SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Apr 19, 2016

TFF YAMZURUMU MAGOLI KIUNGO WA MBEYA CITY

Na Haji balou
KIUNGO chipukizi wa Mbeya City FC,
Rafael Daudi Alpha  amesema anashangaa hatajwi katikaorodha ya wafunga wa mabao mengi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wakati hadi sasa ana mabao sita.
Amesema anashangaa wakati wote
orodha ya wafungaji wa mabao mengi wa

Apr 18, 2016

HII NDIO REKODI MPYA YA LIONEL MESSI

Na Haji balou
Superstar wa Argentina Lionel Messi usiku wa jana amefikisha magoli 500 katika maisha yake ya soka aliyoifungia klabu yake na timu yake ya taifa baada ya kufunga bao moja wakati Barca ikilala 2-1 nyumbani mbele ya Valencia.
Nyota huyo mwenye miaka 28 alimaliza ukame wa

Apr 17, 2016

SIMBA CHALI KESSY AONESHWA NYEKUNDU

Na Haji balou
Leo April 17 uwanja wa Taifa
Dar es Salaam Simba wamekubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Toto Africans na kuendeleza rekodi yao ya kusumbuliwa na Toto kila mara
wanapokutana.
Simba kabla ya

MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA

Baada ya Jana Yanga kuibuka Na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa sugar huu ndio msimamo wa ligi kuu ya Vpl.

PLUIJIM ATOA LAWAMA KWA WAANDISHI WA HABARI

 
Na Haji balou
Kocha mkuu wa Yanga amelalamika juu ya waandishi ambao wamekuwa wakiandika vitu ambavyo yeye hajazungumza kwasababu
vinamletea matatizo na waajiri wake.
Hans amesema hivyo baada ya gazeti moja kutoa habari ambayo inasababisha mazingira magumu, anasema yeye ni mwajiriwa hivyo
anatarati zake za kazi na badala yake amewaomba waandishi kuchukua na kufanyia kazi kile ambacho anakuwa amekizungumza
mwenyewe.
“Mimi huwa zizungumzi kuhusu kuhusu makocha, timu nyingine wala TFF, kuna gazeti linasema mimi nilienda TFF kujaribu kubadilisha
tarehe za baadhi ya mechi lakini kulikuwa hakuna uwezekano juu ya hilo kwahiyo nikawa nimekasirishwa na TFF na kuanza kuwashutumu
kwamba hawajui kufanya mambo yao, sijawahi kuzungumza kuhusu federation watu wanatakiwa
kujua hilo”, amesema Hans ambaye anaonekana kuchukizwa na habari hiyo.
Kuhusu mchezo wao wa kiporo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao Yanga walishinda kwa bao 1-0 na kukwea hadi kileleni mwa ligi, Hans
amekimwagia sifa kikosi chake kuwa kimecheza vizuri kwenye mchezo huo licha ya kupoteza nafasi nyingi za kufunga magoli.
“Tulicheza vizuri sana kitu kimoja
kilichotuangusha ni kutotumia nafasi
tulizozipata, na wakati mechi inaelekea kumalizika kulikuwa na ‘tension’ kubwa kwa wachezaji wangu na hiyo ilisababishwa na kuwa na goli moja tu mkononi lakini kama unamagoli zaidi ya mawili unakuwa huna presha”.
“Tumecheza dhidi ya timu ngumu na tulilijua hilo kabla ndiyo maana mwanzoni tulianza na mfumo wa 3-5-2 lakini kwasababu tupo nyumbani na ni lazima tushinde mechi ndiyomaana tukamtoa beki mmoja nje na kuongeza mshambuliaji mwingine”.

SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1UGENINI

Na Haji balou
NYOTA ya Nahodha wa Tanzania,
Mbwana Samatta imeendelea
kung’ara Ulaya baada ya leo kuifungia tena klabu yake, KRC Genk katika ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya
Ubelgiji uliofanyika Uwanja wa
Regenboogstadion mjini Waregem,
Samatta alifunga bao la kwanza
dakika ya saba tu kwa kichwa
akimalizia kona ya mkongwe wa umri wa miaka 25, Mbelgiji Thomas Buffel.

Beki wa Kongo mzaliwa wa Ufaransa, Marvin Baudry akajifunga katika harakati za kuokoa dakika ya 15 kuipatia Genk bao la pili, kabla ya
mshambuliaji Msenegali, M'Baye Leye kuifungia SV Zulte-Waregem bao la kufutia machozi kwa penalti dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza.

Hilo linakuwa bao la nne kwa Samatta katika mechi tisa alizocheza tangu ajiunge na Genk Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DRC.

