NA Haji balou
SIMBA SC ina nafasi ya kurejea
kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara leo iwapo itashinda
dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.
Simba wanaikaribisha Ndanda leo
katika mfululizo wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam wakihitaji
ushindi ili kuongoza ligi.
Na kocha wa Wekundu hao wa
Msimbazi, Mganda Jackson Mayanja amesema kwamba timu yake ipo vizuri baada ya maandalizi ya tangu Jumatatu wakiwa kambini nje kidogo ya mji ili wachezaji wapate utulivu.