SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 2, 2015

USIKU WA ZARI ALL WHITE PARTY ULIVYOFANA NDANI YA MLIMANI CITY JIJINI DAR

Diamond Platnumz akimbusu mpenzi wake Zari katika usiku wa Zari All White Party ndani ya Mlimani City.
Zari na Diamond katika pozi ndani ya Mlimani City.
Zari na Diamond wakati wakiingia ukumbini.
Wasanii wa Yamoto Band wakiwa wametulia tayari kwa shoo.
Mpiga Picha Mkuu wa Global Publishers, Richard Bukos (kati) akipozi na watangazaji Sauda Mwilima wa Star TV(kulia) na Khadija Shaibu 'Dida' wa Times FM.
Wanausalama wakiwaondoa baadhi ya watu waliokosa tiketi.
Baadhi ya mabango waliyokuwa nayo mashabiki wa Diamond.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)

HIKI NDIO KITUO KITAKACHO RUSHA LIVE MECHI YA YANGA LEO

AZAM TV, Televisheni namba moja Tanzania ya michezo na burudani- leo inatarajiwa kuonyesha moja kwa moja mchezo kati ya Yanga SC dhidi ya wenyeji Etoile du Sahel nchini Tunisia.
Mchezo huo utaanza Saa 1:00 usiku kwa Saa za Kaskazini mwa Afrika na Saa 3:00 usiku kwa Saa za Afrika Mashariki Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse na Azam TV wataanza Saa 2:00 kutoa maelezo ya utangulizi kupitia chaneli ya Azam Two. 
Etoile du Sahel wamethibitisha kufikia makubaliano na Azam TV kurusha mchezo huo ‘Live’ leo.  
Aidha, kamera za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) zimezuiwa Uwanja wa Ndege wa Tunis. 
Watangazaji wa TBC wakiongozwa na Enock Bwigane walizuiwa kutoka na kamera na wakalazimika kuziacha kwenda kuripoti mechi hiyo.
Hakuna tatizo kwa Waandishi wa Habari kuingia Tunisia, bali kamera za video ndizo zimezuiwa na wakati wafanyakazi wa TBC wanarejea nyumbani watakabidhiwa vifaa vyao.

HII NDIO KAULI YA MSUVA KUELEKEA MECHI YA ETOILE


NgassanaMsuva1
WINGA wa Dar Young Africans, Simon Happygod Msuva amefurahia hali ya hewa ya Tunisia na kusema wanaweza kuwafunga Etoile du Sahel.
Mchezo huo wa marudiano wa hatua ya 16 ya kombe la shirikisho utapigwa kesho jumamosi katika dimba la Olympique de Sousse katika mji wa Sousse kuanzia majra ya saa 3 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.
Katika mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam, Young Africans ilitoka sare ya bao 1- 1 na Etoile  na mshindi wa jumla atacheza hatua ya mtoano (Play-off) dhidi ya timu zitakazokuwa zimetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa (CL) kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi.
kuelekea katika mechi Msuva amesema: “Sisi tunashukuru Mungu hali ya hewa iko vizuri, tunaamimi kesho tunaweza kufanya chochote. Kama wao waliweza kupata goli moja kwetu nasisi tunaweza kupata kwao”.
Msuva ndiye kinara wa mabao Yanga na ligi kuu Tanzania bara kwa sasa akiwa ameshafumania nyavu mara 17 akifuatiwa na mchezaji mwenzake wa Yanga Amissi Tambwe mwenye magoli 14.

KAVUMBAGU APONDEA TUZO ZA KILA MWEZI VPL, ADAI ZINAENDESHWA KWA KUJUANA

kavumbagu 222Na. Richard Bakana, Dar Es Salaam
Mshambuliaji wa klabu ya Azam FC, Didier Kavumbagu, amefunguka ya moyoni juu ya muenendo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambayo inaelekea ukingoni na kusema kuwa inaendeshwa kwa kujuana zaidi.

Akizungumza na Shaffihdauda.com Mshambuliaji huyo ambaye alijiunga na Azam FC mwaka jana akitokea Yanga SC, amesema kuwa kutokana na mchango ambao anauonyesha katika klabu yake hasa pale mwanzoni mwa ligi, alikuwa anastahili kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba 2014, lakini anadai kuwa kujuana ndio kulipelekea akanyimwa na kupewa mchezaji wa Mbeya City Antony Matogolo licha ya timu yake kufanya vibaya kwa wakati huo.
“Unaweza kusema ligi inaenda kwa kujuana, ilitakiwa nipewe tuzo ya mchezaji bora mwezi Januari lakini akapewa wa Mbeya City, Ukiangalia Muda huo nilikuwa ninafunga katika kila mechi huku timu yangu ikifanya vizuri lakini nikanyimwa akapewa yeye wakati timu yake ilikuwa inafanya vibaya” Amesema Didier Kavumbagu.

