SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Jun 20, 2016

YANGA YAANZA VIBAYA KOMBE LA SHIRIKISHO

Na Haji balou
YANGA SC imeanza vibaya mechi za
Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika,
baada ya kufungwa bao 1-0 wenyeji
Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja
wa Unite Maghrebine mjini Bejaia
usiku huu.

Goli pekee la MO Bejaia alikuwa ni beki
Yassine Salhi aliyefunga bao hilo
pekee dakika ya 20, akimalizia kazi
nzuri ya mshambuliaji Ismail
Belkacemi.

Matokeo hayo yanaifanya MO Bejaia
ishike nafasi ya pili katika kundi hilo,
nyuma ya TP Mazembe ambayo
iliifunga Medeama ya Ghana 3-1
katika mchezo wa kwanza mjiji
Lubumbashi Jumapili, wakati Yanga
inashika nafasi ya tatu.

Mechi zijazo za kundi hilo, Yanga
watakuwa wenyeji wa Mazembe Dar
es Salaam na Medeama
wataikaribisha Mo Bejaia.