=
Lakini
ajabu Messi, ameshindwa kuonyesha nakala ya mkataba wake ambayo ingeweza
kuonyesha kama kweli Simba wamekosea au la.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amemvulia uvivu meneja wa
kiungo wao, Ramadhani Singano ‘Messi’ kwamba analazimika kuwa makini.
Hans
Poppe amesema meneja huyo anapaswa kuwa makini kutokana na maneno aliyoyatoa
kwamba mkataba wa mchezaji wake ‘umechezewa’.
“Kwa
kweli anapaswa kuwa makini sana, maneno anayoyazungumza hayana ukweli na
anapaswa awe na uhakika.
“Anaposema
kuna ujanja umefanyika katika mkataba huo wakati uko TFF, maana yake TFF
wanahusika kuufanyia ujanja.
“Tumegushi
saini, tumegushi na dole gumba. Sidhani kama ni jambo zuri kuzungumza tu hayo
mambo.
“Anapaswa
kuwa makini, nasema hivi kumuasa lakini bado naweza kusema simtambui kwa kuwa
sijui yeye Messi ana meneja na wala hajawahi kuutambulisha uongozi wa Simba,”
alisema Hans Poppe.
Meneja
huyo amekuwa akilalama kwamba mkataba wa Simba na Messi unapaswa kulazimika
msimu huu lakini ulio TFF unaonyesha unamalizika mwakani yaani 2016.