MOJA YA NDEGE ZINAZOMILIKIWA NA SERIKALI YA TANZANIA. |
Yanga inatarajiwa kwenda Zimbabwe Ijumaa,
tayari kuivaa FC Platinum.
Kikosi cha Yanga kinatarajia kufanya safari
yao ya Zimbabwe kwa kutumia ndege ya serikali.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga
zimeeleza timu hiyo itasafiri na ndege hiyo baada ya Yanga kufanikiwa kupata
kibali.
Uamuzi wa kupanda ndege ya serikali ni
kupunguza gharama lakini pia uhakika kuepuka kutumia ndege za kawaida za abiria
na kuwapa nafasi wenyeji wao kupanga mipango ya kuiangamiza.
Yanga inashuka dimbani dhidi ya Plutinum Jumamosi
ikiwa ugenini baada ya kushinda mabao 5-1 katika mechi ya kwanza ya Kombe la
Shirikisho.
“Kweli, uongozi wa juu unaendelea
kushughulikia suala la safari na tayari upande wa serikali umekubali kuikodisha
ndege yetu,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Yanga inahitaji sare ya aina yoyote ili kusonga mbele na ikifanikiwa itakutana kati ya Etoile du Sahel ya Tunisia au Benfica kutoka Angola.