SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 11, 2015

GOR MAHIA MABINGWA WAPYA SUPER CUP

MABINGWA wa Kenya, Gor Mahia usiku huu wametwaa taji la DSTV Super Cup, mechi maalum ya kuashiria kupenuliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Kenya, baada ya kuifunga mabao 2-1 Sofapaka Uwanja wa Nyayo, Nairobi.
Kwa ushindi huo, Gor inayofundishwa na kocha Mscotland, Frank Nuttal imezawadiwa fedha za Kenya, Sh. Milioni 1, zaidi ya Sh. Milioni 14 za Tanzania, wakati mabingwa wa Ngao ya GOtv, Sofapaka wamepatiwa Sh 500,000 za Kenya.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Moses Osano, hadi mapumziko, tayari Gor- mabingwa mara nyingi zaidi Ligi Kuu Kenya, (14) tayari walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na Victor Ally Abondo.
Abondo alifunga bao hilo dakika ya 20 akiupitisha mpira juu ya kipa, David Okello kufuatia krosi ya Mganda, Khalid Aucho.
Mkuu wa SuperSport Afrika, Andre Venter akimkabidhi Kombe la DSTV Super Cup, nahodha wa Gor Mahia, Victor Ally Abondo kulia usiku huu Uwanja wa Nyayo


Sofapaka inayofundishwa na kocha Mganda, Sam Timbe, ilipambana kurudisha bao hilo kipindi cha kwanza bila na mafanikio.
Kipindi cha pili, nyota ya Gor Mahia iliendelea kung’ara baada ya kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 68, mfungaji Abondo tena kwa mkwaju wa penalti, baada ya Michael Olunga kuangushwa kwenye eneo la hatari na kipa Okello.
Zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo kumalizika, kiungo wa Gor Mahia, Mganda Innocent Wafula alimfunga kipa wake, Boniface Oluoch wakati akiondoa mpira kwenye himaya ya mshambuliaji wa Sofapaka, Enock Agwanda.
Kwa ujumla, Gor walistahili ushindi wa leo, kutokana na kucheza vizuri kuliko wapinzani wao.
Ligi Kuu ya Kenya inatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki, ingawa Gor na Sofapaka zote zitakuwa kwenye michuano ya Afrika.       
Hata hivyo, bado kiza kimetanda katika soka ya Kenya kufuatia mgogoro unaoendelea baina ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF) na Kampuni inayosimamia Ligi Kuu (KPL).
KPL chini ya Mwenyekiti wake, Ambrose Rachier ambaye pia ni Mwenyekiti wa Gor Mahia, imekwishaandaa Ligi Kuu, lakini FKF chini ya Rais wake, Sam Nyamweya imeikana Ligi hiyo- huku nayo ikiandaa ligi yake.
FKF wamesema Ligi Kuu yao itaanza wikiendi hii, wakati KPL wamesema Ligi Kuu halisi ya Kenya itaanza Februari 21, mwaka huu.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Gor Mahia kilikuwa;Boniface Olouch, Godfrey Walusimbi, Abouba Sibomana, Mussa Mohammed, Khalid Aucho, Victor Abondo/Timoth Otieno, Ernest Wendo, Ronald Otieno/Innocent Wafula na Glay Dirkir, Abdul Nzigiyimana na Michael Olunga.
Sofapaka; David Okello, Felly Mulumba, Collins Shivachi, Ekaliana Ndolo, Willis Ouma, Abdul Yorou, Maurice Odipo, Kevin Omondi/Shafiq Batambuze, Danson Kago/Elly Asieche, Enock Agwanda na Fiston Abdul Razack.  

MASHABIKI 160 WA YANGA WAKODI BOTI KUIFUATA TIMU YAO DAR


Mashabiki wa Yanga wapatao 160 wamekodi boti kuja jijini Dar kuongeza nguvu.



Yanga inashuka kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar kuivaa BDF XI ya Botswana katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho.

Wanachama na mashabiki hao wanasafiri kwenda jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuisaidia timu yao kwa kushangilia kwa nguvu.

Mmoja wa wanachama wa Yanga kutoka Zanzibar, Mohammed Hamis amesema wamekuwa wakichangishana kwa zaidi ya wiki moja sasa.

"Yanga ni timu ambayo inawakilisha taifa, tumeona tuwe na wawakilishi Dar es Salaam siku ya mechi.

"Tayari tumeanza kuandikisha majina kwa wale wanaotaka kwenda na michango imekuwa ikitolewa.

"Tunaamini idadi inaweza kuzidi hata hao watu mia sitini maana mwamko ni mkubwa sana," alisema.

WAPINZANI WA AZAM FC WAONYESHA JEURI YA FEDHA


Wapinzani wa Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, El Merreikh ya Sudan inatua kesho na moja kwa moja kwenda kufikia katika moja ya hoteli kubwa nchini ya nyota tano ya Serena.


Merreikh inatarajia kutua nchini saa 7 mchana tayati kwa mechi yao ya kwanza dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar.

Timu ni moja ya zile tajiri zaidi barani Afrika na ina uzoefu mkubwa wa michuano iliyo chini ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf).


