Na. Richard Bakana
Kocha msaidizi wa klabu ya
Coastal Union, kutoka Tanga, Jamhuri Kihwero ‘Julio’ ameangushia zingo
la lawama safu yake ulinzi na kusema kuwa wamecheza kipuuzi kitu
kilichopelekea kugawana pointi moja moja na Kagera Sugar kwenye mchezo
wa ligi kuu ya Tanzamia bara uliomalizika kwa sare ya 2-2 Mkwakwani.
Akizugumza na Shaffihdauda.com
baada ya mchezo huo, alisema kuwa tayari mchezo huo walikuwa
wameuweza, lakini kutokana na makosa yaliyofanywa na mabeki, Kagera
Sugar waliweza kusawazisha licha ya Coastal Union, kuongoza kwa bao moja
hadi dakika 45 za mwanzo zinamalizika, kufatia kazi safi ya Seleman
Kibuta aliyemalizia mpira uliokuwa ukizagaa katika lango la Kagera ikiwa
ni dakika ya 6 ya mchezo.
“Mimi nasema hapa hakuna swala la
Ufundi kwasababu wamepoteza umakini, Mchezo tulikuwa tumeshinda tayari,
zilikuwa zimebaki dakika kama saba wameruhusu goli la kipuuzi ambalo
kila mtu kwa kweli limemuuzi, Na hii ni kukusekana kwa umakini kwa
sababu Kagera hawakuweza kukata tamaa, wameweza kushambulia wakitaka
kurudisha na wamewez, Kwahiyo ni uzembe wa mabeki wetu, Mara ya kwanza
walikuwa wanalalamika kuwa hawafungi kwahiyo kama wanafunga basi mabeki
ndio watakuwa na matatizo, Tutalifanyia kazi ili kuona kwanini
wanaruhusu magoli ya kizembe” Amesema Julio ambaye ni Kocha mkuu wa
Mwadui FC ambayo imepanda ligi kuu msimu huu lakini Costal Union
akifundisha kwa muda.
Baada ya Coastal kufanikiwa
kuongoza kwa dakika 45 za mwanzo, Kagera walirudi katika Uwanja wa
Mkwakwani Tanga wakiwa na presha kubwa wakisaka bao ndipo Mshambuliaji
Atupele Green akaisawazishia timu yake bao akiunganisha kwa kichwa krosi
safi kutoka kwa Salum Kanoni na kumuacha mlindamlango wa Coastal Union
Shaaban Kado akiwa hana cha kufanya ikiwa ni dakika ya 52 ya mchezo.
Katika Dakika ya 60, mwamuzi wa
mchezo huo kutoka Mtwara, David Paul, aliizawadia Coastal Union, penati
ambayo ilizamishwa kambani na Rama Salum, Raia wa Kenya, baada ya Abuu
Mtilo kuunawa mpira ndani ya chumba cha kupigia penati, na kufanya
Wagosi hao wa kaya kufikisha bao 2-1.
Pongezi ziende kwa Rashid Mandawa
aliyeisawazishia Kagera Sugar bao 2 na kufanya kibao kiwe 2-2 ikiwa ni
dakika ya 84 akitumia makosa wa mabeki wa Coastal Union ambao
walishindwa kuosha mbele mpira uliokuwa unazagaa katika lango lao.
Hata hivyo hadi kipenga cha
mwisho kinapigwa kuashiria mtanange huo kumalizika timu hizo zikigawana
pointi moja moja kwa kutoa sare ya 2-2, Wenyeji wa mchezo huo Coastal
Union walimaliza wakiwa Pungufu kufatia mchezaji Othuman Tamimu
kuzawadiwa kadi Nyekundu katika dakika ya 73 kwa kosa la kuchelewesha
mpira ambapo tayari awali alikuwa na kadi ya njano.