SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Jul 7, 2016

VALDEZ ASAINI TIMU HII HAPA ENGLAND

Na Haji balou
Kipa wa zamani wa Fc barcelona Na Manchester united Victor Valdez amesaini mkataba wa miaka miwili Na klabu ya Middlesbrough ya nchini England.

Valdez mwenye umri wa miaka 34 amekuwa Na wakati mgumu tangu atue Manchester united akitokea  Barcelona baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika klabu hiyo.

Kupitia account yake ya Twitter Valdez aliandika hivi  “Very Proud to be part of Middlesbrough.

“A new challenge for me from today!”.

MANYIKA JR AZUNGUMZIA SKENDO YA MAPENZI INAYOMKABILI

Na Haji balou
Mchezaji wa timu ya Simba Peter manyika Jr amesema yeye ni mmoja kati ya wachezaji wenye nidhamu isipokuwa mashabiki wengi wanamsema kutokana Na jinsi wanavyo mwona.

Manyika alisema hayo alipokuwa akihojiwa Na Sauda mwilima kupitia kipindi cha Mcheza kwao kinachorushwa na channeli ya Star Tv.

Pia alipoulizwa kuhusu skendo za mapenzi zinazo mkabili Manyika alisema kuwa "Siku zote ukiwa maarufu watu watazungumzia sana mahusiano yako kutokana Na aina ya mpenzi ambaye unatoka nae".

"Kiukweli Mimi nipo Na mpenzi wangu huyu huyu ambae ninae kwa miaka miwili sasa Ila kwakuwa watu wanaongea waache waongee" alisema Manyika Jr.

Mashabiki walianza kumtuhumu Manyika Jr anashuka kiwango baada ya kugundua anatoka kimapenzi na binti wa kiarabu ambaye anamfanya Manyika kushindwa kufanya mazoezi Mara kwa Mara.