SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 24, 2015

KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO MARCH 24 2015 ZIPO HAPA

.
.
.
.
DSC_0124
.
.

SAMATTA NA ULIMWENGU WAREJEA NYUMBANI JANA KUICHEZEA STARS DHIDI YA MALAWI MWANZA

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
WASHAMBULIAJI wawili wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta watawasili usiku wa leo kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Wawili hao wamo katika kikosi cha wachezaji 27 cha Stars kitakachoingia kambini leo kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Machi 29.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo asubuhi, Ulimwengu amesema wanatarajiwa kutua Dar es Salaam usiku kwa ajili ya majukumu ya kitaifa. “Tunatarajia kuwa Dar es Salaam usiku, tupo njiani hapa,”amesema. 
Samatta kushoto na Ulimwengu kulia watawasili usiku wa jana Dar es Salaam

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, bia inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), inaingia kambini katika hoteli ya Tansoma kujiandaa na mchezo huo kabla ya kuelekea Mwanza machi 24 kwa maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo.
Mbali na Samatta na Ulimwengu, wachezaji wengine walioitwa ni makipa Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga SC, Aishi Manula na Mwadini Ali, wote wa Azam FC, wakati mabeki ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris (Azam FC), Mwinyi Haji (KMKM), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Oscar Joshua (Yanga), Abdi Banda na Hassan Isihaka (Simba SC).
Viungo ni Frank Domayo, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mcha Khamis (Azam FC), Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United).
Washambuliaji Mwinyi Kazimoto (Al Markhiry - Qatar), Simon Msuva, Mrisho Ngassa (Yanga), John Bocco (Azam FC) na Juma Luizio (Zesco United - Zambia)
Malawi inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza machi 27, 2015 ikiwa na kikosi kamili, wakiwemo wachezaji nane wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini, Msumbuji, Congo DR na Zimbambwe.
Malawi inashika nafasi ya 91 katika viwango vipya vya FIFA Duniani vilivyotolewa mwezi huu, huku Tanzania ikipanda kwa nafasi saba na kushika nafasi ya 100.