Samatta alikwenda kufanya majaribo CSK Moscow ya Urusi, lakini hakufanikiwa baada ya kupata majeruhi ya kifundo cha mguu
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Mshambulizi wa kimataifa wa
Tanzania, Mbwana Samatta ameweka wazi kuwa ataachana na mabingwa mara
nne wa kihistoria wa Afrika, TP Mazembe mara baada ya kumalizika kwa
mkataba wake. Akizungumza na mwandishi wa mtandao wa www.shaffihdauda.co.tz muda mfupi uliopita mshambulizi huyo wa Taifa Stars amesema kuwa hana furaha katika timu hiyo ya Congo.
Samatta ambaye alipata nafasi ya
kufanya majaribio katika klabu ya CSKA Moscow ya Urusi mwezi uliopita
amepewa ofa nyingi barani ulaya na kama ataendelea kuchezea TP basi
atakuwa ni mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi barani Afrika. Hivi
karibuni kuna vyombo vya habari ambavyo viliripoti kuwa mchezaji huyo
ana furaha kuendelea kuichezea TP lakini amesema huo ni uzushi mkubwa.
” Sina furaha hapa ( TP Mazembe)
nitaondoka wakati wa majira ya usajili katikati ya mwaka na sitaongeza
mkataba” anasema Samatta. Ni wapi anakwenda, nini kinachomuondoa TP
Mazembe, tafadhaLi endelea kufuatilia mtandao huu wa www.shaffihdauda.co.tz... na www.hajibalou.blogspot.com Utapata kujua wapi mchezaji huyo anakwenda. Je, tayari ameruhusiwa na Katumbi Moies mmliki wa TP?…..