SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Apr 7, 2016

PIGO JIPYA AZAM FC

Na Haji balou
HABARI mbaya Azam FC, tena katika wakati mbaya. Beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Shomary Kapombe (pichani kulia) hatacheza mechi zote mbili za Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya Esperance ya Tunisia.

Kapombe aliyekosa mechi mbili
mfululizo za Ligi Kuu timu hiyo ikitoa
sare zote, 1-1 na Toto mjini Mwanza
Jumapili na 2-2 na Ndanda leo, Na
beki huyo wa zamani wa AC Cannes
ya Ufaransa anatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Afrika Kusini kwa matibabu.

Daktari wa Azam FC, Juma Kwimbe
amethibitisha leo kwamba Kapombe
hatacheza mechi zote dhidi ya
Esperance Jumapili Dar es Salaam na wiki mbili zijazo Tunis kwa sababu ni mgonjwa.

“Amekuwa akilalamika kuumwa
mbavu kiasi cha kulia wakati
mwingine, leo ikabidi afanyiwe vipimo na imegundulika anasumbuliwa na Nimonia, hivyo kesho anakwenda Afrika Kusini kwa
matibabu,”amesema.

Kukosekana kwa Kapombe katika
kikosi cha Azam FC wakati huu
ambao timu ipo kwenye vita ya
kuwania ubingwa wa Ligi Kuu na
Kombe la Shirikisho ni pigo.

Mbali na kuwa mhimili imara wa safu ya ulinzi, Kapombe pia amekuwa mpishi na mfungaji mzuri wa mabao  ya timu msimu huu, hadi sasa akiwa amefunga mabao saba kwenye Ligi Kuu pekee.