Apr 12, 2016

HII NDIO DROO YA NUSU FAINAL KOMBE LA FA

Na Haji balou
YANGA SC itamenyana na Coastal
Union katika Nusu Fainali ya
michuano ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), maarufu kama
Kombe la Azam Sports Federations
Cup 2016.

Mchezo huo utafanyika Uwanja wa
Mkwakwani mjini Tanga Aprili 24,
mwaka huu, siku ambayo Azam FC
itamenyana na Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Tanga Aprili 24,
mwaka huu pia.

Hiyo inafuatia droo iliyopangwa leo
studio za Azam TV, wadhamini wa
michuano hiyo, Tabata, Dar es
Salaam na kuhudhuriwa na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa.

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya
taifa ya wanawake, Twiga Stars,
Esther Chabruma ndiye aliyechagua
timu za kumenyana katika Nusu
Fainali katika droo hiyo, akisimamiwa na Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto.

Coastal Union iliingia Nusu Fainali
baada ya kuitoa Simba SC kwa
kuifunga mabao 2-1, wakati Azam FC iliitoa Prisons kwa kuifunga 3-1,
Mwadui FC iliitoa Geita Gold kwa
kufunga 3-0 na Yanga SC iliwafunga
Ndanda FC 2-1.

Bingwa wa Kombe la ASFC, michuano iliyoanza na timu 64 Novemba mwaka jana, ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

Katika hatua ya awali, kila timu
ilipatiwa fedha za usafiri Sh Milioni 3,
na vifaa vya mashindano kutoka kwa
wadhamini, Azam TV ikiwa ni sehemu ya udhamini wa Bilioni 3.3.

Bingwa wa Kombe la ASFC
atajinyakuliwa kitita cha Sh. Milioni
50, Fainali inatarajiwa kuchezwa wiki
moja baada ya Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara kumalizika.

Mara ya mwisho michuano hiyo
ilifanyika mwaka 2002 na JKT Ruvu
ikaifunga Baker Rangers ya
Magomeni katika fainali, wakati
ikijulikana kama Kombe la FAT
(Chama cha Soka Tanzania).

AZAM YAMZUIA FARID NA HIMID MAO KWENDA ULAYA SABABU IPO HAPA

Na Haji balou
UONGOZI wa Azam FC umezuia safari ya kiungo wake Farid Mussa  kwenda Ubelgiji kwa majaribio
ya kucheza soka ya kulipwa hadi
amalize mchezo wa marudiano wa
hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia Aprili 19.

Awali, makubaliano kati ya wakala wa Farid na Azam ilikuwa ni mchezaji huyo aondoke baada ya mchezo wa kwanza na Esperance uliofanyika Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Farid alifunga bao moja na kuseti
moja katika ushindi wa 2-1 na baada
ya hapo, benchi la Ufundi chini ya
kocha Muingereza, Stewart Hall
limeona linamuhitaji kinda huyo kwa
mchezo wa marudiano.

Mbali na Farid, kiungo Himid Mao pia
anatarajiwa kwenda Denmark kwenda kujaribu bahati yake.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad
Kawemba, amesema kwamba
wameiomba klabu inayomtaka Farid
kwa majaribio imsubiri kwa wiki moja
zaidi.

“Awali Farid Mussa alitakiwa
kuondoka mara moja kwa ajili ya
majaribio hayo, lakini tumewaomba
wenzetu wanaomtaka wamuache hadi amalizie mechi yetu ya pili dhidi ya Esperance na wamekubali, hivyo Farid ataondoka baada ya mechi hiyo,” alisema.

HUYU NDIYE MWAMUZI ATAKAYE CHEZESHA MECHI YA ATLET VS BARCA REKODI YAKE INAIBEBA ATLETI

Na Haji balou
Mwamuzi wa mechi kali ya Jumatano yenye
ushindani mkubwa sana Ligi ya Mabingwa Uefa, ameteuliwa, ni yule aliyechezesha fainali Kombe la Dunia 2014 Mwamuzi wa Kiitaliano Nicola Rizzoli amepangwa na UEFA kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa baina ya Atlético Madrid na Barcelona katika uwanja wa Vicente Calderón timu hizo zikiwa zinawania kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

Hii itakuwa mechi ya saba kwa Rizzoli kuchezesha Ligi ya Mabingwa katika toleo la 2015/16.
Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 44 anatambulika kwa ubora wake katika kazi yake, si bora tu, ni zaidi ya bora katika ulimwengu wa soka la leo.

Akiwa na uzoefu wa miaka 14 katika Serie A na FIFA tangu 2007, Rizzoli amejizolea sifa kubwa kwa kutenda haki na uwezo wa kuchezesha mechi kubwa.

