Apr 20, 2015
KIUNGO ‘BABU KUBWA’ ANAYELIPWA MILIONI 44 KWA MWEZI TAYARI KUTUA YANGA SC
8:07 AM
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KIUNGO anayelipwa dola 25,000 za Kimarekani kwa mwezi Etoile du Sahel ya Tunisia, (zaidi ya Sh. Milioni 44 za Tanzania), Mcameroon Franck Kom amesema yuko tayari kutua Yanga SC iwapo wataweza kumlipa mshahara huo.
Kom aliwapoteza kabisa viungo wa Yanga Jumamosi katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam timu hizo zikienda sare ya 1-1.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY juzi mjini Dar es Salaam, kiungo huyo aliyekuwa akiichezesha vyema timu yake, alisema kwamba anaweza kuja kucheza Tanzania.
Baada ya mechi Kom alikwenda kwenye benchi la Yanga kusalimiana na wachezaji wa timu hiyo na akatumia muda zaidi kuzungumza na kiungo wa DRC, Mbuyu Twite.
Kom alionyesha kumpenda Mbuyu Twite japo ndiyo walikuwa wanakutana kwa mara ya kwanza siku hiyo na wakapeana mawasiliano.
Alipoulizwa kama anaweza kujiunga na Yanga ikimhitaji, Kom alisema; “Kwa nini hapana, ninaweza kama wataweza kunilipa kama ninavyolipwa Etoile,”alisema mchezaji huyo ambaye wakala wake ni kampuni ya Smart Sports Management inayomilikiwa na Jacques Dongmo. Aidha, Kom aliyetua Etoile mwaka 2011 akitokea Panthere du Nde inayotumia jezi kama za Yanga kijani na njano, ya kwao Cameroon aliyoanza kuichezea mwaka 2009 amesema ndoto zake kubwa ni kucheza Ulaya.
“Nacheza Afrika kutafuta nafasi ya kucheza Ulaya, timu yoyote inayocheza haya mashindano ya Afrika, kama inaweza kunilipa vizuri naweza kujiunga nayo,”amesema mchezaji huyo ‘fundi’ mwenye umri wa miaka 23.
Kom ni mchezaji wa timu ya taifa ya Cameroon na alikuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2010 nchini Angola walipotolewa Robo Fainali na Tunisia.

