NA Haji balou
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa
Tanzania, Thomas Emmanuel
Ulimwengu (pichani) yuko fiti kabisa sasa na atakuja nchini
kuichezea nchi yake mechi mbili za
Kundi G kufuzu Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika mwakani.
Na klabu yake, Tout Puissant
Mazembe imemruhusu kuja Dar es
Salaam kuugana na Taifa Stars kwa
ajili ya michezo miwili ya nyumbani
na ugenini dhidi ya Chad.
TPM imemuambia Ulimwengu,
maarufu kama Rambo mbele ya
mashabiki wa Lubumbashi kwamba
atakwenda Dar es Salaam mara tu
baada ya mchezo wa marudiano wa
Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa
Afrika dhidi ya St George ya Ethiopia
Jumapili ya Machi 20 mjini Lubumbashi.
Taifa Stars watakuwa wageni wa
Chad Jumatano ya Machi 23 mjini
N'Djamena, kabla ya timu hizo
kurudiana Machi 28 mjini Dar es
Salaam.
Ulimwengu aliumia mguu akiichezea
Mazembe dhidi ya St Eloi Lupopo
Februari 17, mwaka huu katika Ligi
Kuu ya DRC timu hizo zikitoka sare
ya 0-0 na akacheza kwa dakika 12 za
mwisho huku akichechemea Februari 20 katika mchezo wa Super Cup ya CAF dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia mjini Lubumbashi, wenyeji
wakishinda 2-1.