Kwa mfano, Muitaliano huyo ndiye
aliyepuliza kipyenga fainali ya Kombe la Dunia 2014 Ujerumani dhidi ya Argentina.

Barca na Atlético zina historia ya mechi zilizochezeshwa na Rizzoli. Alikuwa mwamuzi Atletico iliposhinda 2-0 hatua ya makundi dhidi ya Olympiakos dimbani Calderón, hali kadhalia
Atletico iliposhinda 1-0 dhidi ya Bayer Leverkusen msimu uliopita raundi ya 16.

Apr 11, 2016

FARID KUWAKOSA ESPERANCE MECHI YA MARUDIO ANAENDA ULAYA KUTAFUTA ULAJI

Na Haji balou
KLABU ya Azam FC itamkosa kiungo
Farid Mussa Malik (pichani kushoto)
katika wa mchezo wa marudiano
hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance nchini  Tunis wiki ijayo.

Baada ya kufunga bao la kusawazisha katika ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi,   Farid sasa anajiandaa kwa safari ya majaribio Ulaya.

Bado wakala wa Farid hajaweka wazi basi anampeleka wapi kijana huyo, lakini inaelezwa atampeleka au
Ubelgiji, Scotland au Hispania ambako kote kuna timu za kumjaribu.

MANARA APATA AJALI

Na Haji balou
Mkuu wa Kitengo cha Habari na
Mawasiliano cha Simba, Haji Manara
amepata ajali mbaya.

Manara amepata ajali baada ya
kuchomoka tokea ndani ya Bajaj na
kuanguka barabarani.
Kuanguka huko kumesababisha Manara kupata majeraha sehemu za mkononi na usoni hukua kisema amenusurika kifo kutokana na ajali hiyo.

Manara ameelezea tukio hilo:
“Nilikuwa nakwenda kumuona shangazi yangu, nikaamua kuacha gari nichukue Bajaj. Sasa tukio hilo limetokea hivi; Bajaj ilipiga tuta wakati nikiwa sijashika, ndiyo nikachomoka.

“Hakika nimeumia na nina maumivu
makubwa sana, lakini namshukuru Mungu kwa kuwa ilikuwa ni ajali mbaya sana hasa kama kungekuwa na gari nyuma.”

HARAKATI ZA SOKA  INATOA POLE KWA MANARA NA KUMUOMBEA APATE NAFUU MAPEMA NA KUPONA KABISA.

Apr 10, 2016

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOOL AKIUA 4-1

Na Haji balou
Mshambuliaji Divock Origi akikimbia
kushangilia baada ya kuifungia
Liverpool bao la tatu katika ushindi
wa 4-1 dhidi ya Stoke City kwenye
mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni
ya leo Uwanja wa Anfield. Origi
alifunga mabao mawili, wakati
mengine yamefungwa na Alberto
Moreno na Daniel Sturridge na la
Stoke limefungwa na Bojan Krkic

VARDY APIGA MBILI LEICSTER YAZADI KUKAA KILELENI

Na Haji balou
Leicester imeitungua Sunderland kwa mabao 2-0, yote mawili yakiwa
yamefungwa na mshambuliaji wake hatari Jamie Vardy.

Vardy amefikisha mabao 21 akiwa
anakimbilia ufungaji bora, huku Leicester iliyobakiza mechi tano tu za Ligi Kuu England ikiwa imeanza kusikia harufu ya ubingwa.

Ushindi huo unaifanya ifikishe pointi 72, nafasi ya pili Tottenham wakiwa na pointi 62 na Arsenal katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 59.

BARCA YAPIGWA YAWEKA UBINGWA REHANI

Mikel Oiarzabal aliifungia Sociedad bao pekee dakika ya 5 kipindi cha kwanza lililowapa pointi tatu huku Barca ikishindwa kusawazisha goli hilo hadi dakika 90 zinamalizika.

Kichapo hicho kimewafanya Barca kusogelewa na Atletico Madrid kwenye mbio za ubingwa ambapo sasa Barcelona inaididi Atletico kwa pointi tatu, Barcelona ambao ndiyo vinara wa ligi wanapointi 76 wakifuatiwa na Atletico yenye pointi 73 huku Madrid ikiwa nyuma yao na pointi zake 72 wakati huo timu zote zikiwa zimecheza mechi 32 na kusaliwa na mechi sita pekee ili msimu kumalizika.

Apr 7, 2016

PIGO JIPYA AZAM FC

Na Haji balou
HABARI mbaya Azam FC, tena katika wakati mbaya. Beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Shomary Kapombe (pichani kulia) hatacheza mechi zote mbili za Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya Esperance ya Tunisia.

