SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 25, 2015

MATIC KUKOSA MECHI MBILI


Adhabu ya kufungiwa mechi tatu kwa kiungo wa Chelsea Nemanja Matic imepunguzwa hadi mechi mbili. Mchezaji huyo atakosa mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi siku ya Jumapili dhidi ya Tottenham. Tume huru ya udhibiti ya Chama cha soka cha England FA ilishikilia adhabu, baada ya rufaa kukatwa na Chelsea siku ya Jumanne. Matic, 26, alioneshwa kadi nyekundu siku ya Jumamosi katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Burnley, baada ya kukasirishwa na jinsi Ashley Barnes alivyomkwatua. Katika taarifa iliyotolewa, Chelsea wamesema "wamesikitishwa na kuhuzunishwa" na hatua ya Matic kutumikia adhabu. Mbali na kukosa mechi ya fainali ya Jumapili itakayochezwa Wembley, Matic pia atakosa mchezo dhidi ya West Ham United wa Jumatano Machi 4.

YANGA SC WATUA SALAMA GABORONE, WAFIKIA OASIS HOTEL


Kocha Msaidizi wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa (kulia) akiwa na wachezaji wake eneo la mapokezi katika hoyeli ya Oasis mjini Gaborone, Botswana mchana wa leo baada ya kuwasili kwa ajili ya mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) utakaofanyika keshokutwa nchini humo. Yanga SC ilishinda 2-0 katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam. 

AZAM FC WAPOKEWA ‘KIGAIDI’ SUDAN, WAPEWA ‘GARI LA MKAA’, WACHEZAJI WAPIGISHWA KWATA UWANJA WA NDEGE

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Azam FC wamepata mapokezi ya ‘kigaidi’ mjini Khartoum, Sudan baada ya kuwasili usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya mchezo na wenyeji, El Merreikh.
Kwanza, walipotua Uwanja wa Ndege, wachezaji na msafara mzima walianza kufanyiwa vitimbi na watu wa Idara ya Uhamiaji katika kupatiwa visa za kuingia nchini humo.
Baada ya kuufuzu mtihani huo, walikutana na visa zaidi walipotoka nje ya Uwanja wa Ndege, kufokewa na watu waliokwenda kuwapokea, kabla ya kwenda kuwapakia katika basi bovu na baya aina ya Coaster.
Hili ndilo basi ambalo El Merreikh wamewapatia Azam FC baada ya kuwasili Khartoum
Basi hili mwonekano wake kama limetoka vitani
Basi aina ya Coaster ambalo wamepewa Azam FC Sudan

Pamoja na hayo, Azam FC kwa kuwa walijua watakutana na hali kama hiyo, hawakuonekana kustaajabu, badala yake kuvumilia yote. 
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY kwa simu kutoka Khartoum kwamba wamefanyiwa mambo ambayo kwa ujumla si ya kuanamichezo.
“Tunarekodi kila kitu na tutatuma CAF (Shirikisho la Soka Afrika). Sisi hatuna wasiwasi nao, kwa sababu tunawajua,”amesema. 
Kikosi cha wachezaji 23 wa Azam kimewasili Khartoum tayari kwa mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika mwishoni mwa wiki.
Azam FC inahitaji hata sare au kutofungwa kwa wastani wa zaidi ya bao 1-0 ili kusoga mbele kwenye michuano hiyo, baada ya awali kushinda 2-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wiki iliyopita.

KOCHA JULIO AAMIA COASTAL UNION


???????????????????????????????
Na Augustino Mabalwe
Kocha wa klabu ya Mwadui Jamhuri kihwelo “Julio” ametua katika klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu huu ambapo atakuwa klabuni hapo  kama kocha msaidizi.
Imeripotiwa kuwa kocha huyo amechukua uamuzi huo kutokana na urafiki wake wa karibu na klabu hiyo,pia analengo la kuinua kiwango cha timu hiyo kinachoonekana kuyumba msimu huu.
Coastal Union ambayo iko chini ya kocha mkenya James Nandwa imekuwa ikisuasua kunako ligi kuu Tanzania bara na kwa sasa inashika nafasi 7 ikiwa na pointi 19 katika ligi hiyo.
Julio amekuwa kocha tishio nchini na sasa ameipandisha daraja timu ya Mwadui na kutwaa ubingwa wa ligi daraja la kwanza baada ya kuitandika African sports katika mchezo wa fainali uliopigwa jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Azam Complex huko Chamanzi jijini Dar es salaam.

HUYU NDIE MCHEZAJI ALIECHEZA MUDA MFUPI YANGA


simba yanga
Mchezaji anayeshikilia rekodi ya kuichezea Yanga SC miaka mingi zaidi bila kuhama ni Keneth Mkapa. Yasemekana ameitumikia Yanga zaidi ya miaka 13 huku Mchezaji aliyeitumikia Yanga kwa muda mchache zaidi ni Emerson toka nchini Brazil. Aliitumikia Yanga kwa dakika 45 tu kwenye mechi ya mtani jembe. Baada ya hapo mkataba wake ulivunjwa.

