Apr 28, 2015
TAMBWE AZIDI KUWAUMIZA ROHO SIMBA
7:01 AM
AMISSI Tambwe ameendelea kuonesha
thamani yake na kuwadhihirishia Simba kuwa yeye ni mfungaji hatari
baada ya jana kupiga magoli matatu ‘hat-trick’ katika ushindi wa magoli
4-1 dhidi ya Polisi Moro.
Yanga walichukua ubingwa wa ligi
kuu Tanzania bara msimu wa 2014/2015 baada ya ushindi wa jana
wakifikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Mwaka jana Simba walimuacha
Tambwe katika mazingira ya utata akiwa ndiye mfungaji bora na dakika za
mwisho za dirisha dogo la usajili desemba mwaka jana Yanga wakamsajili
kwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja.
Katika mechi tatu zilizopita, Tambwe amefunga magoli nane na kufikisha magoli 14 katika msimu huu mgumu wa ligi kuu.
Alifunga manne katika ushindi wa
8-0 dhidi ya Coastal, akatia kambani moja kwenye ushindi wa 3-2 dhidi ya
Stand United na jana akapiga tatu dhidi ya Polisi Moro.
Baada ya kufanikiwa kwa muda mfupi ndani ya Yanga, Tambwe amesema anafurahia maisha ndani ya Yanga na ataendelea kufanya vizuri.
“Nashukuru nimefunga ‘Hat-trick’
yangu ya pili msimu huu, nikiwa Simba nilifunga ‘hat-trick’ mbili pia,
kwangu haya ni mafanikio, nilipochukua kiatu cha dhahabu mwaka jana
nilisikitika kuachwa na Simba, kichwa changu hakikuwa sawa”, Amesema
Tambwe na kusisitiza: “Leo hii (jana) nachukua ubingwa Yanga nikifunga
magoli muhimu, namshukuru Mungu, wachezaji wenzangu, mashabiki na
viongozi, wanaonesha upendo mkubwa kwangu”.
MSUVA AZUNGUMZIA GOLI LAKE LINALO FANANA NA LA VAN PERSIE
6:53 AM
SIMON Happygod Msuva amesema
anajisikia furaha kuchukua ubingwa huku goli lake alilofunga
kwa kichwa dhidi ya Ruvu Shooting likijadiliwa mno kwenye mitandao ya
kijamii na kufananishwa na alilofunga mshambuliaji wa Manchester United
na Uholanzi, Robin van Persie kwenye fainali za kombe la dunia mwaka
jana nchini Brazil.
“Watu wanasema nilifunga kama
Robin Van Persie, wanajadili sana kwenye mitandao, haya ni mafanikio
kwangu, juhudi ndio siri ya mafanikio” Amesema Msuva.
Winga huyo anayeongoza orodha ya
wafungaji akiwa amefumania nyavu mara 17 msimu huu akifuatiwa na Amissi
Tambwe mwenye magoli 14 ameongeza kuwa ubingwa waliopata anafurahi
kuchangia kwa kiasi kikubwa na ataendelea kufanya vizuri.
“Huu ni mwanzo tu, kila siku
najifunza na kupunguza makosa, tuna kocha mzuri, tunaamini tutafanya
vizuri zaidi siku zijazo tukianzia na mechi ijayo dhidi ya Etoile du
sahel”. Amesema Msuva.
JOHN TERRY 'ANAVYOMSUTA' BENITEZ AELEKEA KUCHEZA MECHI 38 ZA MSIMU BILA TATIZO
6:38 AM
MIAKA miwili ilitopita, kocha Rafa Benitez alipokuwa wa Chelsea mustakabali wa beki John Terry ulikuwa shakani Stamford Bridge.
Aprili
mwaka 2013, kocha huyo Mspanyola alisema kwamba hawezi kuendelea
kumchezesha mechi mbili kwa wiki na uamuzi huo wa utata ulitokana na
maumivu ya goti ya mwanasoka huyo wa zamani wa kimataifa wa England.
Terry alichezeshwa mechi 14 tu katika msimu wa 2012-2013 kwenye klabu hiyo kipenzi. Leo mwaka 2015, Nahodha huyo wa Blues anakarinia kuinua taji la Ligi Kuu ya England akiwa ametoa mchango wake katika mechi kati ya 33 ilizocheza Chelsea hadi sasa.
Na sasa mkongwe huyo anaelekea kucheza mechi zote 38 za msimu wa Ligi Kuu Chelsea. hakika ni jambo la kujivunia kwake.
Terry alichezeshwa mechi 14 tu katika msimu wa 2012-2013 kwenye klabu hiyo kipenzi. Leo mwaka 2015, Nahodha huyo wa Blues anakarinia kuinua taji la Ligi Kuu ya England akiwa ametoa mchango wake katika mechi kati ya 33 ilizocheza Chelsea hadi sasa.
Na sasa mkongwe huyo anaelekea kucheza mechi zote 38 za msimu wa Ligi Kuu Chelsea. hakika ni jambo la kujivunia kwake.
Nahodha wa Chelsea, John Terry anaelekea kucheza mechi zote 38 za Ligi Kuu msimu huu