Mtandao wa ESPN umeainisha namna ambavyo bosi Diego Simeone na klabu yake ya Atletico Madrid wanavyoweza kuipiku madrid kwa mara nyingine katika mbio za ubingwa wa ligi kuu ya hispania maarufu kama La Liga. Kwa mujibu wa mtandao huo kuna mambo matano ya kutafakari kufuatia kufungwa kwa Real Madrid sambamba na ushindi wa goli 5-2 wa Barcelona.
1.Madrid wamejipa shida
Akizungumza mara baada ya kumaizika kwa pambano la jumamosi walilofungwa 4-0 ugenini Vicente Calderon, kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti alikiri kwamba matokeo waliyopata walistahili huku akisema “lazima tuwe na utulivu na kutafakari kwanini tumepatwa na hali hii lazima tubadilike.”
Hii ilikuwa ni mwenendo mbovu zaidi kwa madrid ambao walikuwa wamefunga katika kila mchezo wa La Liga msimu huu waliambulia kulenga lango mara moja tu katika dakika zote 90 tena kupitia mchezaji aliyeingia kipindi cha pili Asier Illarramendi.
Hali hiyo ni kitu ambacho hakikutarajiwa na kwa timu kama madrid yenye nyota wa safu ya ushabuliaji wa gharama kubwa. Ikumbukwe mpaka kufikia kipindi cha Christimas miamba hiyo ilikuwa imeshinda michezo 22 katika michuano mbalimbali huku ikiwa na wastani wa kufunga goli 3.25 kwa mchezo uwezo ambao umeshuka mpaka 1.88.
Hata wastani wa magoli wa Nyota wao mahiri Cristiano Ronaldo umeshuka toka 1.5 mpaka 0.57 amekiri kuwa suala lao loa kufungwa linahusisha mwili na akili. “Timu haipo sawa si kimwili si kiakili” alisema Ronaldo.
Naodha huyo wa Ureno alibainisha kuwa wamesikitika kuwaumiza washabiki wa klabu hiyo pamoja na jopo la wataalamu wa klabu hiyo na hata wachezaji wenzao hasa ikizingatiwa ushirikiwao katika hafla ya nyota huyo kutimiza miaka 30 ilomalizika jumamosi alfajiri. Ni kama vile pambano hilo la wapinzani halikupewa uzito unaostahili na hivyo ni wazi bosi wa klabu hiyo (Ancelotti) atahitaji kufanya kazi kuwarejesha mchezoni.
2.Kukaribiana na klabu ya Barcelona ni hatari
Mara ya mwisho Real madrid walipopoteza katika la La liga mapema mwezi Januari mwaka huu, wapinzani wao Barcelona walishindwa kunufaika na hali hiyo baada ya kukubali kichapo toka kwa Real Sociedad, ni wakati ambao hali haikuwa shwari klabuni barcelona huku minong’ono kadha wa kadha ikitawala.
Hata hivyo tangu hapo wapinzani wao wameikmarika na hata jumapili katika pambano dhidi ya Athletic Bilbao ni wazi walikuwa katika ubora wao huku wakiwaacha wapinzani wao wakihangaika bila mafanikio.
Na hata mchezaji wao mahiri Lionel Messi alikuwa yule wa ubora wa hali ya juu katika klabu ya Barcelona. Katika pambano hlo muargentina huyo alihusika katika mabao yote matano, akifunga moja na kupika mengine ikiwemo moja ya pasi bora za mwisho msimu huu alipotengeneza bao la Pedro Rodriquez.
