KLABU
ya Arsenal inasikilizia msimamo wa mwisho wa Petr Cech juu ya
mustakabali wake kabla ya haijamtokea kipa huyo huyo wa Chelsea.
Kipa
huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech anajipanga kuondoka Stamford
Bridge mwishoni mwa msimu, na klabu hiyo inajiandaa kuachana na kipa
huyo lakini kwa dau la Pauni Milioni 10 au zaidi.
Lakini kwa Cech kuhamia Arsenal, wapinzani wa Chelsea linaweza kuwa jambo gumu.
Cech, aliyejiunga na Chelsea mwaka 2004, amecheza mechi nne tu za Ligi Kuu England msimu huu
Na
Gunners wanataka kujiridhisha wana nafasi nzuri ya kumsajili kipa huyo,
kabla ya kumtokea, huku Chelsea ikitarajiwa kutokuwa tayari kuwauzia
silaha wapinzani.
Cech
alisema wiki iliyopita kwamba hataki kuona msimu ujao anaendelea kuwa
kipa wa pili nyuma ya Thiabut Courtois Uwanja wa Stamford Bridge.
Mkongwe
huyo mwenye umri wa miaka 32 amepoteza nafasi kikosi cha kwanza The
Blues tangu kurejeshwa kwa Mbelgiji huyo msimu huu, akiwa amedaka mechi
nne tu za Ligi Kuu ya England, huku zaidi akichezeshwa kwenye mechi za
vikombe.