Na Alex Sanga, SHINYANGA
STAND United ya Shinyanga inainyatia saini ya kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Juma Kaseja, imeelezwa.
Mkurugenzi wa benchi La Ufundi wa Stand United, Muhibu Kanu ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, wana mipango ya kumsajili kipa huyo wa zamani wa Simba na Yanga, Juma Kaseja kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
“Kaseja ni kipa mzuri, mzoefu ambaye tunaamini bado ana uwezo mkubwa na atatusaidia tukiwa naye,”amesema.
Kwa sasa, Juma K Juma ni mchezaji huru baada ya kujiondoa katika klabu yake, Yanga SC akiishutumu kukiuka vipengele vya Mkataba baina yao. Hata hivyo, Yanga SC imemfungulia kesi Kaseja ambayo inaendelea Mahakama ya Kazi.
Kwa upande wake, kocha wa Stand United, Mganda Mathias Lure amesema kwamba ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Jumapili umeamsha morali ya wachezaji wake na sasa watapambana zaidi wasishuke.
"Mechi yetu ijayo itakuwa siku ya Jumapili na tunacheza na Polisi Morogoro, kisha tunabakiza mechi sita, dhidi ya Ruvu Shooting, JKT Ruvu
tukiwa nyumbani na ugenini tutacheza na Azam, Yanga na Coastal Union,”amesema Luren ambaye timu yake ipo katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 24.