MSHAMBULIAJI
Robin van Persie usiku huu amefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1
wa U21 ya Manchester United dhidi ya vijana wenzao wa Fulham Uwanja wa
Craven Cottage.
Van Persie
ambaye amekuwa nje ya Uwanja tangu Februari kutokana na majeruhi,
alifunga mabao hayo katika dakika za 13 na 80, huku mabao mengine ya
United yakifungwa na Joe Rothwell dakika ya 20 na 43.
Mholanzi
huyo, Van Persie alirejea uwanjani kikosi cha kwanza cha United
Jumapili timu hiyo ikifungwa 3-0 na Everton katika LIgi Kuu ya England.
Kikosi
cha Fulham kilikuwa: Norman, Donnelly, Buatu, Baba, Sheckleford, Mesca,
Edun/de la Torre dk67, Smile, Evans, Plumain, Redford/Humphreys dk60.
Manchester
United: Lindegaard, Love, Blackett, Thorpe, Kellett, Rothwell/Willock
dk81, Goss/Fletcher dk88, Grimshaw, Pereira, Van Persie/Weir dk81 na
Januzaj.
Van
Persie akipongezwa na wenzake baada ya kufunga mabao mawili katika
ushindi wa 4-1 wa U21 ya Manchester United dhidi ya Fulham usiku wa
Jumanne