Hata hivyo, Azam FC wameonyesha wako sawa na wanawasubiri kwa hamu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Mtibwa Sugar.

STAND UNITED YAILILIA SIMBA KUTOLIPA MSHAHARA WA CHANONGO


Uongozi wa Stand United umelalama kuwa Simba imekuwa hailipi kasi cha mshahara kwa mshambuliaji Haruna Chanongo.



Mkurugenzi wa Ufundi wa Stand United, Mhibu Kanu amesema makubaliano yao na Simba ni kila upande kulipa nusu mshahara lakini Simba wamekuwa hawafanyi hicho.

"Sisi tumekuwa tukitekeleza, lakini wenzetu mambo yamekuwa tofauti. Hawamlipi na hili tunaona wanapunguza utendaji wake maana wanamvunja nguvu.

"Tuko katika mazungumzo tujue inakuwaje lakini vizuri wangetekeleza mkataba," alisema Kanu.

Kwa upande wa Simba, Katibu Mkuu, Stephen Ally alisema wamekuwa wakimlipa Chanongo kupitia akaunti yake kama kawaida.

"Ni kweli tumekubaliana hivyo na Stand, kila upande umekuwa ukilipa nusu na sisi tunatimiza hilo kupitia akaunti yake.

"Huenda hajaenda kuangalia, namshauri angeenda kuangalia kabla ya kulalamika," alisema.

ALICHOKISEMA KOPUNOVIC KUHUSU DANNY SSERUNKUMA


IMG_0522
KOCHA mkuu wa Simba SC, Goran Kopunovic anafurahishwa na kiwango cha mshambuliaji wake, Raia wa Uganda, Danny Sserunkuma ambaye siku za karibuni amekuwa na makali ya kufumania nyavu.
Sserunkuma alifunga bao moja katika ushindi wa Simba wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda fc huko Nangwanda Sijaona na mabao mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa Taifa.
“Danny ni mtu anayevutia, nilikutananaye kwa mara ya kwanza huko Zanzibar, nadhani kwa kiasi fulani alikuwa na kiwango cha chini, lakini sasa anakuja. Amesema Kopunovic.
“ Unajua nafasi anayocheza Danny ndio nilikuwa nacheza katika maisha yangu ya soka na nawaelewa vizuri washambuliaji, wakati wote kitu muhimu ni magoli. Danny ni mtu wa kigeni, ni mchezaji wa kimataifa, anatoka timu ya taifa ya Uganda, ana uzoefu wa kucheza nje ya Uganda, alicheza Kenya katika klabu ya Gor Mahia,kwahiyo ni mchezaji muhimu katika timu” Ameongeza Kopunovic.
Mserbia huyo alipoulizwa kuhusu mwenendo wa klabu yake katika mechi za ligi kuu Tanzania bara na anajisikiaje kupata matokeo yasiyoridhisha, amejibu:  “Siku zote nasema ukweli, siku zote kocha Goran anaangalia mechi ijayo, mimi ni mpaganaji ninayetafuta mafanikio ya timu. Simba ni timu kubwa, inaungwa mkono sana, ina mashabiki wengi, nina furaha sana kwasababu mashabiki wako upande wangu, ni watu muhimu sana”. Amesema Kopunovic.
Kumekuwa na madai kuwa wachezaji wa Tanzania wanashindwa kuwaelewa makocha wa Kizungu, lakini Kopunovic amesema wachezaji wa Simba wanamuelewa vizuri.
“Nadhani ndiyo, mara zote naongea na wachezaji wangu kabla na baada ya mechi, maswali yote nayaelekeza kwa wachezaji kuhusu mazoezi, mfumo wangu, falsafa yangu na mapaka sasa hakuna mtu anayeniambia kuwa kocha tuna matatizo, hiki sio kitu kizuri kwetu, hiki ni kigumu, nadhani tunaenda vizuri”.
Simba imeshuka dimbani mara 13, imeshinda 3, imetoa sare 8 na  imefungwa mechi 2 na kutokana na matokeo hayo ipo nafasi ya 9 nyuma ya Kagera Sugar, Coastal Union, Mtibwa Sugar na Ruvu Shootings.
Mwishoni mwa wiki hii, Simba wataikabili Polisi Morogoro katika mechi ya ligi kuu itayopigwa uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

