SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Jun 10, 2016

DALILI MPYA YA IBRAHIMOVIC KUHAMIA MAN UTD

Na Haji balou
Staa wa zsmani wa
klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa
Zlatan Ibrahimovich kuhusishwa kujiunga na
klabu ya Man United zimechukua sura mpya,
Zlatan anaripotiwa kukamilisha hatua ya nne ya
kujiunga na klabu ya Manchester United .

Dalili inayotajwa kuwa staa huyo yupo mbioni au
katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya
Man United zinazidi kudhihirika, baada ya
kuripotiwa tayari ametafutiwa nyumba ya kuishi
katika jiji la Manchester ambapo ndio makao
makuu au mji inapotoka klabu ya Man United.

Kwa mujibu wa nyaraka iliyopostiwa katika
websites ya Proto Group Ltd ambao ni mawakala
wa nyumba inaashiria kuwa mipango ya Zlatan
kutangazwa kujiunga na Man United ipo tayari
kutokana na mji alipotafutiwa nyumba ya kuishi,
kwani kabla ya hapo alikuwa akiishi Paris
Ufaransa .