Na Haji balou
Timu ya Boda boda fc imeibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Black stars katika mchezo wa ligi ya Mbuzi ya Vijana Cup mchezo uliopigwa katika uwanja wa shule ya Msingi Muungano.
Magoli ya Boda boda fc yamefungwa dakika ya 27 kupitia kwa kiungo wake mshambuliaji Abuu pia goli la pili lilipatikana kupitia kwa mchezaji Kazumali katika dakika ya 40 na goli la mwisho lilifungwagwa na Mbaraka masoud katika dakika ya 85 na goli la kufutia machozi kwa upande wa Black stars lilifungwa na Ally Omari katika dakika ya 20 ya mchezo.
Ligi hiyo itaendelea tena hapo kesho kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwaja wa Shule ya Msingi Muungano.