SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 7, 2016

KOCHA JULIO AMETOA SABABU INAYOFANYA CHUJI AKAE BENCHI MWADUI

Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ hamtumii Athuman Idd ‘Chuji’ katika kikosi chake, ishu ikiwa ni moja tu, kwamba kiungo huyo anatakiwa ajitume ili apate nafasi ‘first eleven’.

Tangu Desemba mwaka jana, Chuji
amekosa mechi za Mwadui na kuzua
maswali mengi miongoni mwa wadau wa soka lakini Julio amesisitiza: “Siridhishwi na kiwango chake.” Chuji sambamba na nyota wengine kutoka Simba na Yanga wakiwemo Jerry Tegete, Nizar Khalfan na Joram Mgeveke, walisajiliwa na Mwadui msimu huu ili
kuiongezea nguvu timu hiyo katika Ligi Kuu Bara.

Julio amesema mchezaji anayepata nafasi ya kucheza katika kikosi chake ni yule anayeonyesha uwezo na si vinginevyo, hivyo ni sawa na Chuji ambaye hamtumii kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake.

“Kwa nini aulizwe Chuji tu wakati nina wachezaji wengi? Inawezekana siwezi kumchezesha kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake, mpira unahitaji mazoezi, kama haupo vizuri utakaa nje.

“Hakuna nafasi kwa mchezaji asiyekuwa na kiwango, akiwa vizuri atacheza kama wachezaji wengine wanavyocheza, ukiona mtu yupo nje, ujue amezidiwa kiwango na wachezaji wengine,” alisema Julio.