SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 18, 2015

KIKOSI BORA VPL KILICHOTAJWA NA KOCHA JOSEPH KANAKAMFUMU


DSC_9372
Salum Telela ni miongoni mwa wachezaji waliongia kwenye kikosi bora cha Kanakamfumu
BAADA ya kuona vikosi bora vya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 uliomalizika mei 9 mwaka huu kutoka kwa makocha Hans van der Pluijm (Yanga), Jamhuri Kiwhelo (Coastal Union), Juma Mwambusi (Mbeya City) na Mecky Mexime (Mtibwa Sugar), jana tuliahidi kuleta kikosi bora cha kocha Joseph Kanakamfumu na hiki ndicho kikosi chake bora alichopendekeza:
  1. Ally Mustafa (Yanga)
  2. Juma Abdul (Yanga)
  3. Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba)
  4. Salim Mbonde (Mtibwa Sugar)
  5. Kelvin Yondani (Yanga)
  6. Michael Balou (Azam fc)
  7. Said Ndemla (Simba)
  8. Salum Telela (Yanga)
  9. Simon Msuva (Yanga)
  10. Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
  11. Deus Kaseke (Mbeya City)
Kanakamfumu amesema katika kikosi chake hajawaweka wachezaji kwa kigeni kwasababu utafiti wake uliangalia zaidi wachezaji wazawa, lakini kwa upande wa kocha bora  msimu wa 2014/2015 amemtaja kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm.
Kesho tutakuletea kikosi bora cha kocha wa Mgambo JKT, Bakari Shime…endelea kutufuatilia

RASMI;SIMBA YAMWAGANA NA GORAN KOPUNOVIC


_MGM6121
Goran Kopunovic
UONGOZI wa Simba umethibitisha rasmi kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wake, Mserbia Goran Kopunovic baada ya kushindwa kufikia makubaliano juu ya mkataba mpya.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema Kopunovic ameshuka kidogo mno kwenye dau alilotaka na Simba wameshindwa kufikia uwezo huo.
“Amebaki palepale, ameshuka kidogo sana, tumeona atafute maslahi ya namna hiyo kwenye timu nyingine, sisi hatuwezi kufikia. Unaweza kusema hakushuka kabisa, yaani katika hela zote alizotaja ameshuka kwa dola elfu tano tu”. Amesema Hans Poppe na kuongeza: “Tumeshaona makocha karibu sita kutoka Serbia, Hungary, Bulgaria na Burundi pia tunaangalia, kuna kocha ambaye CV zake ni nzuri”.
Goran Kopunovic 
Hans Poppe ameongeza: “Hatudaiani na Kopunovic, mkataba wake umekwisha. Mrithi wa Goran ndani ya wiki moja tutakuwa tumempata. Atakakuja kocha tu, wasaidizi wataendelea walewale, hatukupenda kubadilisha, lakini bahati mbaya tumeshindwa kuafikiana, amekwenda juu mno tofauti na matarajio yetu, tungependa kuendelea na Kopunovic, ni kocha mzuri, ameifundisha timu vizuri”.
Kopunovic alitaka mshahara mkubwa wa dola za Kimarekani elfu tisa (9,000) sawa na shiloingi milioni 18 za Kitanzania.
Pia anataka dau la kusaini la dola za kimarekani elfu hamsini (50,000) sawa na shilingi million 100 za Kitanzania.
Taarifa zilizoripotiwa jana ni kwamba kocha Mbelgiji, Piet de Mol atatua Dar es Salaam Mei 21, mwaka huu kwa ajili ya mazungumzo ya kuifundisha Simba SC.
Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, De Mol mwenye umri wa miaka 60 ana uzoefu mkubwa wa kufundisha soka Afrika, Asia na Ulaya na alikuwa nchini Ghana akifanya kazi ya Mkurugenzi wa Ufundi wa akademi mjini Kumasi. Pia alifanya kazi na Asante Kotoko. Pia alifundisha timu ya kwao Ubelgiji, Dubai, Qatar na China. Alikuwa kocha Msaidizi wa AA Gent kuanzia mwaka 1997 hadi 2001.
Naye kopunovic leo akiwa Hungary amethibitisha kushindwana na Simba, lakini amedai kuwa atakuwa shabiki mkubwa wa timu hiyo kwani hakupenda kuondoka.
Simba imekosa kushiriki michuano ya kimataifa kwa miaka mitatu, kwa mara ya mwisho ni mwaka 2012 walipotwaa ubingwa wa Tanzania.
Moja ya sababu kubwa Simba kuchemsha katika michuano ya ligi kuu ni mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha.
Toka walipochukua ubingwa 2011/2012 chini ya kocha Maserbia Milovan Circovic, Simba imepitia mikononi mwa Mfaransa Patrick Liewig, Mzawa Abdallah Kibadeni, Mcroatia, Zdravko Logarusic, Mzambia Patrick Phiri na sasa wameachana na Mserbia, Goran Kopunovic.

BARCELONA MABINGWA WAPYA LA LIGA

1431888676589_lc_galleryImage_MADRID_SPAIN_MAY_17_Lione Messi akishangilia goli la ubingwa LIONEL Messi amewapa Barcelona ubingwa wa La Liga msimu wa 2014/2015  baada ya kuifungia bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Atletico Madrid  kwenye uwanja wa Vicent Calderon. Messi amefunga goli hilo katika dakika ya 65′ akimalizia pasi ya Pedro Rodriguez. Kwa matokeo hayo Barcelona wamefikisha pointi 93 baada ya kushuka dimbani mara 37 na wamebakiza mechi moja. Real Madrid wameshinda magoli 4-1 dhidi ya Espanyol na kufikisha pointi 89 katika mechi 37 walizocheza. Kwa maana hiyo wakishinda mechi ya mwisho watafikisha pointi 92 ambazo tayari zimeshavukwa na Barcelona . Inawezekana msimu ukawa mkubwa kwa Barcelona, leo wameshatwaa taji la ligi kuu, La Liga na watacheza fainali mbili, ligi ya mabingwa ulaya na kombe la mfalme ‘Copa del Rey’. Licha ya kuugulia maumivu ya kutolewa nusu fainali ya Uefa na Juvuntes katikati ya wiki hii na leo kukosa ubingwa wa La Liga, mshambuliaji hatari wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunga magoli matatu peke yake ‘hat-trick’ katika ushindi wa Madrid.  Ronaldo amefunga magoli hayo katika dakika ya 59′, 83′ na 90′. Goli lingine limefungwa na Marcelo dakika ya 79′ wakati goli la kufutia machozi kwa Espanyol limefungwa na Cristian Stuani dakika ya 73”.