DANNY SSERUNKUMA AFUNGUA MDOMO

SSERUNKUMA-VS-NDANDA
BAADA ya kufuta ukame wa kufunga magoli katika mechi za ligi kuu, Mshambuliaji wa Simba, Danny Sserunkuma amesema limekuwa jambo jema kwake kufunga magoli matatu mpaka sasa.
Danny amesema kazi ya mshambuliaji ni kufunga magoli na inapokuwa kinyume lazima presha iwe kubwa.
“Siku zote ni vizuri kwa mshambuliaji unapoanza kufunga magoli na kuisaidia timu kupata ushindi, hata nilipokuwa sifungi nilikuwa na furaha kwasababu timu ilishinda kombe, lakini kwasasa nina furaha zaidi baada ya kuanza kufunga,  kwa mshambuliaji hili ni jambo nzuri.”Amesema Danny na kuongeza:  “Siku zote kuna presha, lakini kocha anatuambia tufurahie mchezo, tusiwazie presha,  siku zote presha ipo katika soka”.
Wakati huo huo, Emmanuel Okwi amesema anamfahamu vizuri Danny na amecheza naye timu ya taifa na hana wasiwasi na uwezo wake.
“Namjua Danny (Sserunkuma), ni mfungaji mzuri, Kenya alifunga sana, kilichomsumbua hapa Tanzania ni kukosa uzoefu na wachezaji wenzake, ona sasa amepata uzoefu na ameanza kufunga”.
Simba ina wachezaji watano wa Kigeni wote kutoka Uganda ambao ni Juko Mursheed, Joseph Owino, Danny Sserunkuma, Emmanuel Okwi na Danny Sserunkuma.

AZAM FC YAREJEA KILELENI, YAICHARAZA 5-2 MTIBWA SUGAR CHAMAZI

kikosi-azam-fc
Na Bertha Lumala, Dar es salaam
Azam FC, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara wamefanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 5-2 kwenye Uwanja wa Azam uliopo Chamazi, Mbande jijini hapa jioni hii.
Mabao mawili ya kiungo Frank Domayo na washambuliaji Kipre Tchetche na Didier Kavambagu, aliyefunga moja, yamewapa uongozi wa ligi hiyo Azam FC wakifikisha pointi 25 sawa na Yanga SC waliowafunga Mtibwa Sugar FC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini hapa Jumapili na kukaa kileleni kwa muda, lakini wanalambalamba wanabebwa na tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Mechi hiyo ya kipigo kikubwa kwa Mtibwa Sugar FC msimu huu na kipigo kikubwa zaidi cha ligi hiyo msimu huu, imeshuhudiwa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij aliyekuwa Jukwaa Kuu la Uwanja wa Azam.
Kagera Sugar FC, timu ndugu na Mtibwa Suga FC, ilifungwa mabao 4-0 dhidi ya Azam FC kwenye uwanja huo huo msimu uliopita, kikiwa ni kipigo kikubwa kwa tmabingwa hao wa Kombe la Tusker 2008 katika miongo miwili iliyopita.
Timu hiyo inayomilikiwa na familia ya tajiri mkubwa nchini, Said Salum Bakhresa (SSB), imefunga mabao 22 na kufungwa 12 wakati Yanga SC wamefunga mabao 15 na kuruhusu nyavu zao kutikishwa mara saba. Timu zote mbili zimecheza mechi 13.
Dakika ya 19 tu ya mchezo, mshambuliaji Tchetche, anayetoka kwa mabaingwa wa Afrika mwaka huu, Ivory Coast, alifunga mlango wa mabao kwa wenyeji Azam FC akiuwahi mpira uliogonga mwamba kutokana na shuti la winga mpya na hatari Brianm Majwega.
Hilo lilikuwa bao la pili kwa Tchetche katika mechi mbili baada ya kufunga pia bao la kwanza katika sare yao ya 2-2 dhidi ya Polisi Moro mjini Morogoro Jumamosi.
Kwa bao hilo, Tchetche, mfungaji bora wa ligi kuu ya Bara msimu wa 2012/13 na mchezaji bora wa ligi hiyo msimu uliopita, akafikisha mabao matano ligi kuu ya Bara msimu huu sawa na Ame Ally Amour wa Mtibwa Sugar FC na Danny Mrwanda wa Yanga SC.
Dakika nne kabla ya nusu saa ya mchezo, kiungo Domayo aliyerejea uwanjani Januari baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika Kusini mwaka jana, alipatia bao la pili Azam FC akimalizia pasi fupi ya winga ‘fundi’ Majwega iliyopenyezwa ndani ya boski.
Hilo ni bao la pili kwa Domayo baada ya kufunga pia bao pekee katika mechi yake ya kwanza ya ligi kuu akiwa na kikosi cha Mcameroon Jopseph Omog waliyoshinda 1-0 dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarge mjini Shinyanga Januari 17.
Domayo alikuwa na nafasi ya kufunga bao katika shambulizi kali la kwanza la Azam FC, lakini akapaisha. Ilikuwa mechi ya tatu ya ligi kuu kwa Domayo ndani ya kikosi cha Azam FC.
Katika dakika ya 34 Musa Nampaka alifumua shuti la kushtukiza na kuwapatia Mtibwa Sugar FC bao akiitendea haki pasi murua ya Mzanzibar Ally Shomari Sharrif. Hilo ni bao la kwanza kwa Nampaka msimu huu.
Kinara wa mabao Didier Kavumbagu alihakikisha anaendelea kuiwakimbia Samwel Kamuntu wa JKT Ruvu Stars na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar FC wenye mabao sita baada ya kuifungia Azam FC bao la tatu baada ya kupewa pasi safi na kiungo Salum Abobakar ‘Sure Boy’ dakika tano kabla ya mapumziko.
Kwa bao hilo, Mrundi huyo amefikisha mabao nane msimu huu ambayo ni sawa na mabao yote aliyoyafunga mfungaji bora wa ligi hiyo msimu uliopita, Mrundi mwenzake Amisi Tambwe katika raundi saba za awali msimu uliopita.
Tchetche amerejea tena kambani dakika ya nne kabla ya kipenga cha mwisho na kufikisha mabao sita ligi kuu msimu huu akiwakamata Mandawa, Ame na Kamuntu. Tchetche amemalizia krosi nzuri iliyomiminwa na beki wa pembeni Shomari Kapombe baada ya gonga gonga nyingi zilizofanywa na kikosi cha Azam kuanzia katikati ya uwanja.
Dakika mbili kabla ya saa ya mchezo, Domayo aliyejiunga na Azam FC muda mfupi baada ya kumalizika kwa msimu uliopita akitokea Yanga SC, alitupia bao la nne kwa timu yake, la pili kwake katika mechi ya leo na la tatu kwake msimu huu baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Mohamed kutokana na shambulizi kali la wanalambalamba.
Dakika 12 baada ya goli hilo, yaani katika dakika ya 70, Ame Ally Amour alifunga bao la pili kwa Mtibwa Sugar FC akimalizia kwa ufundi pasi maridhawa ya mtokeabenchini Abdallah Juma ambaye ulikuwa mpira wake wa kwanza tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Mussa Hassan ‘Mgosi’.

