Ligi Kuu Bara imekuwa na ushindani mkubwa, mastraika wakisaka kiatu cha dhahabu makocha wakitafuta ushind VPL, Makipa nao hawapo nyuma, Je! kipa bora msimu huu
nani? Kipa wa Azam FC, Aishi Manula, ametajwa kuwa ndiye kipa bora katika Ligi Kuu Bara msimu huu mpaka sasa akiwapiku makipa Deogratius Munishi ‘Dida’ wa Yanga na JumabKaseja wa Mbeya City.
Goal kinatambua mchango wa Aishi Manula katika kikosi chake cha Azam FC, hali kadhalika amekuwa akionyesha jitihada katika
timu ya Taifa ya Tanzania lakini bado
hajafanikiwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Charles Mkwasa.
Kwa mujibu wa aliyekuwa kocha wa zamani wa makipa wa Simba, Mkenya, Iddi Salim, kwa kipindi cha miezi sita alichokaa Tanzania
kufundisha soka, amemuona Manula kuwa ndiye bora huku akisisitiza kama ataendelea kulelewa kwenye misingi bora, bila shaka atakuja kuwa msaada mkubwa kwa timu ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Akizungumza na waandishi wa habari Iddi Salim alisema “Kwa miezi sita niliyokaa Tanzania, naweza kusema nimewaona makipa wengi katika Ligi Kuu Bara, lakini kipa
wa Azam, Manula, kwangu ndiye ni bora zaidi kuliko mwingine kutokana na mambo anayoyafanya uwanjani ikiwemo kucheza penalti nyingi.
“Lakini pia ukiangalia kwa makipa vijana, Manula anashika namba moja akifuatiwa na Manyika Jr., na kama watazidi kukomaa basi
watakuja kuwa makipa wazuri siku za usoni,”
alisema kocha huyo aliyewahi kuinoa Gor Mahia na timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars' .
Akizungumzia kipa mwingine bora, Idd alisema Peter Manyika wa Simba, kama atapata matunzo mazuri, mafunzo mazuri na
kuthaminiwa, ndiye atakuwa tegemeo la Tanzania hapo baadaye.