Na Haji balou
MSHAMBULIAJI wa TP Mazembe ya
DRC, Thomas Emmanuel Ulimwengu
'Rambo' jana hakufanya mazoezi na
timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars
kwa sababu ya maumivu ya mguu.
Ulimwengu baada ya kuwasili na
wachezaji wenzake Uwanja wa Taifa,
alijaribu kufanya mazoezi ya awali ya
kuamsha misuli kidogo, kabla ya
kushindwa kuendelea na kutoka nje.
Madaktari wa Taifa Stars walijaribu
kuhangaika naye kumrejesha
uwanjani, lakini hakuweza kabisa
kurudi mazoezini.
Daktari Mkuu wa Taifa Stars, Gilbert
Kigadye akasema Ulimwengu aliumia
juzi Taifa Stars na jana ameshindwa
kabisa kufanya mazoezi kwa sasa wanaangalia namna ya ya punguza maumivu.