Vikosi vilikuwa;
Azam FC: Manula, Kapombe, Nyoni/ Bocco (dk.65), Moradi, Wawa, Bolou/ Mudathir Yahya (dk. 55), Tchetche, Domayo, Kavumbagu/ Mcha (dk.80), Sure Boy na Majwega.
Mtibwa Sugar SC: Said Mohamed, Andrew Vicent, Majaliwa Mbaga, Ally Lundenga/ Vicent Barnabas (dk. 46), Salim Mbonde, Shaban Nditi, Ramadhani Kichuya, Musa Nampaka, Ame Ally Amour, Henry Joseph/ Ally Shomari (dk.33) na Musa Hassan ‘Mgosi’/ Abdallah Juma (dk. 70).

KOCHA YANGA ATAJA MBINU ZA KUWAKALISHA WABOTSWANA

DSC_0863
*El-Merrikh kutua Dar kesho
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Wakati wapinzani wa Azam FC katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, El-Merrikh FC ya Sudan watatua jijini Dar es Salaam kesho, Yanga SC wameahidi kuichakaza kwa pasi nyingi timu ya BDF XI ya Botswana katika mechi yao ya hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Azam FC (CEO), Saad Kawemba, kikosi cha El-Merrikh, mabingwa mara 19 wa Ligi Kuu ya Sudan, kitatua jijini hapa kesho tayari kwa mechi yao ya kwanza ya hatua ya awali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi jijini hapa Jumapili.
MKWASA: TUTAICHAKAZA BDF
Kocha Msaidizi wa Yanga SC, CHarles Boniface Mkwasa amesema kikosi chao kitacheza soka la pasi nyingi lililopotea tangu kufukuzwa kwa Mbrazil Marcio Maximo, ili kukikarisha kikosi cha BDF XI ya Botswana katika mechi yao ya kwanza ya hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mechi hiyo itachezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa jijini hapa kuanzia saa 10:00 jioni.
Kuelekea mechi hiyo, Mkwasa amesema: “BDF XI ni timu ya jeshi, tunatambua kwamba itacheza soka la kutumia nguvu nyingi kama ilivyo kwa timu za majeshi za hapa nchini.”
“Tunatambua watacheza soka la namna hiyo, hivyo tumejipanga kuwadhibiti kwa kucheza pasi nyingi ili tuwafunike na kuwachosha maana watakuwa wakiutafuta mpira,” amesema zaidi kocha huyo wa zamani wa Twiga Stars na Ruivu Shooting, anayesifika kwa kufundisha soka la kasi na la pasi fupi fupi.
Tayari Yanga SC imeshatangaza viingilio vya mechi hiyo, kiingilio cha chini kiwa Sh. 5,000.

ALICHOSEMA BEKI SIMBA

ALIYEKUWA beki wa Simba SC David Naftali Tevelu ameahidi kuwakilisha taifa lake vyema katika ligi kuu ya taifa la Kenya akivalia jezi ya Ushuru FC pindi tu msimu wa 2015 utakapong’oa nanga mwishoni mwa mwezi Februari.

Katika mahojiano na BIN ZUBEIRY, Tevelu alithibitisha uhamisho wake kutoka Bandari FC ya Mkoa wa Pwani hadi Ushuru FC ya Mkoa wa Nairobi kwa mwaka mmoja.

“Nimejiunga na Ushuru FC kwa mkataba wa mwaka mmoja kutoka Bandari nilikokuwa kwa miaka minne sasa,” alisema.

