SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 21, 2016

BAADA YA MECHI ZA JANA HUU NDIO MSIMAMO VPL

Na Haji Balou
Baada ya Simba kufungwa na Yanga goli 2-0 na Azam fc kuifunga Mbeya City goli 3-0 huu ndio msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Wakati Simba ikiwa imemzidi Azam michezo miwili Yanga nae amemzidi Azam mchezo mmoja lakini Yanga nao wamezidiwa mchezo mmoja na Simba ac.

HII NDIO SABABU YA AZAM KUVAA JEZI MBILI TOFAUTI KATIKA MCHEZO WA JANA

Na Haji Balou
Timu ya Azam fc Jana imeibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya wenyeji wao Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.

Sehem kubwa ya mchezo huo ilitawaliwa na mvua hususa ni kipindi cha kwanza kulikuwa na mvua kubwa ambayo ilisababisha Azam fc kubadili jezi katika kipindi cha pili baada ya jezi za dark blue walizo vaa kipindi cha kwanza kuloa sana na kipindi cha pili walirudi wamevaa jezi nyeupe.

Feb 20, 2016

ALICHOSEMA TAMBWE BAADA YA YANGA KUPATA USHINDI DHIDI YA SIMBA

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe ambaye amefunga bao la pili katika mechi ya leo ambapo Yanga imeilaza Simba kwa mabao 2-0. Beki Abdi Banda alilambwa kadi ya njano ya pili katika dakika ya 25 na kuzaa nyekundu baada ya kumwangusha Donald Ngoma.

Tambwe alifunga bao katika dakika ya 72 baada ya beki Juuko Murshid kushindwa kumdhibiti baada ya krosi safi ya Geofrey Mwashiuya.
“Tulianza vizuri, mechi ilikuwa na
ushindani mkubwa. Lakini baada ya ile kadi nyekundu, ilitusaidia sisi kuingia kwa wingi katikati na kuwabana Simba.

Mechi ilikuwa nina ushindani sana, Simba walijitahidi kucheza vizuri licha ya kuwa pungufu. Lakini sisi tulikuwa bora zaidi leo,” alisema Tambwe raia wa Burundi.
Hilo ni bao la 15 msimu huu, huku akiwa amebakiza bao moja tu kumkamata Amissi Kiiza ambaye ana mabao 16.

AZAM YAIONESHA ADABU MBEYA CITY KWAO

Mchezo kati ya Mbeya City na Azam fc umemalizika na wenyeji wamekubali kichapo cha goli 3-0 kutoka kwa Azam fc magoli ya Azam yalifungwa na Kipre Tchetche dakika 41, John Bocco dakika ya 63 na Faridi Mussa dakika ya 84.

MAPUMZIKO KATIKA UWANJA WA SOKOINE MBEYA NA HAYA NDIO MATOKEO

Dakika 45 za kipindi cha kwanza katika uwanja wa sokoine mjini Mbeya  zimemalizika na timu ya Azam inaongoza goli moja dhidi ya Mbeya city goli lililofungwa na Kipre tchetche Dakika ya 41.

Feb 18, 2016

MAN UNITED YAPIGWA UGENINI

Man United imetandikwa mabao 2-1 katika mechi ya Kombe la Europa Cup dhidi ya FC Midtjylland ya nchini
Denmark. Pamoja na kwamba ilikuwa ugenini, Man United ilikuwa ikipewa nafasi ya kushinda dhidi ya timu hiyo ndogo. Lakini imefungwa mabao hayo 2-1 pamoja na mshambuliaji wake Memphis Depay kufunga bao moja.

Feb 7, 2016

KOCHA JULIO AMETOA SABABU INAYOFANYA CHUJI AKAE BENCHI MWADUI

Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ hamtumii Athuman Idd ‘Chuji’ katika kikosi chake, ishu ikiwa ni moja tu, kwamba kiungo huyo anatakiwa ajitume ili apate nafasi ‘first eleven’.

Tangu Desemba mwaka jana, Chuji
amekosa mechi za Mwadui na kuzua
maswali mengi miongoni mwa wadau wa soka lakini Julio amesisitiza: “Siridhishwi na kiwango chake.” Chuji sambamba na nyota wengine kutoka Simba na Yanga wakiwemo Jerry Tegete, Nizar Khalfan na Joram Mgeveke, walisajiliwa na Mwadui msimu huu ili
kuiongezea nguvu timu hiyo katika Ligi Kuu Bara.

