Mar 9, 2015
10 BORA YA WACHEZAJI WANAOONGOZA KUPIGA CHENGA NA KUTOA PASI BARANI ULAYA RONALDO HAYUPO HATA 20 BORA
7:26 AM
Naposema
“kufanikiwa au kukamilisha chenga” namaanisha kuwa unampiga mtu au watu
chenga halafu unafanikiwa kuumiliki mpira bila kupokonywa na kisha
kumpasia mwingine au kufunga au kufanya vyovyote vile, Yaani unapiga
chenga bila kupokonywa mpira, Sasa hapo nadhani umenipata kwa ufafanuzi
huo ili usije kubakia ushangaa hapa.
Sasa twende kazi…
Najua haujui ila nitakujuza hapa aisee…
Lionel Messi ndie mchezaji
aliepiga chenga nyingi kwa mafanikio barani Ulaya kwa zaidi ya misimu
miwili iliopita kuliko mchezaji yeyote.
Messi amepiga chenga 258 bila kupokonywa mpira, Kwa hiyo, Messi ndio top dribbler in Europe zaidi ya misimu miwili iliopita.
Messi amepiga chenga 258 bila kupokonywa mpira, Kwa hiyo, Messi ndio top dribbler in Europe zaidi ya misimu miwili iliopita.
Eden Hazard wa Chelsea anafuatia kwa ukaribu zaidi akiwa amezidiwa chenga nne tu na Messi. Hazard ana chenga 254.
Hazard ni mmoja kati ya wachezaji wawili kutoka kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kuingia kwenye 10 bora hiyo.
Mwingine ni Raheem Sterling wa Liverpool mwenye chenga 172 akishika nafasi ya nane.
Hazard ni mmoja kati ya wachezaji wawili kutoka kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kuingia kwenye 10 bora hiyo.
Mwingine ni Raheem Sterling wa Liverpool mwenye chenga 172 akishika nafasi ya nane.
Lakini katika hali ya kushangaza,
mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo hayupo kwenye 10 bora hiyo na
wala kwenye 20 bora ya waliopiga chenga na wakakamilisha chenga zao.
Cristiano Ronaldo yeye hajafikisha hata nusu ya chenga za Messi na Hazard kwa hiyo zaidi ya misimu miwili.
Cristiano amepiga chenga 99 kwa
kipindi hicho zaidi ya misimu miwili, ambapo imemfanya kuwa nje ya 20
bora kwenye orodha iliotolewa.
Takwimu hizo zinaonyesha jinsi
wachezaji wafupi kina Messi, Hazard na Sterling walivyo wachezaji hatari
kwenye timu zao kama wachezeshaji wakubwa.
Na hapa ndipo wachezaji kutoka
Ligi Kuu ya Ujerumani wanapotamba. Bundesliga imetoa wachezaji sita
katika kumi bora ya wapiga vyenga bora barani Ulaya.
Hapa utawakuta kina Arjen Robben (172) na Frank Ribery (175) wote wa Bayern Munich.Kuna winga Roberto Firmino (244) wa Hoffenheim, Raffael (222) wa Borussia Monchengladbach, Karim Bellarabi (206) wa Bayer Leverkusen, na Eric Choupo-Moting (200) wa Schalke 04.
Lucas Moura wa Paris Saint Germain (PSG) anafunga kumi bora akiwa amepiga chenga 167.
Hakuna mchezaji yeyote kutoka Ligi Kuu ya Italia alieingia kwenye kumi bora ya orodha hiyo.
PICHA; HIVI NDIVYO SIMBA VS YANGA ZILIZYOONYESHANA UBABE MSIMABAZI WAKIIBUKA KIDEDEA
7:05 AM
TAMBWE AKIPAMBANA NA JONAS MKUDE WA SIMBA... |
KESSY WA SIMBA AKIMILIKI MPIRA MBELE YA JAVU WA YANGA, KUSHOTO NI NDEMLA WA SIMBA. |
IVO MAPUNDA WA SIMBA AKIFANYA YAKE... |
BEKI MGANDA WA SIMBA, JUUKO MURISHID AKILONGA NA MWAMUZI WA MECHI HIYO, MARTIN SAANYA... |
TAMBWE AKIJARIBU KUWATOKA MESSI NA KESSY... |
YONDANI WA YANGA AKIRUKA JUU KUMKWEPA KIPA WAKE ALLY MUSTAPHA HUKU MESSI WA SIMBA AKIANGALIA.... |
CANNAVARO WA YANGA AKIMWANGUKIA MESSI WA SIMBA,.... |
OKWI AKIJARIBU KUMTOKA CANNAVARO WA YANGA... |
ILIANZA YANGA B KUSHUGHULIKIWA, IMEPIGWA NNE NA SIMBA B
6:38 AM
TIMU ya vijana ya Simba SC
imewafunga wapinzani wao, Yanga SC mabao 4-2 katika mchezo uliofanyika
mchana wa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo wa utangulizi kabla ya timu za wakubwa za klabu hizo kumenyana katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ulishuhudiwa na maelfu ya wapenzi wa timu hizo waliowahi uwanjani.