“Naamini mazingira haya mapya yatanisaidia katika mchezo wangu. Kwa sasa natia bidii mazoezini ili niweze kuwafurahisha walimu maana hii ni timu mpya na mchezaji yeyote mgeni lazima atie bidii ndiposa kuonyesha uwezo wake uwanjani,”David Naftali (mbele) katika Ligi ya Kenya




“Nipo tayari kwa msimu huu, mwalimu wangu Ken Kenyatta akinipa nafasi bila shaka nitamfrahisha na timu iweze kusajili matokeo mazuri. Kwa watanzania wenzangu kule nyumbani, nipo hapa (Kenya), kwa ajili yao na katu sitoshusha hadhi ya taifa letu katika ligii kuu ya Kenya. Nitajituma kwa uwezo wangu niwafurahishe hata walimu wa Taifa Stars.”

Tevelu ni mchezaji pekee mwenye uraia wa Tanzania katika ligii kuu ya Kenya kwa sasa. Kabla ya kujiunga na Bandari mwaka 2011, beki huyo alikuwa akiwajibikia Wekundu wa Msimbazi alikokuwa tangu mwaka 2007.

Mzawa huyo wa Mbeya aliwahi pia kuichezea AFC Arusha mwaka 2006. Anakuwa mchezaji wa kumi na tano kujiunga na klabu hiyo inayofadhiliwa na Kampuni ya kutoza Ushuru, Kenya (KRA).

Ivo Phillip Mapunda (Bandari na Gor Mahia), Idris Rajab na Salim Kinje (AFC Leopards) ni baadhi ya Watanzania waliokuwa wakisaka pato lao Kenya vilabuni.







FABREGAS KAMILI KUICHEZEA CHELSEA LEO




Cesc Fabregas has returned to Chelsea training and will be in the squad for the visit of Everton on Wednesday night
Kiungo aliyekuwa majeruhi, Cesc Fabregas amerejea mazoezini jana Chelsea kujiandaa na mchezo wa ugenini Ligi Kuu ya England usiku wa leo dhidi ya Everton




The Spanish midfielder passes the ball at Cobham ahead of the Premier League clash at Stamford Bridge

REAL MADRID WAONYESHA JEURI YA FEDHA

ANGALIA JEURI WANAYOTAKA KUIFANYA REAL MADRID SANTIAGO BERNABEU





Real Madrid imetenga kitita cha pauni milioni 328 ili kuukarabati kwa kuutanua na kuufanya wa kisasa zaidi Uwanja wake wa Santiago Bernabéu.





Rais wa Madrid, Florentino Perez ameonyesha michoro ya uwanja huo itaoufanya kuwa uwanja bora zaidi duniani.



Project hiyo inatarajia kuwa ya miaka mitatu na itauongezea uwanja huo uwezo wa kuchukua watu kutoka 85,454 hadi 90,000.





Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kujifunga na kujifungua kwa juu.







Madrid ndiyo klabu namba moja kwa utajiri duniani.







HII YA SAKHO ILIKUWA KALI JANA






BEKI MAMADOU SAKHO WA LIVERPOOL, JANA ALITOA KALI WAKATI ALIPOMRUKIA KIUNGO MOUSSA DEMBELE WA SPURS KATIKA MECHI YA LIGI KUU ENGLAND.

SAKHO ALIRUKA KWA ULE MFUMO KAMA WA MCHEZO WA RUGBY IKIWA NI BAADA YA DEMBELE KUMTOA. ANGALIA MWENYEWE.













NI VITA YA UBINGWA LA LIGA LEO


pic_2015-01-11_BARCELONA-ATLETICO_46.v1421017727


Mtandao wa ESPN umeainisha namna ambavyo bosi Diego Simeone na klabu yake ya Atletico Madrid wanavyoweza kuipiku madrid kwa mara nyingine katika mbio za ubingwa wa ligi kuu ya hispania maarufu kama La Liga. Kwa mujibu wa mtandao huo kuna mambo matano ya kutafakari kufuatia kufungwa kwa Real Madrid sambamba na ushindi wa goli 5-2 wa Barcelona.



1.Madrid wamejipa shida



Akizungumza mara baada ya kumaizika kwa pambano la jumamosi walilofungwa 4-0 ugenini Vicente Calderon, kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti alikiri kwamba matokeo waliyopata walistahili huku akisema “lazima tuwe na utulivu na kutafakari kwanini tumepatwa na hali hii lazima tubadilike.”





Hii ilikuwa ni mwenendo mbovu zaidi kwa madrid ambao walikuwa wamefunga katika kila mchezo wa La Liga msimu huu waliambulia kulenga lango mara moja tu katika dakika zote 90 tena kupitia mchezaji aliyeingia kipindi cha pili Asier Illarramendi.



Hali hiyo ni kitu ambacho hakikutarajiwa na kwa timu kama madrid yenye nyota wa safu ya ushabuliaji wa gharama kubwa. Ikumbukwe mpaka kufikia kipindi cha Christimas miamba hiyo ilikuwa imeshinda michezo 22 katika michuano mbalimbali huku ikiwa na wastani wa kufunga goli 3.25 kwa mchezo uwezo ambao umeshuka mpaka 1.88.



Hata wastani wa magoli wa Nyota wao mahiri Cristiano Ronaldo umeshuka toka 1.5 mpaka 0.57 amekiri kuwa suala lao loa kufungwa linahusisha mwili na akili. “Timu haipo sawa si kimwili si kiakili” alisema Ronaldo.