KOPUNOVIC ATOA BONGE LA DARASA SIMBA


simba+px
“Niwaambie ukweli mashabiki wangu, kila mtu anayeniunga mkono ni kama familia yangu, kila shabiki wangu ni kama mtoto wangu, kila shabiki ni mtu muhimu kwangu, kila shabiki ni muhimu kwa Simba, lakini kila shabiki lazima aelewe kitu hiki muhimu;
“Timu hii ni changa sana, timu hii inahitaji muda, sisemi kuwa tunahitaji miaka kumi, hapana! Tunahitaji muda, nilikuja nimechelewa, nikiwa na Matola tunajaribu sana kuiboresha timu hii, lakini timu hii ina presha, tunawapa presha kubwa wachezaji wangu kila wiki, lakini wachezaji wangu hawana uzoefu kwasababu ni wachanga”
Wakati fulani tunacheza vizuri, wakati fulani tunaanguka, wakati fulani tunashinda, kila shabiki lazima aelewe kitu hiki, hata sare, lazima wawape wachezaji wangu nguvu kwa ajili ya mechi ijayo, unapoanza kupiga kelele..aaaah! nini? Aaaah! mechi inayofuata inakuwa hatari zaidi kwa mchezaji mchanga kwasababu hana uzoefu wa kuwaza mechi iliyopita, pia hana uwezo binafsi wa kujijenga na kuongeza morali ya mchezo ujao”.
“Kwa timu yangu, kocha Goran anaahidi, kila mechi, kila mazoezi, ninafanya kazi kwa asilimia mia moja, wachezaji wangu kila wanapocheza mechi wanacheza kwa juhudi, wanacheza kwa ajili ya Simba, lakini wakati fulani hatushindi kila mechi”
Maneno haya yamezungumzwa na kocha mkuu wa Simba Sc, Goran Kopunovic wakati huu kikosi chake kikijiandaa kuivaa Prisons uwanja wa Taifa, Dar es salaam katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Simba walifungwa bao 1-0 dhidi ya Stand United katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga

SIMBA, YANGA ZAPIGWA BAO NA AZAM FC


04
AZAM FC ni klabu inayojifunza na kuendeleza pale inapofikia kwa misimu minne sasa tofauti na klabu kongwe za Simba na Yanga ambazo hupanda na kushuka.
ANGALIA TAKWIMU HIZI
2010/2011-Simba walishika nafasi ya pili kwa pointi 49, huku Yanga wakichukua ubingwa kwa pointi  49, lakini walibebwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Walifunga magoli 32, walifungwa magoli 7, tofauti ilikuwa magoli 25.
Simba walifunga magoli 40, walifungwa 17, tofauti ya magoli ilikuwa 23.
2011/2012-Simba walitwaa ubingwa wa ligi kuu kwa kujikusanyia pointi 62, huku Azam fc wakishika nafasi ya pili kwa pointi 56, Yanga wakashika nafasi ya tatu kwa pointi 49.
Kumbuka msimu uliopita wakati huo, Yanga walikuwa mabingwa na Simba walikuwa wa pili.
2012/2013- Yanga walichukua ubingwa kwa pointi 60, Azam fc wakashika nafasi ya pili kwa pointi 54, Simba wakawa wa tatu kwa pointi 45.
Hapa utaona Yanga kutoka nafasi ya tatu msimu uliopita wakati huo akachukua ubingwa, Simba akashika nafasi ya tatu kutoka kuwa bingwa. Azam akaendelea kubakia nafasi ya pili kwa msimu wa pili mfululizo.
2013/2014- Azam fc walitwaa ubingwa kwa pointi 62, Yanga wakashika nafasi ya pili kwa pointi 56, Simba nafasi ya nne kwa pointi 38.
Utagundua kuwa Azam waliendeleza walipoishia, kutoka nafasi ya pili mfululizo na kutwaa ubingwa, Simba wakashuka zaidi mpaka nafasi ya nne wakiwapisha Mbeya City nafasi ya tatu waliojikusanyia pointi 49.
Mpira wa miguu ni takwimu, hapa Azam fc wamekuwa bora kuliko Simba na Yan

BARCELONA YAILAMBA MAN CITY KWAO, SUAREZ SHUJAA


 Barcelona imefanikiwa kushinda kwa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 Bora.

Barcelona imeshinda kwa mabao hayo ugenini dhidi ya wenyeji wake Manchester City huku Luis Suarez akiwa shujaa kwa kufunga mabao yote mawili.

Lionel Messi alipata nafasi ya kufunga mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa na Zabaleta katika dakika ya 90 lakini Joe Hart akaokoa, mpira ukamrudia Messi, akakosa.
Sergio Aguero ndiye alifunga bao pekee la Barcelona, akionyesha juhudi binafsi na kufanikiwa kufunga bao tamu kabisa.




TEVEZ ATUPIA JUVE IKIITUNGUA DORTIMUND BAO 2-1


 
Carlos Tevez ameendelea kuwa mtamu zaidi ya Mcharo baada ya kuingoza Juventus kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 Bora.
Tevez ndiye alifunga bao la kwanza huku Alvaro Morata akitupia la pili.

Marco Reus alifunga bao pekee la Dortmund waliokuwa ugenini hivyo kufanya mabao yote ya mechi hiyo kuwa yamefungwa katika kipindi cha kwanza.

Tevez alikuwa mwiba kwa mabeki wa Dortmund, hata hivyo walijitahidi kuhakikisha hawafungwi mabao mengi zaidi.

LISTI:
Juventus starting XI: Buffon, Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Evra, Marchisio, Pirlo, Pogba, Vidal, Tevez, Morata
Juve subs: Storari, Caceres, Ogbonna, Padoin, Pereyra, Coman, Llorente
Borussia Dortmund XI:  Weidenfeller, Piszczek, Sokratis, Hummels, Schmelzer, Gundogan, Sahin, Mkhitaryan, Reus, Aubameyang, Immobile
Subs: Langerak, Ginter, Kirch, Kagawa, Kuba, Kehl, Ramos
Referee: Antonio Mateu Laho




ZIPO HAPA KURASA ZA MWANZO ZA MAGAZETI YA MICHEZO FEB 25,2014

.
.
.
.
.
.
.
.
.