SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 8, 2015

DADA YAKE ADEBAYOR AMPA MAKAVU KAKA YAKE KUHUSU POST YA JANA…SOMA ALICHOKISEMA

DADA ADDE2
Baada ya status ya Adebayor ambayo ilishtua watu wengi kwenye mtandao hao mchezaji Didier Drogba alimpost Adebayor na kumuombea mambo ambayo yanaenda vibaya na familia yake yaende vizuri. Sasa kwenye ile ile post dada yake Adebayor anaitwa Lucia Adebayor amemjibu akienda kinyume na status ya Ade.
Tafsiri yake kwa ufupi ni hii hapa,
“Endelea kuongopea kaka, yako wapi magari uliyompa mama. Umeyachukua yote. nyumba unayosema umemnunulia dada vyote ni uongo. Simu alizoiba Rotimi vyote ni uongo. Pesa sio kila kitu, sisi ni familia na hatukuitaji tena uwe peke yako na sisi tuwe peke yetu. Ukweli kwamba unazo sasa hivi lakini havikuhakikishi mambo ya kesho. Mungu akusamehe.”
DADA ADDE

MGHANA MPYA SIMBA, ILIKUWA NI SHUGHULI NZITO DHIDI YA MGANDA



 Ingawa ni mazoezi lakini ushindani mkali kati ya beki Mganda, Juuko Murishid dhidi ya Mghana, Aboagye Nelson haikuwa kazi ndogo.

Katika mazoezi ya Simba kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam (UDSM), Aboagye ambaye anafanya majaribio Simba akiwaniwa kusajiliwa, alikuwa akijaribu kuonyesha uwezo wake kwa kuwatoka mabeki mara kadhaa.

Hali hiyo ilionyesha kutokubalika kwa Murishid, ambaye alikuwa akipambana naye vilivyo utafikiri ni mechi.

Hali hiyo iligeuka kuwa burudani kwa wengine huku Mghana huyo naye akionekana kuwa mbishi ile mbaya.


YAYA KUIHAMA MANCHESTER CITY

YAYA_TOURE

Huku msimu wa ligi ukiwa si wa mafanikio kwa Manchester City baada ya klabu hiyo kushindwa kutetea taji lao la ligi kuu ya England ambalo walitwaa msimu uliopita na pia wakishindwa kwenda mbele kwenye michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kutolewa kwenye hatua ya 16 bora , hali imezidi kuwa mbaya kwa Manchester City baada ya taarifa za kuondoka kwa kiungo wake wa kutegemewa Yaya Toure kuibuka .
Wakala wa kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure Dimitri Seluk amevithibitishia vyanzo mbalimbali vya habari hii kuwa mteja wake ana asilimia 90% ya kuihama klabu hiyo baada ya kumalizika kwa msimu huu .
Wakala huyo amefichua kuwa uhusiano wa Yaya na Manchester City umekuwa mbovu na imefikia hatua mbaya kiasi cha mchezaji huyo kufanya maamuzi ya kuondoka na kufikia uamuzi ambao hawezi kuubadilisha .
Itakumbukwa kuwa Kiungo huyo aliingia kwenye ugomvi ambao uliripotiwa sana kwenye vyombo vya habari mwaka jana wakati klabu yake iliposhindwa kumfanyia hafla ya siku yake ya kuzaliwa wakati City ilipokuwa kwenye ziara ya huko Falme Za Kiarabu ripoti ambazo baadae zilikanushwa.

Yaya Toure amehusishwa na kuungana na kocha wake wa zamani Roberto Mancini anayefundisha klabu ya Inter Milan .
Yaya Toure amehusishwa na kuungana na kocha wake wa zamani Roberto Mancini anayefundisha klabu ya Inter Milan .
Wakati hayo yakiendelea Yaya Toure kwa nyakati kadhaa wamekuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na kocha wake wa zamani Roberto Mancini ambaye kwa sasa anaifundisha Inter Milan .
Kwa upande wa uongozi wa Man City inasemekana kuwa klabu hiyo inajiandaa kusikiliza ofa zitakazokuja kwa ajili ya mchezaji huyo kutokana na umri wake kusogea huku uongozi ukiwa na mpango wa muda mrefu wa kujenga kikosi cha City kwa kuwategemea zaidi wachezaji wenye umri mdogo .