Frank Kom kushoto akizungumza na BIN ZUBEIRY juzi baada ya mechi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam |
Kom alionyesha kumpenda Mbuyu Twite japo ndiyo walikuwa wanakutana kwa mara ya kwanza siku hiyo na wakapeana mawasiliano.
Alipoulizwa kama anaweza kujiunga na Yanga ikimhitaji, Kom alisema; “Kwa nini hapana, ninaweza kama wataweza kunilipa kama ninavyolipwa Etoile,”alisema mchezaji huyo ambaye wakala wake ni kampuni ya Smart Sports Management inayomilikiwa na Jacques Dongmo. Aidha, Kom aliyetua Etoile mwaka 2011 akitokea Panthere du Nde inayotumia jezi kama za Yanga kijani na njano, ya kwao Cameroon aliyoanza kuichezea mwaka 2009 amesema ndoto zake kubwa ni kucheza Ulaya.
Kom alitumia muda zaidi kuzungumza na kiungo Mbuyu Twite, raia wa DRC siku hiyo |
“Nacheza Afrika kutafuta nafasi ya kucheza Ulaya, timu yoyote inayocheza haya mashindano ya Afrika, kama inaweza kunilipa vizuri naweza kujiunga nayo,”amesema mchezaji huyo ‘fundi’ mwenye umri wa miaka 23.
Kom ni mchezaji wa timu ya taifa ya Cameroon na alikuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2010 nchini Angola walipotolewa Robo Fainali na Tunisia.
HANS POPPE AWACHOKOZA YANGA, AWAAMBIA; “MTAFUNGWA TUNISIA, NA PIGA, UA MSUVA ATAVAA JEZI NYEKUNDU”.
8:04 AM
Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameendeleza wimbi la kuitisha la kuitisha timu ya Yanga baada ya kutamba kwamba winga wa timu hiyo Simon Msuva ni damu ya Simba ana atatua Msimbazi msimu ujao.
Poppe ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha TAMASHA LA MICHEZO kinachorushwa na kituo cha Luninga cha ITV kila siku ya jumapili saa nane kamili mchana.
Alisema kuwa kwasasa wataendelea kuitesa timu ya ya Yanga kwakuendeleza wimbi la kuifunga kutokana na wao kuwa na mbinu nyingi za ndani na nje ya uwanja kila wanapokutana katika michuano yeyote.
Amedai sababu za kuifunga Yanga mara kwa mara wanazijua na baadhi ya mbinu hizo ni kuwavuruga na maneno kabla ya mchezo na kwamba wapo wachezaji wengi waliyowahi kuitumikia Simba ambao kwasasa wapo Yanga na hivyo kuiona Yanga kama ni Simba B.
``Wale Yanga sisi tunawaona kama ni Simba B kwakuwa wao wanaona kutuchukulia wachezaji wetu ndiyo sifa ya kutufunga jambo ambalo siyo kweli,tutaendelea kupa supu yam awe na kachumbari ya miba mpaka wawache wachezaji wetu``. Alisema Pope.
Alipoulizwa kama wamaechana na harakati za kumuhitaji winga Simon Msuva, Poppe alisema kuwa bado wanamuhitaji Mchezaji huyo kwakuwa ni `mtoto` wao na harakati za kumuwinda haziwezi kukoma mpaka hapo atakapovaa jezi Nyekundu za Simba.
``Yule Msuva ni kijana wetu toka siku nyingi tunajua Yule ni Simba damu na na anamapenzi na Simba hivyo lazima tuhakikishe anakuja Nyumbani kucheza Soka`. Alisema Mwenyekiti huyo wa Usajili asiyeogopa kutoa kauli zenye kuumiza.
Hakuishia hapo aliendelea kuimbea Yanga mabaya ili itupwe nje ya michuano ya Shirikisho na timu ya Etoel du Sahil ya Tunisa katika Mchezo wa marudiano utakaopigwa huko Tunisia wiki mbili zijazo.
``Mimi naomba Mungu Yanga itolewe hata kwakufungwa mabao nane,kwakuwa siipendi hii timu hata kidogo`.Aliongeza.

Hans Poppe kushoto amesema anaitakia dua mbaya Yanga SC ifungwe na Etoile |

Hans Poppe amesema Msuva atavaa jezi nyekundu |
Hakuishia hapo aliendelea kuimbea Yanga mabaya ili itupwe nje ya michuano ya Shirikisho na timu ya Etoel du Sahil ya Tunisa katika Mchezo wa marudiano utakaopigwa huko Tunisia wiki mbili zijazo.
``Mimi naomba Mungu Yanga itolewe hata kwakufungwa mabao nane,kwakuwa siipendi hii timu hata kidogo`.Aliongeza.
YANGA SC WAINGIA KAMBINI LEO, KESHO WANA STAND UNITED TAIFA
8:02 AM
Kocha wa Yanga SC, Hans van der Pluijm |
YANGAS SC wanarudi kambini leo baada ya mapumziko ya siku moja, kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Stand United kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga SC walilazimishwa sare ya 1-1 na Etoile du Sahel ya Tunisia katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika juzi Uwanja wa Taifa.
Na kabla ya kwenda Tunisia katika mchezo wa marudiano, Yanga SC watakuwa na mechi tatu za Ligi Kuu kesho na Mgambo na mwishoni ma wiki dhidi ya Polisi Morogoro na mwanzoni mwa wiki ijayo na Ruvu Shooting.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba timu inaingia kambini leo na habari njema ni kwamba, kiungo aliyekuwa majeruhi, Salum Telela amepona.
“Habari njema ni kwamba kiungo wetu tegemeo, Salum Telela aliyekuwa majeruhi amepona na atakuwepo dhidi ya Stand,”amesema.
Telela alikosekana dhidi ya Etoile Jumamosi kutokana na maumivu ya enka aliyoyapata katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City wiki iliyopita.
Kwa ujumla, Ligi Kuu itaendelea mwishoni mwa wiki kwa Mbeya City kuwakaribisha Kagera Sugar, Simba SC na Ndanda FC, Azam FC na Stand United, Polisi Morogoro na Coastal Union Jumamosi, wakati Jumapili Mtibwa Sugar wataikaribisha JKT Ruvu na Prisons watakuwa wenyeji wa Mgambo JKT.