Naodha huyo wa Ureno alibainisha kuwa wamesikitika kuwaumiza washabiki wa klabu hiyo pamoja na jopo la wataalamu wa klabu hiyo na hata wachezaji wenzao hasa ikizingatiwa ushirikiwao katika hafla ya nyota huyo kutimiza miaka 30 ilomalizika jumamosi alfajiri. Ni kama vile pambano hilo la wapinzani halikupewa uzito unaostahili na hivyo ni wazi bosi wa klabu hiyo (Ancelotti) atahitaji kufanya kazi kuwarejesha mchezoni.



2.Kukaribiana na klabu ya Barcelona ni hatari

Mara ya mwisho Real madrid walipopoteza katika la La liga mapema mwezi Januari mwaka huu, wapinzani wao Barcelona walishindwa kunufaika na hali hiyo baada ya kukubali kichapo toka kwa Real Sociedad, ni wakati ambao hali haikuwa shwari klabuni barcelona huku minong’ono kadha wa kadha ikitawala.



Hata hivyo tangu hapo wapinzani wao wameikmarika na hata jumapili katika pambano dhidi ya Athletic Bilbao ni wazi walikuwa katika ubora wao huku wakiwaacha wapinzani wao wakihangaika bila mafanikio.



Na hata mchezaji wao mahiri Lionel Messi alikuwa yule wa ubora wa hali ya juu katika klabu ya Barcelona. Katika pambano hlo muargentina huyo alihusika katika mabao yote matano, akifunga moja na kupika mengine ikiwemo moja ya pasi bora za mwisho msimu huu alipotengeneza bao la Pedro Rodriquez.



Barca walitikiswa kunako dakika tano za mwanzo lakini hata hivyo walipambana na kuonesha umahiri wao katika pambano hilo wakashind 5-2 huku kiwango walichokionesha kikiwa miongoni mwa viwango bora kabisa msimu huu. Ukitizama walivyocheza ni wazi matatizo baina ya Luis Enrique na vijana wake yametulia kiasi maana Barca wameshinda michezo tisa mfululizo katika michuano mbalimbali huku wakifunga goli 32 na kuruhusu goli 7 pekee. Ni wazi ndo wana nafasi kubwa zaidi ya kutwaa taji hilo kwa sasa



3.Atletico pia wanaweza kucheza



Moja ya kibwagizo ambacho kimekua kikifuatia ushindi wa Atletico Madrid ni namna vijan ahao wa Diego Simeone wanavyotumia nguvu, mabavu na hata uteegemezi wa mipira iliyokufa kujipatia ushindi na hivyo hata kama watashinda si timu kubwa utakuwa umebadilika.



katika mchezo wa jumamosi walionesha kiwango cha hali ya juu hususani katika kipindi cha pili wakiongozwa na umahiri wa washambuliaji Arda Turan na Antoine Griezman huku kila goli likitokana na gonga za hapa na pale.



hata baada ya pambano kocha Simeone alisema kuwa kuwa aliamua kuchagua kikosi hicho cha wachezeshaji ambacho hususani wale ambao wangeweza kupasiana kwa haraka. “tuliitaji kuchezea mpira na katika hilo tulifanikiwa”



4.Real Sociedad “bado wamo”



Washabiki wa Real Sociedad watakuwa walishangazwa namna timu yao ilivyoelekea kumaliza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Celta Vigo jumamosi usiku kwani timu yao ni miongoni mwa vilabu vilivyopoteza alama nyingi msimu huu hasa katika dakika kumi na tano za mwisho. Hili lilidhihirika tena pale Nolito aliposawazisha dakika sita kabla ya kumalizika pambano hilo.



hata kocha wao David Moyes alikiri hilo pale aliposema “tulikuwa tukimiliki wakati tulipokuwa tukiongoza 1-0 lakini hatukuweza kutengeneza nafasi”. “hii ni pambano la nne mpaka tano tunatokewa na hali hii, inasikitisha kwani nilihitaji tupate bao lingine la pili, la tatu na hata la nne lakini hatuonkani kuwa na hali hiyo. Tunapaswa kujaribu na kufunga magoli mengi kadri tutavyoweza.”



ni wazi meneja Moyes atahitaji kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo kwani si tu pointi nane walizopoteza katika michezo hiyo zingewafanya kuwa wanane katika msimamo bali pia zimewaacha katika hali mbaya na hatari ya kuangukia timu zilizo katika hatari. Kitakwimu klabu hiyo chini ya Moyes imeongoza katika michezo nane kati ya kumi na moja lakini ni mara moja tu wamefanikiwa kupata bao la pili na ni mara tatu tu wameibuka na ushindi. Hiyo iliwafanya Celta Vigo kuungana na Levante na Granada kuambulia sare katika mechi ambazo Real walikuwa wakiongoza.



5.Hadhi ya Gaya inapanada wiki baada ya wiki



ni katika ushindi wa Valencia wa bao 2-1 dhidi ya Espanyol jumapili jioni ambapo kinda Jose Gaya alidhihirisha umahiri wake katika kulinda na kushambulia.Ni krosi yake ndiyo iliyochangia bao la kwanza lililofungwa nae Pablo Piatti, na hivyo kumfanya kupika mabao manne msimu huun.



