SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 18, 2015

MBEYA CITY YANG’ARA, YAILAZA STAND UTD 2-0

MBEYA City imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United ya Shinyanga jioni ya leo Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Mabao ya Mbeya City inayodhaminiwa na kampuni ya Bin Slum Tyres Limited kupitia betri za RB, yamefungwa na Yussuf Abdallah dakika ya 65 kwa penalti na Paul Nonga dakika ya 75.
Ushindi huo unaifanya Mbeya City ifikishe pointi 24 baada ya kucheza mechi 20, wakati Stand inabaki na pointi zake 22 baada ya kucheza mechi 20 pia.

SIMBA YAKALISHWA TANGA, YAPIGWA 2-0 NA MGAMBO, IVO ALIMWA NYEKUNDU, OKWI…

Na Princess Asia, TANGA
SIMBA SC imepunguzwa kasi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kufungwa mabao 2-0 na Mgambo Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga jioni ya leo.
Matokeo hayo yanazidi kuondoa matumaini ya Simba SC inayofundishwa na Mserbia, Goran Kopunovic siyo tu kutwaa ubingwa, bali hata kushika nafasi ya pili. 
Mgambo ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa mchezaji wa zamani wa Coastal Union ya Tanga pia, Ally Nassor ‘Ufudu’ aliyemalizia krosi ya Fully Maganga.
Mapema dakika ya 21, Emmanuel Okwi aliikosesha Simba SC bao la wazi, baada ya kushindwa kuunganisha krosi nzuri ya Ibrahim Hajibu.  
Wachezaji wa Mgambo wakishangilia ushindi wao leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga

Dakika ya 35 pia, Okwi tena alishindwa kuunganisha krosi nzuri ya Hassan Kessy.
Kipindi cha pili ndipo jahazi la Simba lilipozama kabisa, baada ya kuongezwa bao la pili.
Bao hilo lilifungwa na Malimi Busungu kwa penalti dakika ya 66, baada ya kipa Ivo Mapunda kumchezea rafu Fully Mganga aliyekuwa anakwenda kufunga.
Emmanuel Okwi wa Simba SC akimizuia beki wa Mgambo, ili achukue mpira leo Uwanja wa Mkwakwani
Kiungo wa Simba SC, Abdi Banda (kushoto) akipambana na kiungo wa Mgambo 

Ivo alitolewa kwa kadi nyekundu na refa Amon Paul kutoka Mara, na Smba SC ikamuingiza kipa Peter Manyika kwenda kuchukua nafasi ya Said Ndemla. 
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Hassan Kessy, Mohammed ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murushid, Jonas Mkude, Abdi Banda, Said Ndemla/Peter Manyika dk66, Ibrahim Hajibu/Elias Maguri dk46, Emmanuel Okwi/Simon Sserunkuma dk79 na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Mgambo Shooting; Godson Mmasa/Said Lubawa dk60, Bashiru Chanache, Salim Mlima, Salim Kipanga, Ramadhani Malima, Novaty Lufunga, Mohammed Samatta, Ally Nassor, Fully Maganga, Malima Busungu na Salim Aziz Gilla.

YANGA YAREJEA KILELENI LIGI KUU, KAGERA WAPIGWA 2-1 TAIFA

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
YANGA SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Andrew Shamba kutoka Pwani, aliyesaidiwa na Martin Mwaliaje wa Tabora na Hajji Mwalikita wa Tanga, Yanga SC ilikwenda kupumzika ikiwa tayari inaongoza kwa mabao hayo 2-1.
Winga Simon Msuva alianza kufunga bao la kwanza kwa penalti dakika ya nane baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Benjamin Asukile.
Mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Mrundi Amisi Tambwe aliifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 15, akimalizia pasi ya Mrisho Ngassa ambaye naye alipasiwa na Kpah Sherman.
Wafungaji wa mabao ya Yanga SC leo, Amisi Tambwe kulia na Simon Msuva kushoto wakishangilia leo Uwanja wa Taifa