Jinsi mastaa wa Afrika walivyomuandikia Adebayor kwenye mgogoro wa familia

LONDON, ENGLAND - FEBRUARY 09:  Emmanuel Adebayor of Tottenham Hotspur reacts during the Barclays Premier League match between Tottenham Hotspur and Everton at White Hart Lane on February 9, 2014 in London, England.  (Photo by Shaun Botterill/Getty Images)
(Photo by Shaun Botterill/Getty Images)
Siku chache baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Togo na Tottenham Hotspurs Emanuel Sheyii Adebayor kufichua siri kadhaa nzito za ugomvi na familia yake, mastaa kadhaa wa Afrika wamemuunga mkono kwenye hii ishu.
Moja kati ya mapacha wanaoiunda P-Square Peter amemuunga mkono Adebayor ambapo amemsifu kwa ujasiri wake na jinsi alivyojitokeza kuwa muwazi na kutoa yanayomsibu maishani mwake.
Mwanamuziki Peter wa kundi la P-Square amemuunga mkono Adebayor kwa kitendo chake cha kufichua mgogoro ulioko kati yake na familia yake .
Mwanamuziki Peter wa kundi la P-Square amemuunga mkono Adebayor kwa kitendo chake cha kufichua mgogoro ulioko kati yake na familia yake .
Peter amemuandikia Adebayor kwa kuandika ‘Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayekudai lolote , familia yako inapaswa kuona fahari kuwa na mtoto kama wewe na si kinyume chake ‘.
Nyota wa zamani wa Arsenal Emmanuel Frimpong kwa upande wake aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter ambapo amesema kuwa baada ya kusoma kilichomsibu Adebayor anashukuru Mungu kwani familia yake ni kila kitu kwake .
Nyota wa Chelsea na mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast Didier Drogba naye alionyesha kumuunga mkono na amemuombea kwa Mungu na anajua ipo siku familia ya Adebayor itarudi katika msingi wa familia zote ambao ni Upendo.
Nyota wa Chelsea Didier Drogba naye amejitokeza kumpa 'Support' Adebayor katika mgogoro wake na familia yake.
.
Didier Drogba ni mmoja kati ya watu ambao wamekuwa karibu na Adebayor katika kipindi hiki kigumu na inasemekana kuwa alizungumza na Adebayor saa chache kabla ya kuandika waraka mrefu kwenye mtandao wa Facebook .
Adebayor amefichua mgogoro mkubwa ulioko baina yake na ndugu zake pamoja na mama yake mzazi ambapo amesema kuwa kilichomfanya afanye hivyo ni kutoa fundisho na picha halisi ya jinsi ambavyo familia za Afrika zina shinikizo kwa vijana waliofanikiwa.
Dada wa Adebayor anayefahamika aitwae Lucia amejibu mapigo ya waraka ulioandikwa na Adebayor ambapo amesema kuwa kila kilichoandikwa na staa huyu wa soka ni uongo na kwa sasa familia yake haimuhitaji.

MAN UNITED YANASA 'BONGE LA KIFAA' LA UHOLANZI, KILA KITU SAFI

KLABU ya Manchester United imefanikiwa kushinda mbio za kuwania saini ya Memphis Depay baada ya mchezaji huyo na wakala wake kufanya mazungumzo mazuri na Louis van Gaal kuhusu uhamisho wa Pauni Milioni 25.
Klabu hiyo imethibitisha uhamisho huo leo na Depay atajiunga na United - iwapo akifaulu vipimo vya afya dirisha la usajili litakapofunguliwa Juni.
United imesema kupitia ukurasa wake Twitter: 'Manchester United imefikia makubaliano na PSV Eindhoven na Memphis Depay kwa uhamisho wa mchezaji huyo, iwapo akifaulu vipimo vya afya,". 
PSV Eindhoven's  Depay celebrates with the trophy after securing the Eredivisie championship last month
Winga wa PSV Eindhoven, Depay akisherehekea na taji la Ligi Kuu Uholanzi, maarufu kama Eredivisie mwezi uliopita

WASIFU WA MEMPHIS

Kuzaliwa: Februari 13, 1994
Nafasi: Winga
Klabu: PSV Eindhoven 2011-
2014/15 season
Mechi alizocheza: 35
Mabao aliyofunga: 24 
"Itategemea na kama atafaulu vipimo vya afya, mpango utakamailishwa mara dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi Juni.'
Kocha wa PSV, Philip Cocu ametangaza hatua ya kikosi chake asubuhi ya Alhamisi. 
Mkurugenzi wa Usajili, Marcel Brands amesemea kupitia tovuti ya PSV; "Tunajivunia sana juu ya uhamisho huu ujao. Memphis ametokea kwenye mpango wa soka ya vijana katika akademi ya PSV na ametoa mchango mkubwa kwa timu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Uholanzi msimu huu.
Depay celebrates winning the Eredivisie with PSV
The PSV star also appeared at the World Cup with Holland
Depay akishangilia na taji la Eredivisie na kulia akiichezea Uholanzi katika Kombe la Dunia