Wadhamini wakuu wa Ligi hiyo ambao ni kampuni ya Simu za mkononi Vodacom, Mwaka jana walikuja na wazo la kutoa tuzo kwa mchezaji bora wa mwezi kufatia kazi nzuri na mchango wao katika timu, zoezi ambalo lilipokelewa vizuri na kusimamiwa vyema na TFF wakishirikiana na Bodi ya ligi ambao waliteua watu maalumu (Makocha) ili kuhakikisha mshindi anapatikana kwa haki na kwakuzingatia vigezo husika, Kigezo kimojawapo kikiwa ni Mchezaji awe ameisaidia timu yake kufanya vizuri ndani ya mwezi husika.
Hadi Matogolo anakabidhiwa tuzo hiyo ikiwa ni kabla ya Mbeya city kumpeleka Panone FC kwa mkopo, Wagonga Nyundo hao wa jiji la Mbeya tayari walikuwa wamepoteza michezo minne mfululizo huku Azam FC ikichanja mbuga katika kutetea Ubingwa ilioupata msimu uliopita bila kufungwa pamoja na Mtibwa Sugar, Tukio ambalo lilifanya wachambuzi wengi wa soka Tanzania kushangaa na kujiuliza ni vigezo gani ambavyo TFF na Bodi ya Ligi walitumia hadi kumpatia mchezaji huyo tuzo na kuwaacha watu kama Kavumbagu na Ame Ally ambao kwa muda ule ndio waliokuwa wanafanya vizuri sana.

Michezo ambayo Mbeya City ilipoteza Antony Matogolo akicheza ni dhidi ya Ruvu Stars zilitoka sare tasa Septemba 20, Septemba 27 Mbeya City 1-0 Coastal Unon. Oktoba 4, Ruvu Shooting 0-0 Mbeya City. Oktoba 18, Mbeya City 0-1 Azam FC. Oktoba 26, Mbeya City 0-2 Mtibwa Sugar. pamoja na ule mchezo wa mwanzoni mwezi Novemba ambapo City walikutana na JKT Mgambo wakapoteza kwa bao 2-1 Mkwakwani Tanga.

Kavumbagu ameiambia Shaffihdauda.com kuwa kama kweli haki na sheria zote zingefatwa basi yeye ndio angeibuka kinara wa tuzo hiyo ambayo inathamani ya Pesa za Kitanzania Milioni Moja.

Mbali na Antony Matogolo kunyakua tuzo hiyo baadhi ya wachezaji wengine ambao wamewahi kuchukua tuzo hiyo ni pamoja na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wa Azam FC (Oktoba), Rashid Mandawa wa Kagera Sugar (Novemba), Mahundi (Desemba), Said Bahanunzi wa Polisi Moro (Januari) na Godfrey Wambura wa Coastal Union (Februari).

PLUIJM ATANGAZA KIKOSI KITAKACHOIVAA ETOILE DU SAHEL, LEO


Kocha Hans van der Pluijm ametangaza kikosi kitakachoanza leo Jumamosi dhidi ya Etoile du Sahel.

Mholanzi huyo ametangaza kikosi hicho baada ya mazoezi ya mwisho.
KIKOSI:
1) Ally mustapha
2) Mbuyu Twite
3) Oscar Joshua
4) Kelvin Yondan
5)  Nadir Haroub
6) Saidi makapu
7) Saimon msuva
8) Salum Telela
9) Hamis Tambwe
10) Mrisho ngasa
11) Pah Sherman

MAYWEATHER AMZIDI UZITO PACQUIAO, LAKINI IKO POA TU KWA WELTER

Mayweather poses on the scale at the MGM Grand and was inside the limit by just one pound

Bondia Floyd Mayweather Jr akiwa kwenye mzani wakati wa kupima uzito ukumbi wa MGM Grand usiku wa kuamkia leo kuelekea pambano lake na Manny Pacquiao usiku wa kuamkia kesho kwenye ukumbi huo. Mayweather 'alibalanasi' uzito wa pambano (Paundi za 147 za Welter), tena akiwa amepungua Paundi moja. 
Pacquiao flexes his muscles on the scales and came in at  two pounds under the weight limit
Pacquiao naye amepungua Paundi mbili za uzito kamili wa Welter