Kapombe aliyekosa mechi mbili
mfululizo za Ligi Kuu timu hiyo ikitoa
sare zote, 1-1 na Toto mjini Mwanza
Jumapili na 2-2 na Ndanda leo, Na
beki huyo wa zamani wa AC Cannes
ya Ufaransa anatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Afrika Kusini kwa matibabu.

Daktari wa Azam FC, Juma Kwimbe
amethibitisha leo kwamba Kapombe
hatacheza mechi zote dhidi ya
Esperance Jumapili Dar es Salaam na wiki mbili zijazo Tunis kwa sababu ni mgonjwa.

“Amekuwa akilalamika kuumwa
mbavu kiasi cha kulia wakati
mwingine, leo ikabidi afanyiwe vipimo na imegundulika anasumbuliwa na Nimonia, hivyo kesho anakwenda Afrika Kusini kwa
matibabu,”amesema.

Kukosekana kwa Kapombe katika
kikosi cha Azam FC wakati huu
ambao timu ipo kwenye vita ya
kuwania ubingwa wa Ligi Kuu na
Kombe la Shirikisho ni pigo.

Mbali na kuwa mhimili imara wa safu ya ulinzi, Kapombe pia amekuwa mpishi na mfungaji mzuri wa mabao  ya timu msimu huu, hadi sasa akiwa amefunga mabao saba kwenye Ligi Kuu pekee.

Apr 5, 2016

GOTZE KUHAMIA LIVERPOOL

Na Haji balou
Timu ya Liverpool ipo mbioni kuinasa saini ya kiungo wa Bayern Munich Mario Gotze Na hii ni kwamujibu wa
Mwanahabari wa kicker Jorg Jakob.

Gotze mwenye umri wa miaka 23  amejitahidi kupata namba
mara kwa mara katika  kikosi cha kwanza chini ya Pep Guardiola katika
timu yake ya Bayern Munich.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani  amekuwa akihusishwa na kuondoka Allianz Arena na inasemeka anaweza kujiunga na  bosi wake wa zamani Jurgen Klopp
Kwenye klabu ya Liverpool.

MATOLA APONDA MAAMUZI YA TFF

Na Haji balou
Kocha wa timu ya Geita Gold Mine, Seleman Matola, ameponda maamuzi ya Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka Tanzania TFF,
kwa kutoa maamuzi ya kukurupuka ya kuishusha daraja timu hiyo bila kuzingatia haki.

Matola ameiambia Goal, maamuzi hayo yamemsikitisha sana na haamini kama Kamati hiyo ya TFF, imewatendea haki wakazi wa Geita kwani haki hakuna baya lolote walilotenda na walipanda kwa kutumia uwezo wao ndani ya uwanja na siyo hongo.

“Hukumu haiko sahihi, naweza kusema kamati imekurupuka kwa sababu huwezi kuihukumu Geita pasipo kuwa na vithibitisho
vinavyoonekana machoni mwa watu
amesema Matola. Matola amesema anaamini viongozi wake watapambana kwa kukata rufaa ili kutafuta haki yao ambayo inapotea bila ya sababu zozote za msingi na ameiomba TFF kukutana na Kamati yake ili kuweza kulijadili upya
swala hilo kwasababu wametumia garama kubwa ili kuifikisha timu hiyo hapo.

Kamati hiyo ya nidhamu ilizishusha daraja klabu nne za Geita Gold Mine, Polisi Tabora, Geita JKT Kanebwa na JKT Oljoro pia baadhi ya viongozi na wachezaji watimu hizo walikumbana na kurungu la kufungiwa maisha
kujihusisha na mchezo wa soka huku wengine wakisimamishwa kwa miaka 10 na kutozwa faini ya Sh. 10 milioni.

Apr 4, 2016

JUMA KASEJA AWEKA HADHRANI MAPACHA WAKE


Watoto mapacha wa kipa mkongwe nchini, Juma Kaseja jana walifikisha siku 40 na rasmi kuanza kuonekana hadharani. Katika dua iliyosomwa nyumbani kwa Kaseja Mbezi kwa Msuguri jijini Dar es Salaam, wadau mbalimbali waliwaona "live" watoto hao kwa mara ya kwanza.

Mkewe Kaseja, Nasra Nassor maarufu kama "Naa" au  "Kikono" naye alionekana ni mwenye furaha kuu hiyo jana huku kukiwa na wageni wengi waliojitokeza kuwaunga mkono.
SALEHJEMBE INAWAPONGEZA KASEJA NA NASRA NA KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU AWAKUZIE MAPACHA HAO.



Malkia wa Kaseja