Mabao ya Simba SC inayofundishwa na kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Nico Kiondo yalifungwa na Ibrahim Suleiman dakika ya tatu, Issa Abdallah dakika ya 41 na 51 na Mbarak Yussuf dakika ya 72.
Mabao ya Yanga SC inayofundishwa na kiungo wake wa zamani, Salvatory Edward anayesaidiwa na beki wa zamani wa timu hiyo, Nsajigwa Shadrack yamefungwa na Amos dakika ya 57 na Sospeter dakika ya 72.
Mchezo huo wa utangulizi kabla ya timu za wakubwa za klabu hizo kumenyana katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ulishuhudiwa na maelfu ya wapenzi wa timu hizo waliowahi uwanjani.
Mabao ya Simba SC inayofundishwa na kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Nico Kiondo yalifungwa na Ibrahim Suleiman dakika ya tatu, Issa Abdallah dakika ya 41 na 51 na Mbarak Yussuf dakika ya 72.
Kiungo wa Simba B, Mohammed Kijiko akipasua katikati ya wachezaji wa Yanga B leo Uwanja wa Taifa
|
Mohammed Kijiko akimtoka beki wa Yanga B, Issa Ngao
|
James Msuva wa Simba B akimtoka beki wa Yanga B
|
Makocha wa Yanga B, Salvatory Edward kulia na Nsajigwa kushoto katia benchi lao leo
|
Mabao ya Yanga SC inayofundishwa na kiungo wake wa zamani, Salvatory Edward anayesaidiwa na beki wa zamani wa timu hiyo, Nsajigwa Shadrack yamefungwa na Amos dakika ya 57 na Sospeter dakika ya 72.
LIVERPOOL YABANWA NYUMBANI KOMBE LA FA NA BLACKBURN ROVERS
6:36 AM
Mshambuliaji
wa Liverpool, Mario Balotelli akimtoka beki wa Blackburn Rovers, Conway
katika mchezo wa Robo Fainali Kombe la FA usiku wa leo Uwanja wa
Anfield. Timu hizo zilitoka sare ya 0-0 na sasa zitarudiana Uwanja wa
Ewood Park kusaka timu timu ya kwenda Nusu Fainali.
BARCA YAPAA KILELENI LA LIGA BAADA YA KUIFUMUA VALLECANO 6-1, MESSI APIGA TATU, SUAREZ MBILI
6:34 AM
BARCELONA
imepanda kileleni mwa La Liga, baada ya ushindi mnono wa mabao 6-1
dhidi ya Rayo Vallecano jana jioni Uwanja wa Nou Camp.
Barca
sasa inafikisha pointi 62, baada ya mechi 26, ikiishushia nafasi ya
pili, Real Madrid yenye pointi 61, baada ya jana kufungwa 1-0 na
Athletic Bilbao.
Luis Suarez alianza kuifungia Barca dakika ya sita, kabla ya Gerard Pique kufunga la pili dakika ya 49.
Barcelona walipata penalti na Tito akatolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kucheza rafu kwenye boksi.
Lionel
Messi alipiga mara ya kwanza penalti akakosa, lakini refa akamuambia
arudie ndipo akafunga dakika ya 56, kabla ya kufunga tena dakika za 63
na 68 kukamilisha hat-trick yake leo.
Alberto
Bueno aliifungia bao la kufutia machozi Vallevano kwa penalti dakika ya
81 na Dani Alves akatolewa kwa kadi nyekundu kwa kucheza rafu iliyozaa
penalti hiyo, kabla ya Suarez kuhitimisha ‘pati la mabao’ la Barca kwa
bao la dakika ya 90.
Kikosi
cha Barcelona kilikuwa: Bravo, Pique, Xavi, Pedro, Iniesta/Rafinha dk66,
Suarez, Messi, Mascherano/Rakitic dk66, Alba/Adriano dk76, Alves na
Mathieu.
Rayo Vallecano:
Alvarez, Tito, Amaya, Ba, Insua, Trashorras, Lica/Aquino dk71,
Jozabed/Quini dk66, Bueno, Kakuta, Baptistao/Manucho dk83.
Luis Suarez amefunga mabao mawili katika ushindi wa 6-1 wa Barcelona dhidi ya Rayo Vallecano
HIVI NDIVYO KUPONOVIC ALIVYO SHANGILIA GOLI LA OKWI
6:31 AM
Anavuta kasi kurusha ngumi hewani |
Tayari ameutandika upepo 'right-hook' ya maana, hizo ni furaha za bao la Okwi |