Na hata ziliposalia dakika kumi huku ikionekana kama Espanyol wangesawazisha kufuatia gonga safi baina ya Lucas Vazquez, Sergio Garcia na Christian Stuani, mara Gaya alitokea na kuokoa ikiwa ni kwenye msitari wa lango. Huo ulikuwa ni mchango muhimu kwa Valencia ulochangia kujipatia ushindi wake wa kwanza ugenini katika mwaka 2015 (ikumbukwe sevilla walipoteza jumapili kwa kufungwa 2-1 na Getafe na hivyo sasa Valencia ni ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo. Hata hivyo wakati wakati mazungumzo na kinda huyo mwenye miaka 19 yakiendelea huku madrid ikidaiwa kutenga million 20 ni wazi mengi tutayasikia toka kwa kinda huyo.



N'DOYE AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO HULL CITY IKUA 2-0 ENGLAND


Mchezaji mpya wa Hull City, Dame N'Doye akipambana na Ciaran Clark wa Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usikunwa jana. Wenyeji, Hull City walishinda 2-0, mabao ya N'Doye na Nikica Jelavic.
 Home debutant Dame N'Doye runs away in celebration after scoring for his new Hull side to secure the three points against Aston Villa
 
 Hull City striker Nikica Jelavic scores the opener as his shot deflects off Kieran Clark and loops over Aston Villa keeper Brad Guzan
 
 Croatian Jelavic celebrates his seventh goal of the season at the KC Stadium to put Hull City 1-0 up against Aston Villa on Tuesday

QPR YAPATA USHINDI WA KWANZA UGENINI NA KUJINASUA MKIANI


Fer beats Liam Bridcutt to Matt Phillips's cross and powers a header past Pantilimon to open the scoring
Leroy Fer akipiga mpira kichwa mbele ya Liam Bridcutt kuunganisha krosi ya Matt Phillips kumtungua kipa Costel Pantilimon kuifungia QPR bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji Sunderland Uwanja wa Light usiku wa jana. Bao la pili la QPR lilifungwa na Bobby Zamora na ushindi huo wa kwanza ugenini msimu wote huu, unaitoa timu hiyo nafasi za mkiani.
 
QPR striker Bobby Zamora gave Chris Ramsey's side a two-goal lead just before half-time when he unleashed a brilliant volleyLL
 Costel Pantilimon could only stand and watch as Zamora's strike flew into the top corner to double QPR's lead at the Stadium of LightLL
 Leroy Fer wheels away in celebration after the Queens Park Rangers midfielder gives the visitors the lead against Sunderland

WAPINZANI WA YANGA KUWASILI KESHO

WAPINZANI wa Yanga SC, BDF XI wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Alhamisi kuelekea mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali, Kombe la Shirikisho la Afrika Jumamosi.
Yanga SC watacheza na BDF XI Jumamosi katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali, Kombe la Shirikisho wakihitaji ushindi mzuri kujiweka katika mazingira mazuri kabla ya mchezo wa marudiano baadaye Gaborone.
Na wapinzani wao hao ambao awali ‘walizusha’ eti wamejitoa, watawasili kesho Dar es Salaam huku ikiwa bado haijajulikana watafikia hoteli gani- kwa sababu ya taratibu mpya za Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

CAF sasa imeamua timu zijilipie malazi zinapokwenda kwenye mechi za ugenini baada ya kuwapo malalamiko timu ngeni kupatiwa hoteli duni miaka ya nyuma.
Yanga SC imeweka kambi katika hoteli ya Tansoma, eneo la Gerezani, Dar es Salaam tangu juzi kujiandaa na mchezo huo. 
Refa wa mchezo huo atakuwa Thierry Nkurunziza, wasaidizi wake Ramadhani Nijimbere namba moja, Herve Kakunze namba mbili na mezani George Gatogato, wote wa Burundi wakati Kamisaa atakuwa Joseph Nkole wa Zambia.
Kiingilio cha chini kabisa katika mchezo huo kitakuwa Sh. 5,000, wakati viingilio vingine vitakuwa Sh 10,000, 15, 000, 20, 000 na 30,000.

