SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 10, 2016

SIDO FC YAGAWA DOZI KWA BLACK STAR

Na Haji balou
Leo may 10 ligi ya Mbuzi vijana  Cup  imeendelea tena kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwanja wa shule ya  msingi muungano mechi kati ya Sido fc dhidi ya Black star.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu ambayo ilifanikiwa kuona lango la mwenzake lakii kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Sido ndio walikuwa wa kwanza kupata  goli kupitia kwa Haikosi mpwate katika ya dakika ya 65 dakika tisa baadae Festo Ashapira alifunga goli la pili dakika ya 80 Adam chonde aliipatia Black stars goli la kufutia machozi lakini dakika ya 85 haikosi mpwate aliiandikia Sido fc  goli la tatu mpaka mchezo unamalizika Sido fc 3-1 dhidi ya Black stars.

Baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa sido fc Rajabu Mohammedi amesema pamoja na kupata ushindi mnono lakini wachezaji wake hawakucheza vizuri kutokana na kutofanya mazoezi ya kutosha.

Ligi hiyo itaendelea tena hapo kesho katika mchezo mmoja utakao ikutanisha Kombaini dhidi ya Kigamboni.