Watoto
mapacha wa kipa mkongwe nchini, Juma Kaseja jana walifikisha siku 40 na
rasmi kuanza kuonekana hadharani. Katika dua iliyosomwa nyumbani kwa
Kaseja Mbezi kwa Msuguri jijini Dar es Salaam, wadau mbalimbali
waliwaona "live" watoto hao kwa mara ya kwanza.
Mkewe Kaseja,
Nasra Nassor maarufu kama "Naa" au "Kikono" naye alionekana ni mwenye
furaha kuu hiyo jana huku kukiwa na wageni wengi waliojitokeza kuwaunga
mkono. SALEHJEMBE INAWAPONGEZA KASEJA NA NASRA NA KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU AWAKUZIE MAPACHA HAO.