanavyokuwa treated bila usawa. Utakuta yule anapata kila kitu na mwingine hapati kiufupi tu lazima wachezaji hawatakuwa na morality nzuri katika kucheza mpira.
Baadhi ya viongozi au Kiongozi kuzuiwa kuingia katika kambi ya timu lazima pande moja itakuja na mtazamo tofauti na kwa situation hiyo hakuna umoja utakaokuwepo.
Simba kama Brand hakuna haja ya kuwa na matabaka au kutotimiza mahitaji kwa wachezaji hakuna la maana ambalo litafanyika watu wangu.
Nawapongeza Yanga kwasasa walio na umoja na wapo kwenye morality nzuri hivi sasa na imekuwa timu ya kuigwa na haya Simba iwe mfano wa kuiga jinsi Yanga wanavyofanya hivi sasa hakuna kabisa matabaka.
Ni halali yako kushare mawazo yako mtu wangu au kama una breaking News kuhusiana na matukio ya kimichezo au maoni au hata ushauri unaolenga kufika sehemu husika, tuma na tutafikisha sehemu husika mawaidha yako kwa njia ya WhatsApp +255688665508.

JULIO ALIANZISHA MAPEMAAA, ASAKA WAKANDIAJI WA ‘VIBABU VYAKE’

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa Mwadui ambayo jana ailitwaa 'mwali' wa ubingwa wa Ligi Daraja la kwanza Jamhuri Kihwelo 'Julio' amefurahia mafanikio hayo kwa kuwasaka wale wote waliokuwa wakimbeza kwa kuwaita wakongwe.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Julio amesema alikuwa anajua nini anakitaka kwa wachezaji wakongwe wakiongozwa na viungo Athuman Idd 'Chuji', Uhuru Seleman, Julius Mrope, mshambuliaji Monja Liseki na mabeki Juma Jabu na Said Sued.
Kocha wa Mwadui FC ya Shinyanga ameanza kutamba baada ya kupanda Ligi Kuu

Julio amesema uzoefu wa wachezaji hao ndiyo umesaidia kupatakana kwa mafanikio hayo ambapo nyota hao walikuwa wanazingatia mafundisho yake.
"Nilikuwa nawashangaa wote waliokuwa wananiona mimi mjinga kwa kuwaita hawa ndiyo maana wakati tunashangilia pale uliona vijana wangu wakiimba hayo maneno ya wazee,alisema Julio.
"Nilijua nataka nini kwao,mimi ni kocha wa mpira kuna wakati lazima watu watuachie walimu kazi yetu tuifanye bila kuingiliwa wakongwe hawa waliokuwa wanaonekana wazee ndiyo sasa wametupa kombe.

SIMBA YAANZA KUDILI NA WAANDISHI WA HABARI.


evansssBaada ya Simba kufanya vibaya uongozi wa klabu na baadhi ya wadau wa karibu wamekaa kikao cha dharula kufikiri kwamba kuna baadhi ya waandishi wa habari ambao wanawaambia ukweli juu ya mwenendo wa Uongozi uliopo madarakani kwamba ndio wanasababisha Simba kufanya vibaya.
Hivyo maamuzi ya kikao hicho ni kwamba kuanzia leo katika vipindi vya redio mbali mbali wameandaliwa wanachama kwa ajili ya kutetea madudu ya Uongozi na kuanza kuwaponda waandishi hao hivyo naombeni leo mchukue mda wenu kusikiliza redio mbali mbali hapa nchini ili muhifahamu sinema hiyo iliyoandaliwa na Uongozi katika kujitetea.
Lakini cha msingi mtandao mzima tunao na mawasiliano yao tunayo na meseji na namba wanazotumiana ili kupeana mgao kwa hao watangazaji watakaofanya kazi hiyo tunazo, kazi kwenu wadau
NAWASILISHA ASANTENI.

LUIS NANI APIGA BONGE LA BAO KISHA AANGUSHA KILIO UWANJANI

 Kiungo wa Man United anayecheza Sporting Lisbon kwa mkopo amefunga bonge la bao, halafu akaanza kulia.


Nani amefunga bao hilo umbali wa zaidi ya mita 30 wakati Sporting ilipishinda Gil Vicente kwa mabao 2-0, jana.
 
Baada ya kufunga bao hilo safi kabisa, Nani alijilaza na kuanza kulia.
Licha ya wenzake kumshawishi kuinuka, aliendelea kulia huku akiinua mikono juu akionyesha kumshukuru Mwenyezi Mungu.
 
Nani ,28, alipelekwa kwa mkopo katika timu yake hiyo iliyomkuza kisoka baada ya kuonekana hana kiwango kizuri.
Wakati wa Alex Ferguson na Man United ikiwa tishio, Nani alikuwa mmoja wa wachezaji bora wanaotegemewa.




KWIZERA AANZA VIBAYA RWANDA


Kiungo wa zamani wa Simba, Pierre Kwizera ameanza vibaya katika kikosi chake kipya nchini Rwanda.

Rayon Sports, imekumbana na kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa watani wao wa jadi APR katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amahoro, Kigali, juzi.
Kwizera ambaye alicheza katika mechi hiyo na kuonyesha kiwango kizuri.
Lakini mambo yakawa magumu kwao katika kipindi cha pili kwani APR walifunga mabao yote ndani ya hizo dakika 45 za pili.


Mabao ya APR yalifungwa na Nsahindula Michelle, emiry Bayisenge, Yannick Mukunzi na Sekamana Maxime.

KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO FEB 23, 2015

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC09824
.
.
.

ALICHOSEMASEMA KAPOMBE BAADA YA KUTOKA SARE NA PRISONS

_DSC0548
Kapombe (kushoto) siku walipocheza na Simba
MCHEZAJI kiraka wa Azam fc, Shomari Salum Kapombe amesema matokeo mabaya wanayopata Prisons ndio chanzo cha kuwakazia jana usiku katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyomalizika kwa suluhu uwanja wa Azam Complex.
“Prisons walifungwa mechi iliyopita na Yanga, leo wamekuja na nguvu. Wameonesha kiwango kizuri na nidhamu ya mchezo. Wamejilinda vizuri na kucheza mpira”.
“Tumejitahidi kufika mara nyingi golini kwao, lakini kipa wao (Mohammed Yusuph) amekuwa imara”.
Kwa matokeo ya jana, Azam fc wanaendelea kushika nafasi ya pili kwa pointi 27 baada ya kushuka dimbani mara 15, wakati Yanga wanaongoza msimamo kwa pointi 31 baada ya kucheza mechi 15.
Kapombe amesema baada ya mechi hiyo, sasa wanaelekea macho yao katika mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Merreick.
Mechi ya kwanza Azam walishinda 2-0 na mechi ya marudiano itayopigwa mwishoni mwa wiki hii, matajiri wa Dar wanahitaji ushindi au kufungwa magoli yasiyozidi mawili.

REAL MADRID YAICHAPA ELCHE

Cristiano Ronaldo clenches his fist in celebration after scoring Real Madrid's second goal of the night against Elche
Mshambuliaji Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia timu yake, Real Madrid usiku wa kuamkia leo katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Elche katika mchezo wa La Liga. Bao lingine la Real lilifungwa na Karim Benzema.
 Â Benzema expresses his delight after giving the Spanish giants the lead against relegation-threatened Elche
 The forward duo celebrate after the France striker (left) scored the opening goal for Real against Elche on Sunday night