Yanga SC walionekana ‘kuridhika’ baada ya kuwa mbele kwa mabao 2-0 na kucheza kwa mbwembwe, hatimaye kuwaruhusu Kagera kupata bao.
Bao hilo lilifungwa na Salum Kanoni kwa penalti, kufuatia Rajab Zahir kumuangusha kwenye eneo la hatari Atupele Green.
Kagera waliongeza kasi ya mashambulizi baada ya kupata bao hilo, lakini Yanga SC walisimama imara kuwadhibiti wapinzani wao hadi mapumziko.
Kipindi cha pili, timu zote zilishambuliana kwa zamu na kila upande ulikosa mabao zaidi ya mawili ya wazi.
Sherman alipewa pasi nzuri na Ngassa akiwa ndani ya boksi, lakini akazubaa hadi beki wa Kagera, Eric Kyaruzi alipotokea na kuokoa.
Mshambuliaji wa Yanga SC, Mrisho Ngassa kulia akimtoka beki wa Kagera Sugar, Benjamin Asukile
Kpah Sherman akimtoka beki wa Kagera Sugar Benjamin Asukile


Rashid Mandawa naye alipiga nje akiwa kwenye nafasi nzuri dakika ya 64.   Tegete aliyetokea benchi alipoteza nafasi mbili za wazi dakika za lala salama.
Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe pointi 34, baada ya kucheza mechi 17 na kurudi kileleni mwa Ligi Kuu, ikiwazidi kwa pointi moja mabingwa watetezi, Azam FC.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Mbuyu Twite, Salum Telela/Nizar Khalfan dk90, Simon Msuva, Hassan Dilunga, Amisi Tambwe/Hussein Javu dk35, Mrisho Ngassa na Kpah Sherman/Jerry Tegete dk74.
Kagera Sugar; Andrew Ntalla, Benjamin Asukile, Salum Kanoni, Ibrahim Job, Eric Kyaruzi, George Kavilla, Daud Jumanne/Juma Mpola dk36, Babu Ali, Rashid Mandawa, Atupele Green/Adam Kindwande dk63 na Paul Ngway. 

YANGA KUIVAA KAGERA BILA MASTAA WAKE ZAIDI YA WATANO

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC inashuka dimbani leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Kagera Sugar kujaribu kurudi kileleni mwa LIgi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lakini itawakosa wachezaji wake sita tegemeo.
Hao ni beki Kevin Yondan, kiungo Said Juma ‘Kizota’na mshambuliaji Danny Mrwanda, ambao kila mmoja ana kadi tatu za njano na klabu haijawaombea kucheza mechi hiyo.
Kanuni mpya ya Ligi Kuu inaruhusu klabu kumuombea mchezaji mwenye adhabu acheze mechi inayofuata ili aje kukosa mechi za baadaye, lakini Yanga haijajisumbua kufanya hivyo.
Aidha, kiungo mwingine Haruna Niyonzima atakosekana leo kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi nyekundu, wakati beki na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kiungo Andrey Coutinho wao bado hawajapona sawasawa maumivu yao.
Beki tegemeo wa Yanga SC, Kevin Yondan atakosekana katika mchezo wa leo kwa sababu ana kadi tatu za njano

Yanga SC yenye pointi 31, inahitaji ushindi katika mechi ya leo, ili kurejea kileleni, kufuatia juzi mabingwa watetezi, Azam FC kuifunga Ndanda FC 1-0 na kufikisha pointi 33. 
Baada ya mchezo wa leo, Yanga SC itaondoka kesho Dar es Salaam kwenda Tanga kwa ajili ya mchezo mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Mgambo Shooting.
Mara tu baada ya mechi na Mgambo, Yanga SC watageuza Jumapili kurejea Dar es Salaam na Jumatano ijayo watacheza mechi nyingine ya Ligi Kuu ya dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Taifa.
Machi 29, kikosi cha Yanga SC kitakwea ‘pipa’ kuelekea Bulawayo, Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza, Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Platinum FC utakaopigwa kati ya Aprili 3 na 5.
Yanga SC itakwenda kwenye mchezo huo ikiwa na mtaji mzuri wa ushindi wa mabao 5-1 katika mchezo wa kwanza Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo ya marudiano, itachezeshwa na marefa Helder Martins de Carvalho, Jerson Emiliano dos Santos, Wilson Valdmiro Ntyamba na Joao Amado Goma wote wa Angola, wakati Kamisaa atakuwa William Makinati Shongwe kutoka Swaziland.