Julio amesema mchezaji anayepata nafasi ya kucheza katika kikosi chake ni yule anayeonyesha uwezo na si vinginevyo, hivyo ni sawa na Chuji ambaye hamtumii kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake.

“Kwa nini aulizwe Chuji tu wakati nina wachezaji wengi? Inawezekana siwezi kumchezesha kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake, mpira unahitaji mazoezi, kama haupo vizuri utakaa nje.

“Hakuna nafasi kwa mchezaji asiyekuwa na kiwango, akiwa vizuri atacheza kama wachezaji wengine wanavyocheza, ukiona mtu yupo nje, ujue amezidiwa kiwango na wachezaji wengine,” alisema Julio.

Feb 6, 2016

STORY 3 KUBWA KUTOKA MAGAZETI YA ULAYA

3. Leta Pogba katika Real
Madrid
Meneja mpya wa Real Madrid Zinedine Zidane amemhimiza rais wa klabu Florentino Perez kutumia kitita kikubwa cha pesa kumleta kiungo wa Juventus Paul Pogba katika Santiago Bernabeu. (Source: AS)

2. Sturridge anataka
kuiondoka Liverpool
Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge yaripotiwa kwamba aliiambia klabu kwamba anataka kuondoka katika kiangazi kijacho baada ya kukabiliana na ukusoaji kutoka pande zote za dunia kuhusu shida za majeruhi.
Arsenal na Manchester United waripotiwa kwamba wanafuatilia karibu hali ya Mwingereza huyu na uhamisho wa mshambuliaji huyu
waweza kuwatokea katika kiangazi kijacho.
(Source: Daily Mail)

1. Chelsea yapuuza
£57.5m kumuuza Oscar
Chelsea yaripotiwa kwamba imepuuza pauni milioni 57.5 kutoka klabu ya China Jiangsu Suning kwa huduma za kiungo wa Brazilia Oscar.
Klabu hiyo iliyomsajili Ramires kutoka Blues hivi punde na walikuwa hata wakiwasiliana na kiungo wa Manchester City Yaya Toure. (Source: The
Sun)

HII NDIO RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO NA KESHO

Ligi Kuu ya Vodacoma Tanzania bara raundi ya 18 inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa
michezo nane kuchezwa katika viwanjabmbalimbali nchini, Jumamosi ukichezwa mchezo
Mmoja na Jumapili kuchezwa kwa michezo saba.

Jumamosi ligi ya kuu ya Vodacom itaendelea kwa mchezo mmoja tu, ambapo katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, African Sports watawakaribisha Stand United kutoka mkoani Shinyanga.

Michezo saba itachezwa siku ya Jumapili ambapo maafande wa JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Young Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mbeya City dhidi ya
Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, na Ndanda FC watawakaribisha Mtibwa
Sugar katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Kagera Sugar watacheza dhidi ya Simba SC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga,
Azam FC watawakaribisha Mwadui FC uwanja wa Chamazi, Majimaji dhidi ya Mgambo uwanja
wa Majimaji mjini Songea na Toto Africans watawakaribisha Coastal Union uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Hii hapa ratiba kamili ya VPL weekend hii.

Feb 2, 2016

CHANONGO UBWA MAMBO SAFI TP MAZEMBE

Na Haji Balou

KLABU ya TP Mazembe ya DRC
imeingia katika mazungumzo ya
kuwanunua wachezaji wawili wa
Stand United, beki Abuu Ubwa na
kiungo Haroun Chanongo baada ya
kufanya vizuri katika majaribio yao
mapema Januari.

Wawili hao walisafiri hadi
Lubumbashi, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
mapema Januari kwa majaribio ya
wiki moja na taarifa za awali
zikasema, wamefuzu.
Meneja wa wachezaji hao, Jamal
Kisongo amesema tayari Mazembe
imetuma barua rasmi ya majibu ya
majaribio ya vijana hao na kwamba
sasa wanaingia katika mazungumzo
na klabu yake.
“Jana nimepokea taarifa rasmi kutoka Mazembe kwamba (Chanongo na Ubwa) wamefuzu. Tunatarajia watasaini Mkataba wakati wowote baada ya kukamilika kwa mazungumzo na klabu yao,”amesema Kisongo akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo.

Kisongo ambaye pia ni Meneja wa
mshambuliaji wa KRC Genk ya
Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta
amesema kwamba mazungumzo
rasmi yatafanyika baada ya Rais wa
Mazembe, Moise Katumbi kurejea
Lubumbashi kutoka Ulaya.