Van Gaal, sanjari na wachezaji wake mwishoni mwa juma hili
watakabiliwa na mchezo muhimu katika ligi ya nchini England dhidi ya
mahasimu wao wakubwa nchini humo Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Meneja huyo kutoka nchini Uholanzi amethibitisha kukaa kwake pembeni katika mchezo wa soka kama meneja mara baada ya kumalizana na Man utd mwaka 2017, alipozungumza na vyombo vya habari kuelekea katika mchezo huo wa ligi uliopangwa kucheza siku ya jumapili.
Van Gaal, amesema kazi ya kukiongoza kikosi cha Man Utd ni ya mwisho kwake na hafikirii kuendelea kutokana na kuhitaji muda wa kupumzika baada ya kuutimikia mchezo wa soka kwa zaidi ya miaka 20 sasa.
'Nimeshazeeka sasa, hii Itakua kazi yangu ya mwisho' Alisema Van Gaal katika mkutano na waandishi wa habari.
'Nimeshazungumza na familia yangu na kuweka wazi msimamo huu, ambao utanisaidia kuwa karibu na watoto, wajukuu pamoja na mke wangu ambaye kwa kipindi kirefu amekua mpweke kutokana na shughuli nizifanyazo.' Aliongoza Van Gaal
Van Gaal alikubali kukichukua kikosi cha Man Utd baada ya kutimuliwa kwa David Moyes mwishoni mwa msimu uliopita, na alitarajiwa kuwa na mtazamo wa kukibadilisha kikosi cha klabu hiyo msimu huu, lakini mambo yamemuendea kombo.
Kabla ya kuikubali kazi ya Man Utd, Van Gaal alikua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uholanzi ambayo ilishiriki fainali za kombe la dunia huko nchini Brazil na kuishi katika hatua ya nusu fainali, kabla ya kushika nafasi ya tatu kwa kuwafunga wenyeji.