Kiungo kinda wa Simba, Said Ndemla,
anatarajia kwenda kufanya majaribio
kwenye kikosi cha TP Mazembe ya DR
Congo ili kusaka nafasi ya kucheza soka
katika klabu hiyo.
Hivi karibuni, Watanzania, Abuu Ubwa na
Haruna Chanongo walienda kufanya
majaribio Mazembe ambapo kwa sasa
hatua iliyobaki ni makubaliano kati yao na
Stand United inayowamiliki wachezaji hao.
Jamali Kisongo ambaye ni meneja wa
Mbwana Samatta, amesema kuwa,
ataendelea kuwasaidia wachezaji wa
Tanzania kupenya kwenye soka la
kimataifa kama Samatta.
“Nimewapeleka Ubwa na Chanongo
kufanya majaribio TP Mazembe,
kinachoendelea sasa ni mazungumzo kati
ya Stand na Mazembe kwa ajili ya usajili.
“Ndemla naye nitampeleka akafanye
majaribio kule, lengo ni kuwasaidia
wachezaji wengi wa hapa nyumbani
kupata fursa ya kucheza soka nje ya
mipaka ya nchi yetu.
“Mbali na Ndemla, pia kiungo wa Mtibwa
(Sugar), Mohammed Ibrahim, naye
anahitajika kule baada ya awali safari
yake kushindikana,” alisema Kisongo.