SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 6, 2016

STORY 3 KUBWA KUTOKA MAGAZETI YA ULAYA

3. Leta Pogba katika Real
Madrid
Meneja mpya wa Real Madrid Zinedine Zidane amemhimiza rais wa klabu Florentino Perez kutumia kitita kikubwa cha pesa kumleta kiungo wa Juventus Paul Pogba katika Santiago Bernabeu. (Source: AS)

2. Sturridge anataka
kuiondoka Liverpool
Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge yaripotiwa kwamba aliiambia klabu kwamba anataka kuondoka katika kiangazi kijacho baada ya kukabiliana na ukusoaji kutoka pande zote za dunia kuhusu shida za majeruhi.
Arsenal na Manchester United waripotiwa kwamba wanafuatilia karibu hali ya Mwingereza huyu na uhamisho wa mshambuliaji huyu
waweza kuwatokea katika kiangazi kijacho.
(Source: Daily Mail)

1. Chelsea yapuuza
£57.5m kumuuza Oscar
Chelsea yaripotiwa kwamba imepuuza pauni milioni 57.5 kutoka klabu ya China Jiangsu Suning kwa huduma za kiungo wa Brazilia Oscar.
Klabu hiyo iliyomsajili Ramires kutoka Blues hivi punde na walikuwa hata wakiwasiliana na kiungo wa Manchester City Yaya Toure. (Source: The
Sun)

HII NDIO RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO NA KESHO

Ligi Kuu ya Vodacoma Tanzania bara raundi ya 18 inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa
michezo nane kuchezwa katika viwanjabmbalimbali nchini, Jumamosi ukichezwa mchezo
Mmoja na Jumapili kuchezwa kwa michezo saba.

Jumamosi ligi ya kuu ya Vodacom itaendelea kwa mchezo mmoja tu, ambapo katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, African Sports watawakaribisha Stand United kutoka mkoani Shinyanga.

Michezo saba itachezwa siku ya Jumapili ambapo maafande wa JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Young Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mbeya City dhidi ya
Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, na Ndanda FC watawakaribisha Mtibwa
Sugar katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Kagera Sugar watacheza dhidi ya Simba SC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga,
Azam FC watawakaribisha Mwadui FC uwanja wa Chamazi, Majimaji dhidi ya Mgambo uwanja
wa Majimaji mjini Songea na Toto Africans watawakaribisha Coastal Union uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Hii hapa ratiba kamili ya VPL weekend hii.