Jun 22, 2016
WALICHOSEMA REAL MADRID KUHUSU ALVARO MORATA
YANGA WAMEFIKIA HAPA KUHUSU HASSAN KESSY KUCHEZA MICHUANO YA CAF
Na Haji Balou
YANGA wamewaandikia
barua Simba SC kuwajulisha
kumsajili beki Hassan
Ramadhan Kessy na kuuliza
kama kuna pingamizi lolote
kutoka kwao, na wakati huo
huo nakala zimepelekwa
Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) na Shirikisho la Soka
Afrika (CAF).
Yanga ilishindwa kumtumia
Kessy Jumapili katika
mchezo wake wa kwanza
wa Kundi A Kombe la
Shirikisho Afrika wakifungwa
1-0 na wenyeji MO Bejaia
nchini Algeria, baada ya
CAF kuomba barua ya
kuruhusiwa kwake kuondoka
klabu yake ya zamani,
Simba SC, ambayo
hawakuwa nayo.
Na mara baada ya mchezo
huo, Yanga imewaandika
barua mahasimu wao hao
wa jadi, ikiwa
imeambatanisha Mkataba
wa Kessy na Simba ambao
unaonyesha umemalizika
Juni 15, mwaka huu na
mchezaji huyo alikuwa
sahihi kuingia Mkataba
mpya na klabu nyingine.
Na Yanga imepanga iwapo
hadi kufika Jumatano Simba
haitakuwa na majibu yoyote
ya barua hiyo – wataomba
TFF iwasaidie
kumuidhinisha beki huyo wa
kulia kuanza kazi Jangwani,
maana yake klabu yake ya
zamani haitakuwa na
pingamizi naye.
Na iwapo Simba SC
watamuwekea pingamizi
Kessy, watapaswa kuwa na
hoja za pingamizi ambalo
litasikilizwa na Kamati ya
Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya TFF, chini ya
Mwenyekiti wake, Wakili
Richard Sinamtwa.
Na kulingana na uzito wa
suala hilo, inatarajiwa hadi
kufika Ijumaa Kessy
atakuwa amekwishapewa
baraka za kuanza kuitumikia
Yanga.
MAYANJA AREJEA DAR KUANZA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA
Na Haji Balou
KOCHA wa Simba, Mganda
Jackson Mayanja
anatarajiwa kuwasili Juni 25
au Juni 26 na siku moja
baadaye ataanza programu
ya mazoezi ya kujiandaa na
msimu mpya.
Hayo yamesemwa na
Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zacharia
Hans Poppe alipozungumza
na mwandishi wetu leo kuhusu mikakati
ya usajili na maandalizi ya
msimu mpya jana mjini Dar
es Salaam.
Kapteni huyo wa zamani wa
Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ), Popppe amesema
kwamba mara Mayanja
atakapowasili, wachezaji
wote wenye Mkataba na
Simba SC wakiwemo wapya
ambao wamesajiliwa hivi
karibuni wataanza mazoezi.
MZAMBIA WA YANGA APEWA JEZI YA COUTINHO
Na Haji balou
SIKU chache baada ya kusaini mkataba
wa miaka miwili ya kuichezea Yanga,
uongozi wa Yanga umemkabidhi jezi
namba saba mshambuliaji wake Mzambia,
Obrey Chirwa.
Chirwa alitua nchini wiki iliyopita akitokea
FC Platinum ya Zimbabwe aliyokuwa
anaichezea pamoja na mshambuliaji
tegemeo, Donald Ngoma.
Mzambia huyo, alisaini kuichezea Yanga
akichukua nafasi ya Mniger, Issoufou
Aboubacar aliyesitishiwa mkataba wake
wa kuendelea kukipiga Jangwani hivi
karibuni.
Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh
alisema jezi iliyobaki ni namba saba
iliyokuwa inavaliwa na Mbrazili, Andrey
Coutinho.