SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Jun 2, 2015

AZAM FC YAWARUHUSU SIMBA KUMCHUKUA BEKI HUYU

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
AZAM FC imewataka Simba SC kuwasilisha maombi ya kumchukua beki David Mwantika (pichani kushoto) kama kweli kweli wanamuhitaji.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, Mwantika ana Mkataba na klabu hiyo hadi mwishoni mwa mwaka.
“Tunasikia sikia tu kwenye vyombo vya Habari kwamba Simba wanamtaka Mwantika, sisi hatuna tatizo, Simba SC wao waje tuzungumze,” amesema.
Mwantika alisajiliwa na Azam FC miaka miwili iliyopita kutoka Prisons ya Mbeya kwa Mkataba wa kudumu- kwamba atakapoacha mpira, atahamia kufanya kazi kwenye kampuni ya Bakhresa Group Limited, wamiliki wa klabu hiyo.
Maana yake- Simba SC nao kama wanataka kumchukua beki huyo mwenye miraba minne, wawe tayari kumhakikishia ajira nyingine baada ya soka.
Mwantika mwenyewe alipoulizwa kuhusu hilo alisema; “Ni kweli mimi ni mchezaji halali wa Azam, kama Simba wananitaka kweli, wakazungumze na Azam FC, sioni tatizo,”amesema.

BERBATOV 'AFUNGASHIWA VIFURUSHI' VYAKE AS MONACO

MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Bulgaria, Dimitar Berbatov anatafuta timu ya tatu ya kujiunga nayo England, baada ya kutemwa na AS Monaco ya Ufaransa.
Berbatov alijiunga na vigogo hao wa Ligue 1 Januari mwaka 2014 kutoka Fulham ya England na atakumbukwa kwa kufunga bao la pili katika ushindi wa 3-1 kwenye dhidi ya Arsenal kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Pamoja na hayo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 sasa yuko huru baada ya kuachwa na Monaco, iliyomaliza katkka nafasi ya tatu kwenye Ligue 1 msimu huu.
Ligue 1 giants AS Monaco have confirmed they have released Bulgarian striker Dimitar Berbatov
Vigogo wa Ligue 1, AS Monaco wamethibitisha kumtema Dimitar Berbatov

Katika taarifa kwenye tovuti ya klabu hiyo, Makamu wa Rais wa Monaco, Vadim Vasilyev, amesema; "Dimitar Berbatov ameonyesha kipaji chake chote na soka babu kubwa. Dhahiri ni miongoni mwa washambuliaji wakubwa waliojiunga na AS Monaco. Tunajivunia alicholeta katika klabu na tunamtakia kila la heri aendako,".'
Berbatov alikuwa na wakati mzuri akichezea klabu ya Tottenham Hotspur kabla ya kujiunga na Manchester United  iliyomsaini kwa dau la Pauni Milioni 30.75 mwaka 2008.
Amefunga mabao 48 katika Ligi Kuu ya England katika misimu minne chini ya kocha Sir Alex Ferguson, kabla ya kuhamia Fulham, ambako alicheza kwa msimu mmoja na nusu.
He scored 48 Premier League goals in four seasons for Manchester United after arriving in 2008
Before his move to the Red Devils, he enjoyed a successful spell with Tottenham
Mkongwe wa umri wa miaka 34 aling'ara Ligi Kuu England kabla ya kuhamia Ufaransa ambako nako ameacha kumbukumbu nzuri

HANS POPPE: SIMBA SC HATUSAJILI ‘BENDERA FUATA UPEPO’

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe (pichani juu) amesema kwamba ‘hawasajili bendera fuata upepo’, bali wanasajili kulingana na mahitaji ya timu yao.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Poppe amesema kwamba watu wanapenda kuona Simba SC inasajili wachezaji wanaovuma, lakini huo si mpango wa uongozi wa klabu.
“Sisi tuna kikosi kizuri ambacho kilimaliza msimu uliopita vizuri. Sasa tunachofanya ni kukiongezea nguvu kikosi kwa mujibu wa tathmini ya kitaalamu. Tunasajili mchezaji ambaye tunamuhitaji, siye anayevuma,”amesema.
Aidha, Poppe ambaye na Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema kwamba mkakati mzima na mpango wa usajili uko vizuri.
“Kila kitu kiko vizuri, tunafanya mambo yetu kimya kimya, hatushindani na mtu kusajili, tutakuja kushindana mpira uwanjani, hao wanaosajili wanaovuma, acha waendelee, sisi tunasajili kwa mujibu wa mahitaji yetu,”amesema.
Hadi sasa, tayari Simba SC imesajili wachezaji watano wapya, ambao ni kipa Abraham Mohammed kutoka JKU ya Zanzibar, mabeki Samih Haji Nuhu kutoka Azam FC, Mohammed Fakhi kutoka JKT Ruvu na kiungo Peter Mwalyanzi kutoka Mbeya City.    
Wapinzani wao wa jadi, Yanga SC wamesajili wachezaji wanne tu ambao ni kipa Benedicto Tinocco kutoka Kagera Sugar, beki Mwinyi Hajji Mngwali kutoka KMKM na washambuliaji Malimi Busungu wa JKT Mgambo na Deus Kaseke wa Mbeya City.

MBEYA CITY YASAJILI 'STRAIKA'


Na Mwandishi Wetu, MBEYA
MSHAMBULIAJI wa kutumainiwa wa Ndanda FC ya Mtwara, Gideon Brown (pichani juu) amesaini Mkataba wa mwaka mmoja na nusu kujiunga na Mbeya City FC ya Mbeya.
Brown amechagua kujiunga na kikosi cha Juma Mwambusi katika msimu ujao huku akiweka kando ofa kadhaa, alizopata kutoka klabu mbalimbali za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara alizopata hapo kabla.
Akizungumza mara baada ya kusaini Mkataba huo mapema jana kwenye ofisi za MCC FC zilizopo jengo la Mkapa Hall mjini Mbeya, Brown alisema kuwa limekuwa jambo zuri kwake kujiunga na timu ambayo inaweza kumpa mafanikio nje na klabu zingine zilizozoeleka.
“Watu wengi wengi wanaamini kuwa huwezi kufanikiwa bila kupita kule, binafsi nahisi ni tofauti kwa sababu kipaji kinaweza kuonekana popote,imani yangu nitafanikiwa hapa, City ni timu nzuri na ina mipango ya  ya kweli, nataka kufanya kazi kwa kiwango kikubwa na imani yangu sitawaangusha wale wote wenye mapenzi na timu hii, najaua nitakuwa chini ya mwalimu Mwambusi, huyu ni kocha ambaye siku zote nimekuwa na kiu ya kufanya nae kazi, hili limetimia sasa” alisema  mshambuliaji huyo.
Msimu uliopita Brown alikuwa moja ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Ndanda Fc akicheza michezo  21 akiwa kwenye kikosi cha kwanza, na kuifungia timu hiyo ya Mtwara jumla ya mabao 5, awali mshambuliaji  huyu amewahi kukupiga kwenye timu za KMKM ya  Zanzibar na kuisaidia kutwaa taji la ligi kuu ya visiwani humo pia amecheza kwenye kikosi cha Rhino ya Tabora na Moro United.