MAGAZETI YA MICHEZO LEO

BABA’AKE CHEKA AANGUA KILIO

NA DANSTAN SHEKIDELE/Morogoro
WATOTO wa bondia bingwa wa dunia anayetambuliwa na shirikisho la WBE, Francis Cheka aliye gerezani, wamemliza babu yao, Boniface Cheka ambaye ni baba mzazi wa mwanamasumbwi huyo wakati alipowatembelea nyumbani kwao, kwa mara ya kwanza tangu kutolewa kwa hukumu hiyo wiki mbili zilizopita.
Baba wa bondia Francis Cheka Boniface Cheka akiwa mwenye huzuni.
Mzee huyo ambaye makazi yake yako Dar es Salaam alifika mjini hapa kwa mara ya kwanza tangu mwanaye ahukumiwe, akiwa ameongozana na ujumbe kutoka Shirikisho la Ngumi la TPBO chini ya Rais wake, Abdalah Ustaadh.
Ujumbe huo ulifika mjini hapa Jumapili iliyopita na kwenda moja kwa moja katika gereza la Manispaa alikofungwa bondia huyo, ambako baada ya kumsalimia, walikwenda nyumbani kwake, ambapo baada ya kuwaona watoto na mkewe, mzee huyo naye alijikuta akishindwa kujizuia na hivyo kuangua kilio.
Mzee Boniface Cheka akiwa na ndugu zake.
Awali wakiwa gerezani hapo, msafara huo ulishuhudia umati mkubwa wa mashabiki waliofika kwa ajili ya kumuona bondia huyo kipenzi chao, aliyefungwa kwa kosa la kumpiga ngumi meneja wa baa yake. Hata hivyo, wengi wa watu hao walikataliwa kumuona.
Rais wa TPBO, Ustaadh, alisema walikuja mjini hapa wakiwa na mwanasheria wao, ambaye amewaambia kuwa watalazimika kwanza kufika mahakamani ili kujua hatua za kuchukua, katika harakati za kutaka kumtoa hatiani, bondia huyo aliyekuwa kipenzi cha wengi.


HII INAHUSU USAJILI WA MARCO REUS

 

 Marco Reus amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Dortmund mpaka 2019 - akizitosa timu kadhaa zilizokuwa zikitajwa kumuwania ikiwemo Arsenal, Madrid, Chelsea na City.

BALOTELLI AIBEBA LIVERPOOL JANA

Timu ya Liverpool jana imeibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Totenham Hotspur, magoli ya Liverpool yalifungwa na  Lazar Markovic dakika ya 15, Gerrard dakika ya 53 na Balotelli dakika ya 83 na magoli ya Totenham yalifungwa na Kane dakika ya 26 na Dembele dakika ya 61.

MSHAMBULIAJI MARIO BALOTELLI AMEFUNGA BAO LA TATU NA KUIWEZESHA LIVERPOOL KUIBUKA NA USHINDI WA MABAO 3-2.
BALOTELLI ALIYEKUWA AKISAKAMWA KWA KUTOFUNGA, AMEPACHIKA BAO HILO KATIKA DAKIKA YA 83 NA KUAMUA UBISHI WA MECHI HIYO BAADA YA KUWA KILA TIMU IMEFUNGA MABAO MAWILI.
LICHA YA KUFUNGA BAO HILO MUHIMU KWA LIVERPOOL NA KWAKE PIA, BAADA YA MECHI, BALOTELLI HARAKA ALIKIMBIA VYUMBANI.





ARSENAL WAPAA TOP 4



ARSENAL IMEKWEA HADI NAFASI YA NNE KATIKA MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND BAADA YA KUSHINDA KWA MABAO 2-1 DHIDI YA LEICESTER CITY.
SHUKRANI KWA BEKI KISIKI KOSCIELNY ALIYEFUNGA BAO LA KWANZA KABLA YA THEO WALCOTT KUFANYA KAZI YAKE KWA UHAKIKA ZAIDI NA KUFUNGA BAO LA PILI.

JULIO AIPANDISHA MWADUI VPL, AICHAPA POLISI TABORA 2

IMG-20150210-WA0049
Na. Richard Bakana, Dar es salaam
Timu ya Mwadui FC kutoka Mkoani Shinyanga leo imefanikiwa kujihakikishia kiganjani tiketi ya kutinga kunako ligi kuu ya Soka Tanzania bara Msimu wa 2015/2016 baada ya kuichapa Polisi Tabora kwa jumla ya mabao 2-0.
Kupanda kwa Kikosi hicho kinacho nolewa na Kocha wa Zamani wa Simba SC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio Albeto’ inafanya Mkoa wa Shinyanga kufikisha idadi ya Timu mbili zinazocheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ikiungana na Stand United ‘Watoto wa Mjini’.
Mchezo huo ulipata fursa ya kutazamwa na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa TFF akiwemo Mkurugenzi mkuu wa Mashindano ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Bwana Boniface Wambura.
IMG-20150210-WA0048
Kufatia ushindi huo Mwadui wanakuwa wamefikisha Pointi 43 mbele ya Toto Afrika ambao kabla ya mchezo wa leo dhidi ya Geita Gold SC ambao umevunjika kufatia vurugu na Mwamuzi kupokea kipigo, walikuwa na pointi 39 mbele ya JKT Oljoro na Polisi Tabora waliokuwa na alama 38.
 Mwaka jana Julio alitaka kuipandisha timu hiyo ligi kuu lakini kufatia mambo kadha wa kadda ndani ya TFF ikiwemo kuchelewa kutoa uamuzi wa nini kifanye baada ya mchezo kati yao na Stand United kuvunjika hari iliyopelekea Kushindwa kutinga VPL na Stand United kuchukua nafasi hiyo.
Hadi sasa Stand United ipo nafasi ya pili kutoka mkiani yaani ya 13 ikiwa na pointi 11 mbele ya Tanzania Prisons inayokamatilia mkia ikiwa na pointi 10 katika ligi kuu ya Tanzania bara
IMG-20150210-WA0047
IMG-20150210-WA0046