SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 13, 2015

IVO MAPUNDA ASEMA BARTHEZ ASISHAMBULIWE, OKWI NDIYE APONGEZWE


Kipa mkongwe wa Simba, Ivo Mapunda amemtetea Barthez kwa kusema hastahili lawama kwa bao alilofungwa.

Ivo aliyewahi kudakia Yanga kwa zaidi ya misimu miwili amesema Barthez hastahili kulaumiwa kwa kuwa amefungwa bao bora.

“Bado naamini Barthez ni kipa bora na mwenye uwezo wa juu, hatakiwi kulaumiwa bali Okwi ndiye anatakiwa kupongezwa kwa kufunga bao kiufundi,” alisema Ivo.


Barthez alifungwa bao pekee lililoipa Simba ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga, Jumapili iliyopita.

Okwi alifunga bao akiwa katika kasi kubwa na kupiga mpira wa juu uliompita kipa huyo akiwa ametoka kidogo nje ya lango.

WANACHAMA YANGA SASA RASMI HAWAWATAKI WACHEZAJI WA SIMBA WALIO YANGA


Kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Simba, kimeendelea kuitesa Yanga, hiyo ni baada ya jana asubuhi kufanyika kikao kizito kati ya viongozi wote wa matawi wa Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga kisha kutolewa maoni ‘tata’.

Kikao hicho, kilifanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani na Twiga kikiongozwa na Sanga na Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha ambacho wanachama walidai uwepo wa wachezaji wasio na mapenzi, wakiwemo kutoka Simba, unaweza kuwafanya wacheze bila kujituma.
Sanga amesema katika kikao hicho, viongozi hao wa matawi wameuomba uongozi kufanya uboreshaji wa usajili wao msimu ujao baada ya kutokea minong’ono mingi juu ya hujuma hizo.
“Leo nimekutana na viongozi wa matawi na kujadiliana masuala mbalimbali ya timu, likiwemo la kurejesha morali ya timu baada ya kufungwa na Simba.
“Pia kuwataka kuungana kwa pamoja katika kuelekea mechi yetu na Platinum ya Zimbabwe, hayo ndiyo ya msingi na kubwa zaidi viongozi wa matawi wameomba kuwepo na uboreshaji katika mfumo wa usajili kwa kusajili wachezaji wenye moyo na mapenzi na timu,” alisema Sanga.
Hivi karibuni, kuliibuka maneno kuwa, kuna baadhi ya wachezaji ambao walitua klabuni hapo wakitokea Simba, hawana moyo wa kujituma kama wengine, madai ambayo uongozi wa Yanga umeyakanusha.
Wachezaji waliopo Yanga ambao waliwahi kuitumikia Simba ni Ally Mustapha ‘Barthez’, Kelvin Yondani, Danny Mrwanda, Deogratius Munish ‘Dida’, Amissi Tambwe na Mrisho Ngassa.

CHELSEA SASA IKO TAYARI KUMTWAA VARANE WA REAL MADRID

Chelsea imeamua kuboresha safu yake ya ulinzi na sasa iko tayari kumtwaa beki Raphael Varane wa Real Madrid.

Chelsea iko tayari kumwaga kitita cha pauni 40 kwa ajili ya kumnasa beki huyo inayeelezwa hana furaha.

Varane mwenye miaka 21 amekuwa hana furaha huenda kutokana na kutopata nafasi ya kucheza kwa kiasi kikubwa.


Madrid inawategemea wakongwe Pepe na Sergio Ramos.

HIVI ULIONA HANS POPPE ALIVYOWANANGA YANGA? CHEKI HII HAPA

 Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Han Poppe alitoa kali ya mwaka Jumapili mara tu baada ya watani, Simba na Yanga kumalizika.

Mechi hiyo ilimalizika kwa Simba kushinda kwa bao 1-0 na kuwanyamazisha Yanga.
Lakini kama hiyo haikutossha baada Hans Poppe kusimama mbele ya mashabiki wa Yanga na kuanza kuwahoji kuhusiana na timu yao na mbwembwe nyingi walizokuwa nazo.
 
Hans Poppe aliwakumbusha Simba ilivyoonyesha kiwango hasa dakika za mwisho na kufunga bao bora kabisa.
Halafu baada ya hapo, aliondoka kama hile akiwaachia mkono kwa kusema “nendeni kule.”
Mashabiki wa Yanga walioonyesha kumcharua mtani wao huyo, walibaki kimyaa kwa kuwa ndiyo mpira ulikuwa umemalizika na wana machungu ya kufungwa.

LUKAKU AING'ARISHA EVERTON ULAYA

Lukaku shows a clean pair of heels to Danilo Silva as the Everton frontman begins another attack for the home hopefuls

Mshambuliaji Romelu Lukaku wa Everton akimuacha chini Danilo Silva wa Dynamo Kiev katika mchezo wa Europa League jana usiku Uwanja wa Goodison Park. Everton ilishinda 2-1, mabao yake yakifungwa na Steven Naismith na Lukaku, wakati bao la Dynamo lilifungwa na Oleg Gusev. Timu hizo zitarudiana mjini Kiev Alhamsi ijayo, Everton ikihitaji sare ili kwenda Robo Fainali.

KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO MARCH 13 ZIPO HAPA

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.