SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 11, 2015

PART 2 : JAMANI ADEBAYOR KATUPA STORY NYINGINE KUHUSU FAMILIA YAKE ISOME HAPA

NBNB
Emannuel Adebayor ameendelea kuelezea yale ambayo tulikua hatuyajui yanaendelea nyuma ya pazia kwenye maisha yake. Sasa leo ametoa part 2 lakini pia ametoa ahadi ya kuendelea part 3. Hii hapa ni tafsiri ya post yake.
Hii ni sehemu nyingine ya story ambayo nilikaa nayo sana. Leo najiskia sababu ya kuitoa. Kama nikitoa story yangu naamini kwamba kila story inakuja na somo, somo kwa kila mtu ambae anasoma hii story. Hii ni kuhusu mdogo wangu anaeendelea kusema hadi leo kwamba mimi sio mtu ninae support familia yetu.
Jina lake ni Rotimi Adebayor ambae katika umri wa miaka 13 alifanya kitu kibaya, mimi na yeye tulijua nini amefanya. Kwasababu ya hicho kitu wazazi wetu ikabidi wampeleke mbali kabisa nje ya jiji.
Wakati nimeanza kupata mafanikio kwenye soka nikaenda Togo kwa ajili ya likizo, mmoja kati ya marafiki wa mama yangu alikuja kutoka kijijini kututembelea nakutuambia jinsi gani Rotimi anapata tabu kijijini. Nikaomba wamrudishe mjini na alivyorudi nikampeleka shuleni, hicho kitu kwangu ni kawaida.
Mwaka 2002 nilienda kucheza AFCOM huko Mali na nikapata nafasi nzuri ya kubadilishana jezi na Marc Vivien Foe, roho yake ilale mahali pema peponi. Nilivyorudi Togo nikaweka ile jezi sehemu nzuri. Rotimi akaaiba na kwenda kuiuza.
Nilivyohama Metz kwenda Monaco, tukafika hatua ya kucheza dhidi ya Real Madrid. Ulikua ni wakati mzuri kwangu kwasababu nilipata nafasi ya kupewa jezi iliyokua signed na mkongwe Zinedine Zidane.Nilivyorudi nayo Togo, Rotimi akaiiba na kwenda kuiuza.
Wakati nipo Metz nilikua nalipwa €15,000 kwa mwezi, nilitaka kupata kitu maalum kwa ajili ya mama yangu angalau kumshukuru kwa alichokifanya kwa ajili yangu.Nilitaka kumfanya afurahi, kwa hiyo nikachukua mshahara wangu wa miezi mitatu na nikamnunulia kidani cha karibia €45,000. Rotimi na rafiki zake walikiiba na kuuza kwa €800.
Mama alivyojua kuhusu hiyo ishu akasema nimuache kwasababu Rotimi ni mtoto wa mwisho. Japokua kuna huu mkasa lakini napenda kuwatakia wakina mama wote siku nzuri ya wakina mama. Happy Mother’s Day!
Kwenye nyumba yangu nina chemba cha kuhifadhia baadhi ya vitu vyangu nikirudi Ulaya kucheza soka. Mimi ndio mtu pekee mwenye funguo lakini Rotimi na ujanja wake akafanikiwa kupata funguo inayofungua kila mlango. Mara nyingi anaiba vinywaji na vitu vingine kwenye hicho chumba,
Baada ya yote na tunasema damu nzito kuliko maji tukayaacha hayo na tukaendelea mbele. Sasa nikaamua kumpeleka na yeye ambapo mimi nilianza kucheza mpira huko Ufaransa. Nilijitahidi kumpeleka kwenye academy nzuri ya soka. Tayari ushajua nini kiliendelea, aliiba simu za mkononi karibia za kila mchezaji na wakamfukuza.
Lakini baada ya kuandika story ya mara ya kwanza alinipigia simu na kuniambia eti hakuiba simu 21. Aliiba simu chache sio nyingi hivyo, lakini hiyo inakubalika kweli?. Pia aliniambia niwe na furaha kwamba anaiba vinywaji na vitu vingine kwenye vyumba vyangu. Nilivyomuuliza kwanini kasema eti yeye si mdogo wangu.
ade
Jacques Songo’o ambae kwasasa ni mchezaji aliyestafu huko Cameroon alikua na mtoto wake kwenye academy ambae alikua rafiki wa Rotimi. Ngoja niongeze kwamba Songo’o alikua na mchango mkubwa kwenye ukuaji wangu kama mchezaji. Wakati nipo Togo alinipigia simu akiwa na hasira akiniambia jinsi gani Rotimi amemuibia mwanae PSP. Nilivyomuuliza Rotimi alisema mtoto wa Songo’o aliisahau PSP kwenye begi lake(la Rotimi). Utasahau vipi na kusafiri na kitu cha mtu kutoka Ufaransa hadi Togo. Tangu siku ile uhusiano wangu na Songo’o umepungua na amekua mbali kidogo na mimi.
Bado nilikua Monaco ambapo niliamua kukusanya viatu vya kuchezea mpira ili nikawape wachezaji wanacheza mpira Africa. Nilikua na begi kubwa lenye viatu vingi. Nikaja nalo hadi togo, nikaanza kuwapa watu vile viatu. Baada ya muda nikaona lile begi limepotea. Nikaja kugundua kwamba alieiba ni Rotimi na kaenda kuuza sokoni Hedzranawoé soko maarufu kwetu Togo.
Siku moja mama alinipigia simu asubuhi sana ambapo bado nilikua nimelala. Akaniambia Rotimi kapata visa ya kwenda Dubai ili akacheze mpira huko.Alitakiwa kuondoka na rafiki yake Kodjovi ambae na yeye pia alikua kwenye hali hiyo hiyo.Nikamwambia mmoja kati ya watu wangu kipindi kile awatafutie ticket za ndege wote wawili, siku ile tukakosa ticket za Economy so wote wawili niliwanunulia first class ticket.
Ilikua ni nafasi yake yeye kuanzisha maisha yake ya soka lakini baada ya siku 4 tu Rotimi alirudi Togo na kusema maisha ya Dubai hayafanani na yeye. Alisema anataka sehemu yenye uhuru ambapo atakunywa kila sehemu,ajiachie kwenye party au ku-kiss wasichana waziwazi.
Party 3 itakuja hivi karibuni kuhusu kaka yangu ambae anajiita baba wa familia Kola Adebayor al maarufu kama Simba wa Yuda.