SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 24, 2016

LIGI YA MBUZI VIJANA CUP YAMALIZIKA HATUA YA MAKUNDI KWA SIDO FC KUIBUKA NA USHINDI

Na Haji balou
Ligi ya Mbuzi Vijana cup imeendelea tena hii Leo kwa mchezo mmoja kupigwa katika  uwanja wa shule ya msingi muungano katika kuhitimisha hatua ya makundi kati ya Sido fc dhidi ya Vijuso fc mchezo ambao umemalizika kwa Sido kuibuka Na goli 1-0.

Goli pekee la Sido fc lilifungwa Na Haikosi mpwate katika dakika ya 65 ya mchezo huo ligi hiyo itaendelea tena tarehe 26 mwezi huu kwa mechi za robo fainali.

Timu zilizoingia hatua ya robo final katika kundi A  Kigamboni, Kombaini, Mnalani, na Likongowele.

Kundi B ni Sido, Bodaboda, Wakaanga sumu na Vijuso.

YANGA KUPAMBANA NA TP MAZEMBE KOMBE LA SHIRIKISHO

Na Haji balou
YANGA SC imepangwa kundi la A
katika Kombe la Shirikisho Afrika
pamoja na mabingw awa zamani
barani, TP Mazembe ya DRC, MO
Bejaia ya Algeria na Medeama ya
Ghana.

Kundi B linaundwa na timu za
Kaskazini mwa Afrika tupu ambazo ni Etoile du Sahel ya Tunisia ambao ni  mabingwa watetezi, Ahly Tripoli ya Libya, FUS Rabat na Kawkab zote za  Morocco.

Mechi za mzunguko wa kwanza
zitachezwa Juni 17, mwaka huu na
Ratiba hiyo inamaanisha Yanga
itakutana na timu ya mshambuliaji wa Tanzania, Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC.