SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Jan 27, 2016

TETESI KUHUSU KOCHA MPYA MAN UNITED NA CHELSEA


Taarifa kutoka Manchester United zimedai kwamba uongozi wa klabu hautakata tamaa kufuatilia saini na na huduma za meneja Pep
Guardiola anayemaliza muda wake katika Bayern Munich, ingawa habari zilitependekeza kwamba atajiunga na mahasimu Manchester City.

Mtendaji Makamu Mwenyekiti Ed-Wood Ward anataka kumuajiri meneja wa Barcelona wa
zamani na atafanya hivyo kwa nguvu hadi dakika ya mwisho.

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Uongozi wa Chelsea umemtangaza meneja wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino katika
orodha ya mameneja wanaoweza kumrithi meneja wa mpito Guus Hiddink mwishoni mwa
msimu. Diego Simeone, Didier Deschamps na Jorge Sampaoli wako pia katika orodha hiyo ya
ushindani. (Source: The Times)

KIPRE AIOKOA AZAM DAKIKA ZA JIONI DHIDI YA ZESCO

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC imeanza kwa sare katika harakati zake za kuwania ubingwa wa michuano maalumu nchini Zambia baada ya jioni ya leo kupata matokeo ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wao Zesco United ya huko.

Kocha wa Azam FC, Stewart Hall, aliingia kwenye mchezo huo kwa kukifanyia marekebisho matano
kikosi chake kwa kuwajumuisha mabeki David Mwantika, Pascal Wawa, Wazir Salum, kiungo
Frank Domayo na mshambuliaji Kipre Tchetche, ambao hawakucheza mchezo uliopita wa Kombe la FA dhidi ya African Lyon.
Mchezo huo uliathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua inayoendelea kunyesha jijini Ndola, Zambia,
baada ya Uwanja wa Levy Mwanawasa kusimamisha maji jambo ambalovlilifanya soka la
pasi kutotumiwa sana na timu hizo kufuatia mpira kunasa kwenye maji kila unapoburuzika.

Walikuwa ni Zesco United walioweza kuziona nyavu za Azam FC katika dakika ya kwanza tu ya mchezo huo, bao lililofungwa na mshambuliaji
mpya wa timu hiyo, Jesse Were, aliyeibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Kenya msimu uliopita akiwa na Tusker FC akifunga mabao 22.

Azam FC iliamka baada ya kufungwa bao hilo na kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa
Zesco United, lakini hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Wazambia hao waliondoka kifua mbele kwa bao hilo.
Kipindi cha pili kilianza kwa Azam FC kufanya mabadiliko akiingia kiungo Michael Bolou kuchukua nafasi ya Nahodha Msaidizi Himid Mao
'Ninja'. Mabadiliko hayo yaliweza kuisaidia sana Azam
FC baada ya kutawala kwa kiasi kikubwa eneo la
kiungo na kuanza kulishambulia kwa kasi lango la wapinzani wao.

Dakika 67 Azam FC ilipata pigo baada ya kuumia kwa nahodha wake John Bocco 'Adebayor' na
nafasi yake ilichukuliwa na Allan Wanga huku pia akitoka beki Wazir Salum na kuingia Ramadhan
Singano 'Messi'.

Kuingia kwa wawili hao kukizidi kuongeza kasi kwenye eneo la ushambuliaji la Azam FC na
katika dakika ya 70 beki Shomari Kapombe aliyeachiwa kitambaa cha unahodha na Bocco, almanusura aipatie bao la kusawazisha timu hiyo
baada ya kupiga shuti kali umbali ya mita 30 lililogonga mwamba wa juu na kutoka nje ya lango la Zesco United.

Azam FC ilizidi kuweka kambi katika lango la wapinzani wao dakika 15 za mwisho na hatimaye
ikajipatia bao safi la kusawazisha dakika ya 90 lililofungwa na Kipre Tchetche kwa kichwa
akimalizia kona safi iliyochongwa na Messi upande wa kulia.

Kona hiyo iliyozaa bao ilikuwa ni ya tatu kupigwa na Messi ndani ya dakika hiyo baada ya
wachezaji wa Zesco United kuokoa mara mbili za
mwanzo alizopiga kabla ya tatu haijazaa bao.
Hadi dakika 90 za mchezo huo wa kwanza
zinamalizika timu hizo zilitoka uwanjani zikiwa
nguvu sawa kwa mabao hayo.
Hiyo ni sare ya pili mfululizo baina ya timu hizo kwani katika michuano ya mwaka jana iliyofanyika jijini Lubumbashi DR Congo na
wenyeji TP Mazembe kuibuka mabingwa, zilitoka
sare ya mabao 2-2.