Barca walitikiswa kunako dakika tano za mwanzo lakini hata hivyo walipambana na kuonesha umahiri wao katika pambano hilo wakashind 5-2 huku kiwango walichokionesha kikiwa miongoni mwa viwango bora kabisa msimu huu. Ukitizama walivyocheza ni wazi matatizo baina ya Luis Enrique na vijana wake yametulia kiasi maana Barca wameshinda michezo tisa mfululizo katika michuano mbalimbali huku wakifunga goli 32 na kuruhusu goli 7 pekee. Ni wazi ndo wana nafasi kubwa zaidi ya kutwaa taji hilo kwa sasa
3.Atletico pia wanaweza kucheza
Moja ya kibwagizo ambacho kimekua kikifuatia ushindi wa Atletico Madrid ni namna vijan ahao wa Diego Simeone wanavyotumia nguvu, mabavu na hata uteegemezi wa mipira iliyokufa kujipatia ushindi na hivyo hata kama watashinda si timu kubwa utakuwa umebadilika.
katika mchezo wa jumamosi walionesha kiwango cha hali ya juu hususani katika kipindi cha pili wakiongozwa na umahiri wa washambuliaji Arda Turan na Antoine Griezman huku kila goli likitokana na gonga za hapa na pale.
hata baada ya pambano kocha Simeone alisema kuwa kuwa aliamua kuchagua kikosi hicho cha wachezeshaji ambacho hususani wale ambao wangeweza kupasiana kwa haraka. “tuliitaji kuchezea mpira na katika hilo tulifanikiwa”
4.Real Sociedad “bado wamo”
Washabiki wa Real Sociedad watakuwa walishangazwa namna timu yao ilivyoelekea kumaliza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Celta Vigo jumamosi usiku kwani timu yao ni miongoni mwa vilabu vilivyopoteza alama nyingi msimu huu hasa katika dakika kumi na tano za mwisho. Hili lilidhihirika tena pale Nolito aliposawazisha dakika sita kabla ya kumalizika pambano hilo.
hata kocha wao David Moyes alikiri hilo pale aliposema “tulikuwa tukimiliki wakati tulipokuwa tukiongoza 1-0 lakini hatukuweza kutengeneza nafasi”. “hii ni pambano la nne mpaka tano tunatokewa na hali hii, inasikitisha kwani nilihitaji tupate bao lingine la pili, la tatu na hata la nne lakini hatuonkani kuwa na hali hiyo. Tunapaswa kujaribu na kufunga magoli mengi kadri tutavyoweza.”
ni wazi meneja Moyes atahitaji kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo kwani si tu pointi nane walizopoteza katika michezo hiyo zingewafanya kuwa wanane katika msimamo bali pia zimewaacha katika hali mbaya na hatari ya kuangukia timu zilizo katika hatari. Kitakwimu klabu hiyo chini ya Moyes imeongoza katika michezo nane kati ya kumi na moja lakini ni mara moja tu wamefanikiwa kupata bao la pili na ni mara tatu tu wameibuka na ushindi. Hiyo iliwafanya Celta Vigo kuungana na Levante na Granada kuambulia sare katika mechi ambazo Real walikuwa wakiongoza.
5.Hadhi ya Gaya inapanada wiki baada ya wiki
ni katika ushindi wa Valencia wa bao 2-1 dhidi ya Espanyol jumapili jioni ambapo kinda Jose Gaya alidhihirisha umahiri wake katika kulinda na kushambulia.Ni krosi yake ndiyo iliyochangia bao la kwanza lililofungwa nae Pablo Piatti, na hivyo kumfanya kupika mabao manne msimu huun.
Na hata ziliposalia dakika kumi huku ikionekana kama Espanyol wangesawazisha kufuatia gonga safi baina ya Lucas Vazquez, Sergio Garcia na Christian Stuani, mara Gaya alitokea na kuokoa ikiwa ni kwenye msitari wa lango. Huo ulikuwa ni mchango muhimu kwa Valencia ulochangia kujipatia ushindi wake wa kwanza ugenini katika mwaka 2015 (ikumbukwe sevilla walipoteza jumapili kwa kufungwa 2-1 na Getafe na hivyo sasa Valencia ni ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo. Hata hivyo wakati wakati mazungumzo na kinda huyo mwenye miaka 19 yakiendelea huku madrid ikidaiwa kutenga million 20 ni wazi mengi tutayasikia toka kwa kinda huyo.
0 maoni:
Post a Comment