REKODI YA GORAN KOPUNOVIC SIMBA SC
Simba SC 1-0 Mafunzo (Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 1-0 JKU (Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 4-0 Taifa Jang’ombe (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 1-0 Polisi (Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 0-0 Mtibwa Sugar (Simba ilishinda penalti 4-3 Fainali Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 2-0 Ndanda FC (Ligi Kuu)
Simba SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu)
Simba SC 1-2 Mbeya City (Ligi Kuu Taifa)
Simba SC 2-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
Simba SC 0-0 Coastal Union (Ligi Kuu)
Simba SC 2-0 Polisi Moro (Ligi Kuu)
Simba SC 0-1 Stand United (Ligi Kuu)
Simba SC 5-0 Prisons (Ligi Kuu)
Simba SC 1-0 Yanga SC (Ligi Kuu)
Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
Simba SC 0-2 Mgambo Shooting (Ligi Kuu)
Simba SC 3-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
Simba SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
Simba SC 3-0 Toto Africans (Kirafiki Mwanza)
Simba SC 0-2 Mbeya City (Ligi Kuu)
Simba SC 4-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
Simba SC 3-0 Ndanda FC (Ligi Kuu)
Simba SC 2-1 Azam FC (Ligi Kuu)
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KOCHA wa Simba SC, Goran Koponovic amesema kwamba amemaliza ubishi juu ya timu ipi bora kati yao, Yanga na Azam FC.
Kauli
ya Mserbia huyo inafuatia jana kuwafunga waliokuwa mabingwa watetezi,
Azam FC mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na
kwa kuwa tayari aliwafunga mabingwa wapya, Yanga SC 1-0 katika Ligi
Kuu- Kopunovic amesema hiyo inatosha Simba SC kuwa bora zaidi ya
wapinzani wake hao.
Alisema
licha ya kutotwaa ubingwa, huku akiiombea mabaya Azam ipoteze mechi
zake mbili zilizobaki, lakini anajivunia kikosi bora kuliko timu zote za
Ligi Kuu Bara.
“Leo
nimemaliza ubishi wa kipi kikosi bora, nimemaliza leo kwamba timu yangu
ni bora, hivyo Jumatano nikiwa katika mazoezi akili yangu itakuwa Taifa
kwa kuiombea Azam ipoteze mchezo (dhidi ya Yanga) huo ili ipoteze
mwelekeo wa nafasi ya pili,'' alisema Goran.
Kocha
huyo amesema anaipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa na pia akawapa pole
kwa kutolewa katika Kombe la Shirikisho kufuatia kufungwa 1-0 juzi na
Etoile du Sahel nchini Tunisia.
Kufuatia
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC jana Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, Simba SC imefikisha pointi 44 baada ya kucheza mechi 25. Azam
inabaki na pointi zake 45 za mechi 24 katika nafasi ya pili, wakati
tayari Yanga SC imejihakikishia ubingwa baada ya kufikisha pointi 55 za
mechi 24.
Simba SC
sasa inaiombea dua mbaya Azam FC ipoteze mechi zake zote mbili
zilizobaki dhidi ya Yanga na Mgambo- na wenyewe (Simba SC) washinde
mechi yao ya mwisho, ili kumaliza katika nafasi ya pili waweze kucheza
Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Tangu
atue Msimbazi Januari mwaka huu, Kopunovic ameiongoza Simba SC katika
mechi 23 kati ya hizo, imeshinda 17, imefungwa tatu na sare tatu.