KILICHO ANDIKWA KWENYE KURASA ZA MWANZO ZA MAGAZETI YA MICHEZO KIPO HAPA

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

MANJI AMPANDISHA KIZIMBANI MFADHILI WA SIMBA, WAKILI NDUMBARO AIBUKIA MAHAKAMANI KUMTETEA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MFADHILI wa muda mrefu wa Simba SC, Muslah Al Rawah leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam kwa shitaka la kumjeruhi mtoto wa Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji, aitwaye Meheub Manji.
Wakili wa Serikali, Genis Tesha amesema wakati hati ya mashitaka kwambwa; Al  Rawah alifanya kosa hilo, Machi 8, 2015 kwenye Uwanja wa Taifa uliopo Chang'ombe .
Tesha amesema siku hiyo ya tukio, mshtakiwa Al Rawah alimpiga teke Meheub Manji na katika sehemu nyingine mbalimbali za mwili ukiwamo uso na kumsababishia majeraha mazito.
Muslah (kushoto) leo amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumpiga teke mtoto wa Manji

Al Rawah pia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Simba SC, anayetetewa na Wakili Damas Daniel  Ndumbalo, alilikana shitaka hilo na upande wa mashtaka ukadai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika
Hata hivyo; baada kusomewa shtaka hilo, upande wa mashtaka uliiambia Mahakama kuwa hauna pingamizi na dhamana. Kwa upande wake, Wakili Ndumbalo naye aliomba mteja wake apewe dhamana.
Hakimu Frank Moshi akitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa huyo, alimtaka awe na mdhamini mmoja ambaye anatoka katika taasisi inayotambulika Serikalini.
Baada ya mdhamini kujitokeza, upande wa mashtaka ulizifanyia uhakiki barua hizo ndani ya saa moja kama ilivyoelekezwa na Mahakama na mshtakiwa akaachiwa huru. 
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 20, 2015 kutoa nafasi upelelezi ukamilike.

MTOTO WA MCHEZAJI YANGA AWA MSEMAJI WA KLABU YA SIMBA

Hajji Sunday katika 'gwanda' la CCM 
MTOTO wa mchezaji wa zamani wa Yanga SC, Sunday Manara ‘Computer’, aitwaye Hajji Sundy ameteuliwa kuwa Msemaji ya klabu ya Simba SC.
Taarifa ya Simba SC iliyotolewa leo, imesema kwamba aliyekuwa Msemaji wa klabu hiyo, Humphrey Nyasio sasa atatafutiwa nafasi nyingine ya kazi katika klabu hiyo.
Pamoja na kwamba baba yake amecheza Yanga na ni mpenzi wa klabu hiyo pia, lakini Hajji ametokea kuwa mpenzi wa Simba SC tangu angali mdogo.
Hajji mwenye ulemavu wa ngozi, maarufu kama albino amewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya Habari Tanzania na pia ni mmoja wa makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM). 

DROGBA AREJEA GALATASARAY, AWASALIMIA WASHIKAJI WAKE

MSHAMBULIAJI DIDIER DROGBA AMEONYESHA ANAJALI KWELI BAADA YA KUREJEA JIJINI ISTAMBUL, UTURUKI NA KWENDA KUWATEMBELEA WACHEZAJI WENZAKE WA ZAMANI WA KIKOSI CHA GALATASARAY ALIYOICHEZEA MSIMU ULIOPITA.



ARSENAL YASHINDA 2-0 LAKINI SAFARI YAWAKUTA, YATOLEWA LIGI YA MABINGWA

Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya AS Monaco wakiwa ugenini. Lakini wametolewa na kushindwa kusonga katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kilichowang’oa Arsenal ni kupoteza kwa mabao 3-1 katika mechi ya kwanza wakiwa nyumbani Emirates, London.
Olvier Giroud na Aaron Ramsey aliyeingia kipindi cha pili ndiyo waliofunga mabao hayo mawili.

Juhudi za Arsenal kusaka bao moja litakalowavusha zilishindikana.

Monaco licha ya kuwa nyumbani, walishindwa kucheza kwa kiwango kizuri cha ushindani. Hata hivyo, Arsenal hawakuwa katika kiwango cha juu sana kushindwa kuupasua mfumo wa ulinzi wa Wafaransa hao.