Azam FC itateremka tena dimbani Jumamosi Ijayo kucheza na mabingwa wa Zimbabwe
Chicken Inn kabla ya kumaliza michuano hiyo kwa kukipiga na Zanaco FC ya huko Jumatano
ijayo.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa hivi
Aishi Manula, Shomari Kapombe, Wazir Salum/
Ramadhan Singano 'Messi' dk67, Erasto Nyoni,
David Mwantika, Pascal Wawa, Jean Mugiraneza
'Migi', Himid Mao 'Ninja'/Michael Bolou dk46,
Frank Domayo 'Chumvi', John Bocco 'Adebayor'/
Allan Wanga dk67, Kipre Tchetche

ALICHOSEMA SUAREZ KUHUSU YEYE KUCHEZA TENA ENGLAND

Mshambuliaji hatari wa Barcelona, Luis Suarez amezungumzia uwezekano wa yeye kurudi
nchini England na kuichezea klabu yake ya zamani ya Liverpool, huku akisema kuwa ndio klabu pekee anayoweza kurudi England kwa ajili
yake.

Suarez ambaye aliichezea Liverpool kwa kipindi cha miaka 2 na nusu kabla ya kusajiliwa na
Barcelona ya nchini Hispania ameiambia ESPN kuwa kila mchezaji ambaye alipata kuichezea Liverpool anajua umuhimu wa mashabiki wa
Liverpool Anfield.

Suarez anasema kuwa mashabiki wa Liverpool ni wa pekee zaidi duniani, na kwamba anawakumbuka kila wakati kitu kinachomfanya
awe na ndoto za siku moja kurudi tena Merseyside kufurahia tena maisha na mashabiki hao.

Mchezaji huyo wa zamani wa Ajax alijiunga Liverpool mwaka 2011 kwa ada ya uamisho wa pauni 22m na katika kipindi cha miaka 2 na nusu
aliifungia Liverpool magoli 94 kabla ya kusajiliwa na Barcelona kwa dau kubwa la pauni 75m.

HUYU NDIYE MCHEZAJI ANAYEMZIDI MESSI KWA MAGOLI

Mashabiki wengi wa kilabu ya Athletic Bilbao wangecheka iwapo ungetaja miaka ya nyuma
kwamba Aritz Aduriz angelinganishwa na Lionel
Mesii,Cristiano Ronaldo na Luiz Suarez.

Mchezaji huyo anayekaribia miaka 35 ameingia katika kumbukumbu za daftari lenye wachezaji
wenye mabao mengi pamoja na
Messi,Suarez,Karim Benzema na Neymar msimu huu.
Wale wasiofutilia ligi ya Uhispania huenda wasimtambue Aritz Aduritz ni nani.Aduriz
alifunga mabao mawili katika mechi ya ushindi dhidi ya Eibar na kufikisha mabao yake kuwa 25 katika michuano yote msimu huu.

Nyota wa Real Madrid,Ronaldo ni mchezaji pekee anayesakata soka yake nchini Uhispania
aliyewahi kufunga mabao zaidi,ijapokuwa Messi,Suarez,Benzema na Neymar wana mabao
mengi ukilinganisha na mechi walizocheza dhidi ya Aduriz.

Lakini sio mabao mengi ya Aduriz yaliowavutia wengi,kasi yake ya kuweza kufunga mabao ya
'bicycle kick' dhidi ya Eibar imempa uwezo wa kupigania nafasi ya bao zuri msimu huu na kuweka jina lake katika midomo ya wapenzi
wengi wa ligi ya Uhispania.

Ungana na mchezaji wa Atletico Bilbao Aduriz
ambaye amefunga mabao mengi zaidi ya Messi.
Aduriz, ambaye atafikisha miaka 35 mnamo tarahe 11 mwezi Februari,amefunga mabao 25
katika michuano yote ya Athletico Bilbao msimu huu.

Mchezaji mwenye mabao mengi nchini Uhispania.Bao katika kila mechi.Cristiano Ronaldo 27 27 1.00Aritz Aduriz 25 34 0.74Luis
Suarez 24 28 0.86Karim Benzema 21 20 1.05Neymar 20 24 0.83Lionel Messi 19 23 0.83 Lakini ni vipi Aduriz ameweza kuingia katika
orodha ya wafungaji bora katika ligi ya Uhispania?

Kupitia uvumilivu na ubarakala .
Alirudi katika kilabu ya Atletico Bilbao kwa mara
ya 3 mwaka 2012,baada ya kufeli kuvutia
alipokuwa kijana,ambapo alihudumu misimu
miwili na nusu akichezea Burgos na Real
Valladolid kabla ya kurudi mwaka 2005 na 2008
ambapo alizuiliwa na uwepo wa Fernando
Llorentes.
Athletico ilimchezesha sana Llorentes kuwa
mshambuliaji wa pekee hatua iliomaanisha
kwamba Aduriz alipatiwa nafasi chache,na
baadaye akaelekea Mallorca na Valencia ili
kutafuta fursa hiyo.